Saturday, December 29, 2012

Mwenyekiti CCM-Msiyumbe na maneno ya uchochezi

 File:Ccmlogotz.png
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Mathayo Mwangomo, amewataka wananchi wilayani humo kutokukubali maneno ya uchochezi yanayodhoofisha maendeleo na juhudi za Serikali katika kutatua matatizo ya wananchi wake.
Mwangomo alitoa kauli hiyo wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ruiwa wilayani humo.
Alisema kuwa, hivi sasa Chama cha Mapinduzi ambacho kipo madarakani kinatekeleza sera zake hivyo wananchi hawana sababu za kuendelea kusikiliza maneno ya kubeza maendeleo yanayofanywa na chama hicho.
“Wananchi mnatakiwa kutokubali maneno ya uchochezi yanayotolewa na wanachache ambayo msingi wake ni kudhoofisha maendeleo na juhudi za Serikali katika kutatua matatizo yenu,”alisema Mwangomo.
Alisema kuwa, CCM imefanya mambo mazuri katika jamii ikiwa ni pamoja na kujenga shule za msingi na sekondari za kata, ambazo zimeongeza kiwango cha elimu nchini.
Mbali na kuwaleeza hivyo wananchi hao, Mwenyekiti huyo pia alipokea kero za wananchi wa kata hiyo ya Ruiwa ikiwa ni pamoja na ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh60 milioni zilizochangwa na wananchi hao kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Gwili ambazo zinadaiwa kutafunwa na diwani wa kata hiyo, Alex Mdimilage, anayedaiwa kumtorosha mhasibu wa shule hiyo na kutoroka na fedha za wananchi zaidi ya Sh27milioni na kuiacha shule hiyo ikiwa haina chochote.
Sambamba na hilo wananchi hao pia walilalamikia vitendo vya diwani wao kuwa, amekuwa kikwazo cha maendeleo ya kata hiyo kutokana na uwajibikaji wake mbovu uliopelekea wananchi wengi kukihama chama hicho.
Akijibu tuhuma hizo mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya, Diwani wa kata ya Ruiwa , Alex Mdimilage alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa mambo yote yanayozungumzwa dhidi yake ni chuki za kisiasa na kwamba kwa kipindi chake hiki amesimamia miradi mbalimbali kijijini hapo na kata kwa ujumla.
Mwenyekiti wa CCM huyo alikiri kuwepo kwa viongozi wazembe wilayani humo, hivyo amewataka viongozi wanaohusika na tuhuma hizo kujiengua mapema na hawatasubiri Takukuru na Polisi na kero zote zilizowasilishwa na wananchi atazifanyia kazi.

TUNDULISU ASEMA PROF; SHIVJI AMEPOTOKA KUKOSOA KESI YA LEMA


mwanazuoni wa siku nyingi nchini, Profesa Issa Shivji  Mwananchi


Fredy Azzah
HATUA ya mwanazuoni wa siku nyingi nchini, Profesa Issa Shivji kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufani Tanzania iliyomrejeshea ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema imemtia matatani na baadhi ya watu wanasema gwiji huyo wa sheria “huenda amenukuliwa vibaya au hajasoma hukumu husika.”
Jana Wakili wa Lema, Tundu Lissu, alimkosoa Profesa Shivji pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Francis Stolla akisema wanasheria hao wamepotoka katika matamshi yao ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufani.
Matamshi ya Shivji pia yaliiteka mijadala katika mitandao ya kijamii ya Jamii Forums, Mabadiliko na Facebook ambako wachangiaji  walikuwa wakivutana huku baadhi yao wakisema wazi kwamba msomi huyo amekosea huku wengine wakimtetea kwamba yuko sahihi.
Akizungumza na gazeti hili jana kutoka Songea mkoani Ruvuma, Lissu alipinga vikali hoja zilizotolewa na Profesa Shivji pamoja na Stolla, akisema kuwa hazina mashiko na zinaweza kutolewa tu na mtu ambaye hakufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.
Juzi Profesa Shivji na Stolla walinukuliwa wakiikosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni Lema wakisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao Nathalia Kimaro, inapingana na sheria.
Lissu katika maelezo yake alisema uamuzi wa mahakama katika kesi ya Lema umejenga upya msingi bora wa matumizi ya vyombo vya uamuzi, kwani kesi nyingi za kupinga matokeo ya ubunge, zimekuwa zikifunguliwa na watu ambao wamekuwa wakitumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha.
Akizungumza na Mwananchi, Lissu alisema hoja hizo hazina mashiko na kuwa ile iliyotolewa na Profesa Shivji inatokana na msomi huyo kuzungumza kitaalamu bila kuangalia mazingira halisi ya siasa za Kitanzania.
Lissu alisema mahakama ya rufani haikupiga marufuku wapiga kura kufungua kesi za kupinga ila iliwataka tu kufanya hivyo pale haki zao zinapokiukwa.
“Kwanza siyo kweli kwamba mahakama imepiga marufuku wapiga kura kufungua kesi, ilisema watafanya hivyo pale ambapo haki zao zimevunjwa, haki zenyewe ni kupiga kura, kura zao kutohesabiwa ama suala jingine litakalomnyima kupiga kura, hizo ndiyo haki za mpiga kura,” alisema na kuongeza:
“Sasa mwalimu wangu, Profesa Shivji yeye anatazama tu kwa jicho la kitaalamu na kusema haki za binadamu zimekiukwa, kwa muda wanasiasa, matajiri na CCM wamekuwa wakiwatumia wananchi kuwapinga wabunge wa upinzani.”
Uchambuzi wa Lissu
Alitoa mfano akisema katika uchaguzi wa 1995, Dk Willibrod Slaa alishinda ubunge na watu wanaojiita wananchi walifungua kesi kupinga ushindi huo, mwaka 2000 wakampinga tena na hata 2005.
Alisema 1995 Makongoro Nyerere aliposhinda ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kupitia NCCR- Mageuzi, watu wanaojiita wananchi walifungua kesi ambayo matokeo yake yalikuwa mbunge huyo kupoteza kiti chake.
Lissu alisema 2005 aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe alifunguliwa kesi na watu waliojiita wananchi ambao mwisho wake walishindwa.
“Hawa wananchi ambao wanafungua kesi zenye mawakili wanaolipwa mamilioni ya fedha ni watu ambao hata fedha za kununua viatu hawana,  hawa waliokuwa wakimpinga Marehemu Wangwe nikiwa mahakamani niliwauliza kama wanawajua mawakili waliokuwa wanawatetea, walikuwa hawawajui.
Nikawauliza kama wamewahi kufika Dar es Salaam wakasema hapana, sasa sijui waliwapataje wale mawakili,” alisema na kuongeza:
“Wote hawa  wanakuwa ni watu wanaotumiwa. Mwaka huu kati ya wabunge wote 25  Chadema tulioshinda, 14 tulifunguliwa kesi na kati ya hizi 12 zimefunguliwa na watu wanaojiita wananchi, hii ni kutumiwa,” alisema.
Alisema mara baada ya uchaguzi mwaka 2010 aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliandika waraka kuwataka makatibu wa chama hicho kufungua kesi kwa majimbo yote ambayo chama hicho kiliangushwa jambo alilosema ndilo liliwasukuma kuwatumia wananchi.
Kuhusu hoja kuwa mahakama hiyo ya rufani imeingilia kazi ya kutunga sheria badala ya kuzitafsiri na kuwa imepingana na sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Chediel Mgonja ya mwaka 1980, Lissu alisema hazina mashiko.
“Hiyo ni hoja ya kipuuzi. Hiyo sheria ya kuwa mwananchi yeyote ana haki ya kufungua kesi kuwa imetenguliwa na Mahakama ya Rufani, hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria ukimuuliza atakwambia kuwa, amri ya Mahakama Kuu wala ya Mahakama ya Rufani yenyewe haiwezi kuizuia mahakama hiyo ya juu kabisa nchini kufanya uamuzi wake,” alisema.
Akizungumzia hoja ya Stolla kwamba mahakama iliibua jambo jipya la kuhoji kama wajibu rufani walikuwa wapiga kura ama la, alisema Rais wake huyo hana hoja, kwani wakili wa walalamikaji aliibua hoja kama hiyo na alipoulizwa na mmoja wa majaji kuwa “Hata sisi hatuwezi kulizungumzia suala hili, alishindwa kujibu akawa anajikanyaga tu,” alisema.
Aliongeza: “Kwenye rufaa ya kwanza mahakama inaruhusiwa kuibua chochote, sasa hizo ni hoja zinazotolewa na watu ambao marafiki zao wa CCM wameshindwa sasa wanavaa joho la utaalamu kutoa hoja kama hizi zisizo na mashiko.”
Shivji na Stolla
Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
“Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura,” alisema Profesa Shivji.
Kwa upande wake, Stolla alisema: “Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutopendezwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge’ (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani.
Aliongeza: “Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, ni sababu gani nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?”
Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.
Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha ya matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa wadhifa huo kwa tiketi ya CCM, Dk Batilda Buriani.

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Hata hivyo, alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kukubali rufaa yake.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.

Friday, December 28, 2012

MADAKTARI 30 WASIMAMISHWA KAZI, 289 WAPIGWA MKWARA


Madaktari wakiwa katika chumba cha upasuaji. 


BARAZA la madaktari Tanganyika limewasimamisha kwa muda madaktari 30, kutoa onyo kwa madakari 289 na kuwafutia mashtaka madaktari 49 baada ya kupitia malamamiko ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufuatia mgomo wa madaktari uliotokea Juni 23 hadi 28 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja imeeleza kuwa Baraza lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo.
Alisema mashtaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria ni madaktari wanne na mashtaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza ni madaktari 22.
“Wizara inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za  Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la Madaktari,”aliseleza Mwamaja na kuongeza
“Wizara pia imeridhia kuwapa madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa.”
Hata hivyo alisema fursa hiyo haitawahusu madaktari wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
Alisema kwa taarifa hiyo madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii barua kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa usajili  na kuruhusiwa kuendelea na mafunzo kwa vitendo.
Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu ili kupewa
barua zao kulingana na Adhabu walizopewa.

WANAFUNZI 6,838 WAMEKOSA NAFASI YA KUJIUNGA SEKONDARI JIJINI ARUSHA

 

JUMLA ya wanafunzi 6,838 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu, mkoani Arusha, wamekosa nafasi ya kujiunga na masomo ya Sekondari kutokana na uhaba wa nyumba vya madarasa 172 .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Evelyine Itanisa alitoa taarifa hiyo, juzi katika kikao cha kamati ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 mkoani Arusha.
Itanisa alisema wanafunzi hao, wanatoka  katika halmashauri sita za mkoa Arusha na ni halmashauri moja tu ya Karatu ambayo imeweza kuwachukua wanafunzi wote waliofaulu mwaka huu.
Alisema  katika jiji la Arusha  wanafunzi 2420 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba  vya madarasa 61, Ngorongoro wanafunzi 441 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba 11.
Alisema   Halmashauri ya Arusha vijijini  wanafunzi 1880 wameshindwa kujiunga na sekondari kutokana na  uhaba wa vyumba 47.
“Pia Halmashauri ya Longido kuna wanafunzi 140 ambao wanahitaji madarasa manne, Meru wanafunzi 1,159 wakiwa na mahitaji ya vyumba 29, wilaya ya Monduli wanafunzi 807 wamekosa nafasi kutokana na kukosekana madarasa 20”alisema Itanisa.
Alisema kutokana na hali hiyo, ameziagiza halmashauri hizo sita za mkoa wa Arusha kuiga mfano wa halmashauri ya Karatu, kwa kuhakikisha zinajenga vyumba vya madarasa vya kutosha  ili kuhakikisha wanafuzi wote waliofaulu wanapata nafasi.
“Ili kuhakikisha watoto waliofaulu wote wanaendelea na sekondari, kila halmashauri inapaswa ihakikishe inakamilisha ujenzi wa madarasa kabla ya februari  mwakani “alisema Itanisa.
Hata hivyo, Katibu Tawala huyo alisema kiwango cha ufaulu kwa Mkoa wa Arusha, kimekuwa kikipanda kwa miaka mitatu sasa mfululizo ambapo mwaka huu jumla ya wanafunzi 26,464 wamefaulu mitihani kati ya wanafunzi 37,493 waliofanya mitihani.
“Matokeo haya yanafanya Mkoa wa Arusha uwe umefaulisha kwa asilimia 70.6 na waliofaulu ni wavulana 12,608 na wasichana 13,856”alisema Itanisa.

Thursday, December 27, 2012

MWANAFUNZI AFIA GESTI AKITOLEWA MIMBA



Wanafunzi wakielekea shule 

MWANAFUNZI  wa kidato  cha tatu katika shule ya Sekondari ya Tongoni nje kidogo ya jiji la  Tanga,  (jina tunalihifadhi) amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni alikopelekwa kutolewa mimba bila mafanikio.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe mwanafunzi huyo alikutwa amekufa juzi katika nyumba ya kulala wageni iliyopo barabara ya 21 jijini Tanga.
Mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kwamba mwanafunzi huyo aliingia saa 4.00 asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana mmoja wakakodi chumba.
 
“Baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye alituuliza kama wameingia mwanafunzi huyo na mwenzake, tulipomwonyesha chumba  walichoingia naye akakodi chumba cha jirani ndipo tukaona wote wakijifungia kwenye chumba kimoja,” alisema mhudumu.
Mhudumu huyo alisema baada ya muda wa saa moja, mvulana na mzee huyo wakaaga kwamba wanatoka huku wakisema kwamba msichana amebaki chumbani akiwa amepumzika. Akithibitisha habari hizi, Kamanda Massawe alisema taarifa ya tukio hilo ilitolewa na mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo cha Polisi cha Chumbageni Jijini Tanga.
“Tatizo ni kwamba nyumba hii ya wageni wahudumu wake hawakuwapa wageni hao daftari ili waorodheshe majina yao hivyo inakuwa vigumu  kuwafahamu,” alisema Kamanda Massawe na kufafanua kuwa alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja.
Kamanda Massawe alisema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kifo hicho.

ZANZIBAR;PADRI APIGWA RISASI, ALAZWA ICU


Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki Mpendae,Zanzaibar akipakizwa kwenye gari kupelekwa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar tayari kwa kusafirishwa kwenda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Dar es salaam kwa matibabu zaidi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Mjini Zanzibar juzi jioni. Picha Martin Kabemba. 

PADRI Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki, Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake juzi saa 1:45 jioni wakati akitokea kanisani.
Hili ni tukio la kwanza katika historia ya Zanzibar kwa kiongozi wa kanisa kushambuliwa wakati wa Krismasi, lakini ni tukio la pili kwa kiongozi wa dini kushambuliwa mwaka huu.
Hivi karibuni, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga alimwagiwa tindikali iliyomjeruhi vibaya usoni na kifuani na watu wasiojulikana. Shambulio hilo lilimlazimu kiongozi huyo kwenda kutibiwa India ambako ameambiwa anapaswa kuripoti hospitalini kila baada ya miezi sita.

Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa Mkenda ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mpendae, alipigwa risasi begani na shingoni na afya yake si nzuri.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed alisema jana kuwa majeraha hayo yamemsababishia kutokwa na damu nyingi.

Alisema baada ya shambulio hilo, Padri Mkenda alipelekwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Zanzibar. Hata hivyo, padri huyo alisafirishwa kwa ndege jana hadi Dar es Salaam ambako amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kamanda Aziz alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, lakini akabainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa alipigwa risasi baada ya watu hao kumshuku kuwa alikuwa na fedha za sadaka.

“Father Mkenda kitaaluma ni mhasibu na amekuwa akishika makusanyo ya fedha pale kanisani. Sasa huenda wahalifu hao waliona amechukua fedha na ndipo walipomfuata na kumpiga. Lakini hata hivyo, huo bado ni uchunguzi wa awali tu,” alisema Kamanda Aziz na kuongeza:

“Waliofanya tukio hili wamelifanya kwa madhumuni gani, ni swali gumu kujua sasa. Inawezekana kuna mambo mengine zaidi ya watu hao kutafuta fedha. Uchunguzi ukimalizika tutajua cha kufanya.”

Kamanda Aziz alisema walipata taarifa za tukio hilo saa 2:00 usiku na polisi walikwenda katika eneo hilo la Francis Maria anakoishi Padri Mkenda.

“Tulipofika tukakuta maganda mawili ya risasi za bastola na upande wa kulia wa kioo cha gari yake (padri) kuna damu katika viti vyake,” alisema Kamanda Aziz.

Alisema baadaye padri huyo alipelekwa hospitalini kwa ajili matibabu ambako madaktari walifanikiwa kumtoa mabaki ya risasi mwilini kabla ya jana kupelekwa Muhimbili.

“Tumempokea padri huyo saa 4:20 asubuhi leo (jana). Tulianza kumchunguza afya yake, baadaye kumfanyia uchunguzi kisha kumchukua kipimo cha CT Scan ili kubaini ilipo risasi hiyo,” alisema, mkurugenzi wa zamu katika hospitali hiyo, Agnes Mtawa.
Akizungumzia tukio hilo, Askofu Mkuu Msaidizi, Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa alisema kanisa linasikitishwa na kilichotokea kwani ni kitu ambacho jamii haikukitarajia na wanaviachia vyombo vya usalama vifanye kazi yake... “Sisi kama kanisa tunajitahidi kuhakikisha anapata matibabu yaliyo bora ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.”

Askofu huyo alisema viongozi wa dini wanachukua tahadhari kujilinda ingawa wanafahamu kuwa wahalifu hao nao wanajipanga kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Kwa upande wake, Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikana la Mkunazini, Zanzibar alisema: “Tukio hililimenisikitisha sana.” Alisema amepokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa tukio hilo ni mwendelezo wa mengine kadhaa ya kuwahujumu viongozi wa dini, Zanzibar.
Alisema tukio hilo ni miongoni mwa matukio ya kushtusha na yanayoashiria hali mbaya ya kiusalama katika Mji wa Zanzibar na kuwaomba viongozi wa Serikali kuchukua hatua za tahadhari haraka kunusuru hali hiyo.

“Ni busara Serikali ikachukua hatua sasa kwani hili siyo tukio la kwanza kuwahujumu viongozi wa dini. Katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Soraga aliwahi kukumbwa na mkasa wa aina hiyo pia,” alisema na kuongeza:

“Hii ni hali ya hatari katika nchi yetu na haipendezi kabisa kwa sababu inaashiria na kutishia usalama wa nchi. Sisi hatujawahi kushuhudia kitu kama hiki. Tumezoea Wazanzibari kusherehekea sikukuu kwa pamoja miaka yote. Krismasi tunasherehekea na wenzetu Waislamu na Idd El Haj tunasherehekea kwa pamoja bila ya tofauti za kidini sasa hili linatokea wapi sasa!”

Askofu Hafidh alisema kibaya zaidi ni tukio la Padri Mkenda kutokea katika kipindi ambacho kumekuwa na vipeperushi vilivyosambazwa na watu vikiwatisha watu wenye imani ya Kikristo.

“Tumeona hivi vipeperushi na kwa kweli tulikuwa na hofu, lakini ndiyo tunasema tunaelekea wapi katika maisha haya Zanzibar?” alihoji Askofu Hafidh.
Akizungumzia vipeperushi hivyo, Kamanda Azizi alisema jeshi lake halijaviona wala kuona mtu akivilalamikia na siku zote limekuwa likiimarisha ulinzi katika makanisa na misikiti siku za sherehe za kidini.

“Hakuna hata kanisa moja ambalo hatujaliwekea ulinzi wa kutosha. Tumejitahidi sana na pia kuna askari wetu wanaozunguka kuimarisha ulinzi kwa miguu na wengine wanazunguka kwa pikipiki katika maeneo yote. Sasa tunawaomba wananchi wasaidie kutoa taarifa wanapoona viashiria vya uvunjifu wa amani kwa sababu polisi hawawezi kumlinda mtu mmoja mmoja,” alisema.

Kuhusu uchochezi wa kidini, Kamanda Aziz alisema Jeshi la Polisi haliamini kwamba kuna uchochezi wa kidini... “Sisi hatuamini kwamba kuna kisasi kwa viongozi wa dini, tunachukulia hilo ni tukio la kihalifu.”

Msemaji wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Shaaban Simba alisema ingawa hajapata habari hizo kwa undani kwa kuwa yupo safarini, wanalilaani tukio hilo na kusema kuwa vyombo vya dola vitachukua hatua stahiki.

Tuesday, December 25, 2012

SAMATTA NA ULIMWENGU WAFUNGUKA JUU YA TUHUMA ZA KULINGA KUCHEZEA TAIFA STARS.



Kim Poulsen akiwatoa maelekezo kwa vijana wake Thomas Ulimwengu na mwenzake Mbwana Samatta mazoezini jijini Dar es Salaam
EDO KUMWEMBE
WASHAMBULIAJI wawili wa kimataifa wa Tanzania wanaokipiga TP Mazembe, Mbwana Samatta 'Poppa' na Thomas Ulimwengu wamevunja ukimya kuhusu madai kwamba wanaringa na wanaipuuza timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Mastaa hao walizomewa katika pambano la kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo lililopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa na Stars kushinda bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Ngassa.

Wakiongea kwa uchungu katika nyakati tofauti juzi Jumapili, Samatta na Ulimwengu ambao kitabia ni wakimya walitoa dukuduku lao katika mahojiano maalumu waliyofanya na Mwanaspoti huku kila mmoja akionyeshwa kukerwa na kitendo cha kuzomewa na mashabiki wa soka na kusisitiza kwamba wanaonewa na mashabiki kutokana na kutoambiwa ukweli kuhusu wao.

Maelezo ya Samatta
"Kaka ukweli ni kwamba mimi naumwa ingawa Watanzania hawataki kuelewa. Niliumia bega katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika tuliyocheza ugenini dhidi ya Power Dynamo ya Zambia.

Kama unakumbuka mechi ya marudiano pale Lubumbashi mimi hata sikucheza. Sasa wiki chache zilizopita tulikwenda Congo Brazzaville kucheza mechi ya kirafiki ambayo ilikuwa ni ya kuadhimisha kumalizika kwa vita nchini humo. Katika mechi nikajitonesha bega na mpaka sasa linanisumbua sana," anasema Samatta.

"Mwalimu (Kim Poulsen) nimeongea naye sana na amenielewa. Ameniambia mimi ni kijana mdogo kwa hiyo nikipata tatizo niliseme kwa haraka.

Na ametuambia mimi na Thomas kuwa kwa sababu sisi ni majeruhi basi tutaendelea kuwa chini ya uangalizi wa Daktari Mwankemwa.

Hivi ninavyokwambia sasa hivi naenda katika shamba la baba kule Vikindu kula embe, ikifika saa sita inabidi nirudi niende kwa Daktari Mwankemwa kufanya naye mazoezi.

Januari 6, mwakani tunahitajika katika kambi ya timu ya taifa. Kim kaniambia kuna mechi tatu za kirafiki.

Nikiwa fiti nacheza kama kawaida. Siwezi kucheza wakati sipo fiti jamani.

Nikicheza wakati siko fiti huwa nacheza kwa kiwango cha chini na watu wanasema mimi sio mzalendo, nikikaa nje kupisha watu walio fiti wanasema mimi sio mzalendo, sasa nifanyeje?� alihoji Samatta.

�Mechi yetu ya Zambia ilikuwa ya kirafiki tu, lakini si unakumbuka kuna mechi za maana kibao zinakuja? Inabidi niwe fiti.

Watu wamekasirika kwa sababu tumeikosa Zambia, lakini kuna mechi za Morocco, Ivory Coast ni muhimu sana kuliko hii ya Zambia.

Samatta pia alitoa angalizo kwa TFF kuwa tarehe ambazo Stars itaingia kambini wao wanatakiwa kurudi Lubumbashi kwa hiyo ni bora wawasiliane na timu yao ya TP Mazembe.

"Sisi tunahitajika Lubumbashi kati ya tarehe 7 hadi 10. Lakini kambi ya timu ya taifa itakuwa Januari 6. Kwa hiyo hapo TFF lazima wapeleke taarifa Mazembe kwa sababu tunaweza kuharibu kule au huku tukaonekana wabaya," aliongeza Samatta.

Kuhusu kukosekana kwao katika michuano ya Chalenji kule Uganda, Samatta anajitetea kwa kusema; �Mazembe walitunyima ruhusa. Hatuwezi kutoroka kambini jamani.

Walisema hawaitambui michuano hiyo kwa sababu haiko katika ratiba ya Fifa. Sisi tungefanya nini jamani?

Kuhusu kuzomewa na mashabiki, huku shabiki mmoja akiwa ana bango lililoandikwa "Who needs Samatta, We have Ngassa", Samatta anadai kwamba matukio hayo yameinua ari yake.

"Kuna kitu nimejifunza kwamba watu wanaipenda timu ya taifa. Hilo ni jambo zuri, lakini hawaambiwi ukweli. Na mimi naipenda sana na kila ninapoitwa huwa nakuja kasoro michuano ya Chalenji tu. Mimi sijawasikiliza kabisa walionizomea."

Maelezo ya Ulimwengu
Wakati Samatta akisema hayo, Ulimwengu ambaye alizungumza akiwa maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam, alisema hana sababu ya kuringa kwa ajili ya timu ya taifa lakini amevunjwa moyo sana na kuzomewa na mashabiki.

"Kaka mimi niliumia goti la kushoto kati ya Novemba 7 au 8 mwezi uliopita.

Hata wewe nadhani nilikwambia kabla hata hizi habari za kuitwa na timu ya taifa. Nitakutumia picha uone wakati natibiwa na daktari wa Mazembe ninazo katika laptop yangu, anasema Ulimwengu.

'Hata katika mechi hiyo ya kirafiki ambayo Samatta anasema Mazembe ilikwenda Brazzaville mimi niliachwa niendelee na matibabu.

Siwezi hata kufanya mazoezi na Daktari wa Mazembe aliniambia nikae nje kwa wiki tatu na nianze kufanya mazoezi mepesi mwishoni mwa wiki hii," anasema Ulimwengu.

"Nimesikitika sana kuzomewa lakini mimi ni mzalendo damu. Nimecheza katika mechi zote za timu ya vijana na wote mnajua. Sasa kwa nini niache kucheza leo? Nimesikitika sana kuzomewa na roho inaniuma sana kwa sababu watu wanapotosha ukweli.

"Kocha Kim nimeongea naye na amenielewa sana. Tatizo mashabiki na waandishi hawaelewi kwa sababu hatujawahi kuongea.

Mimi nimewahi kutoka Ulaya kwa ajili ya kuichezea timu ya vijana sasa nitashindwa vipi kuichezea timu ya taifa nikitokea hapo Congo tu," aliongeza Ulimwengu.

Ulimwengu amesema akiitwa tena katika timu ya taifa atacheza kwa nguvu zake zote na kuwanyamazisha mdomo wale wote waliomzomea Jumamosi jioni.

"Mimi mzalendo na nitawaonyesha kwa kucheza kwa juhudi. Waliotuzomea mimi na Samatta wametuharibia sana na vyombo vya habari bado havijatafuta ukweli sana zaidi ya kutuchafua," alisema Ulimwengu.

Monday, December 24, 2012

Get to know Signs of True Love Feelings & Emotional Feelings Of Love



The feelings of love we feel come from an initiation of love, where love intercommunicates loving intentions. The feelings of love follow the affections of love by way of love intentionality. In other words, love feelings follow loving actions. Love feelings are felt within our hearts, we feel the love that others touch us with, and our emotions rise in response to the love that we feel. Everybody wants to feel the emotional feelings associated with love, and the feelings that accompany loves euphoria.
The emotional feelings of love bring us to a feeling of elation, an exhilarating psychological state of great joy. Often it is our ability to appreciate the love that we receive that elevates our emotional feelings. However we sometimes allow our feelings to overtake us in the early stages of our relationships and we actually become infatuated. These feelings of euphoria may actually lead us into infatuation, which is an object of extravagant short-lived passion. These feelings of love, (misrepresented as love), are usually associated to exuberant passion, in temporary admiration. Many times it is due to this infatuated state that people become hurt because they are unable to control their emotional feelings.

The  feelings associated with infatuation are more common among adolescents and younger adults. There are plenty of young women who are so taken by their feelings, and their hormones, that they give themselves away prematurely. They then wonder, and seek to answer the question; If he had sex with me does that mean he loves me? The answer to that question is no, having sex with you does not mean that he loves you. It means that he lusts you, and you lusted him, you had sexual feelings, not love feelings. Unfortunately, our society and it's cultural teachings associate sex to love, when in reality, sex outside of the context of marriage is generally lust driven. It's generally a self absorbing physical desire to selfishly meet ones own physical mania. Sex alone does not meet loves criteria, because love is not self seeking. Love feelings follow love actions, sexual feelings often follow reactions to lust driven desires. We are all human, and we all experience the desires of our flesh, however true love feelings are associated with a deep relational bonding, not just physical intimacy.
Everyone has a desire to be loved and to naturally feel the feelings that accompany love. Remember though that the feelings come in reaction to the love that is expressed. This means that love must first be bestowed in order for the feelings of love to follow. So for you to be feeling the feelings of love means that someone had to express, show, or convey love to you in some form or fashion. It is at this juncture that many people get stuck, they get stuck on their own self interests, they like the love, so they selfishly look to acquire more for themselves. Kind of sounds a lot like what people do with money right? We all battle with inward selfishness and our culture teaches us that more is better, (more for ourselves). Love does not seek it's own desires, it looks to fulfill the needs of others.
If you are feeling the feelings of love, wouldn't you want to know that your spouse or partner is also having those same feelings? Love begins by presentation, show love to your husband, give love to your wife, and they too will enjoy the feelings of love. There are many people who ask the question; how do I get my husband to love me? or.. How do I get my girlfriend to love me? Simply, start with your own loving behavior, quit thinking about what you want to receive and start giving love to them. Ignite their love feelings, and thus the responses to love, by your own initiation. Make love a habit, you can not spread love onto others and not receive it yourself. Kiss me and kiss me again, for your love is sweeter than wine. Song Of Songs 1:2
Intention is multiplied by action, act your way into a loving behavior and you will accomplish loving feelings. Execute love, seek to satisfy the needs of your wife, girlfriend, husband, or boyfriend. Provide love an opening to bring about those feelings of love. Supply love like oxygen, and the love feelings will follow. We must show love through actions that are sincere, not through empty words. 1 John 3:18
But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, patience, kindness, goodness, faithfulness, gentleness and self-control. Against such things there is no law. Galatians 5:22-23
This is my prayer for you: that your love will grow more and more, and that you will have knowledge and understanding with your love. Philippians 1:9

SERIKALI YASEMA BEI YA UMEME HAITO PANDA KAMA TANESCO WALIVYOSEMA AWALI, SASA SHIRIKA KUFUMULIWA KWA AJILI YA MABORESHO


Waziri wa Nishati na Madini,Sospeter Muhongo 


SERIKALI imetoa msimamo wake kwamba bei ya umeme haitapanda kama Shirika la Umeme nchini (Tanesco) lilivyopendekeza, huku ikiahidi kufanya mabadiliko makubwa ndani ya shirika hilo kuanzia Januari mwakani.
Imesema lengo la mabadiliko hayo ni kuhakikisha yanaenda sambamba na kutafuta kampuni nyingine za kuzalisha umeme nchini  ili kuboresha huduma hiyo kwa wateja.
Akizungumza na wadau wa umeme katika Ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kwamba mapendekezo ya Tanesco kupandisha gharama za umeme na ambayo Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) iliyapokea, hayalengi kutatua matatizo ya shirika hilo.
Alisema  kuwa tatizo ndani ya Tanesco siyo pesa, bali ni mfumo mbovu wa uendeshaji, ambao unalifanya shirika hilo kuwa mzigo na kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja wake, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wateja.
“Msimamo wa Serikali ni kwamba, bei haitapanda kwa kuwa  matatizo ya Tanesco yanaeleweka kuwa ni mfumo mbovu,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza:
“Tunategemea kuifumua Tanesco na kuangalia uwezekano wa kupata kampuni zaidi ya mbili za kuzalisha umeme, maana mfumo wa menejimenti ni mbovu na umepitwa na wakati.”
Alifafanua kuwa kuanzia Januari mwakani watabadilisha muundo huo ili kupata kampuni ya kuzalisha na ya kusambaza umeme nchini.
Waziri huyo aliongeza kwamba baada ya mabadiliko hayo, ndipo Tanesco inaweza kutoa maoni ya kuomba kuongeza gharama za nishati hiyo.
Alisema  kutokana na mfumo mbovu ulio ndani ya shirika hilo sasa, wananchi wengi wameshindwa kutumia nishati ya umeme na kwamba hali hiyo inachangia kutokukua kwa uchumi.
“Huwezi kutegemea kupanda kwa uchumi kama uzalishaji wa umeme ni mdogo kwa kuwa hata uzalishaji viwandani utapungua na wananchi wa kawaida nao hawapati umeme kama inavyotakiwa. Tunataka kuliboresha shirika hili,” alisema Profesa Muhongo.
Atangaza vita
Waziri Muhongo pia ametangaza azma ya kuwafukuza kazi vigogo wa shirika hilo watakaoshindwa kutekeleza agizo la Serikali la kuwaunganishia umeme wateja kwa bei ya punguzo.
“Kuanzia Januari mosi mwakani bei ya kuunganisha umeme inaanza kutumika ya punguzo kutoka 455,108 hadi 177,000 sawa na asilimia 61.11, kinyume na hapo mtakuwa mmejiachisha kazi,” alisema.

OFISA WA TAKUKURU ASHAMBULIWA KWA RISASI NA KUPOTEZA MAISHA


Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hoseah 


OFISA uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bhoke Ryoba, ameuwawa kwa kupigwa rasisi na watu wasiojulikana.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la Kigamboni Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, ambako ofisa huyo alikuwa anahudhuria sharehe.
Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hoseah, akizungumzia tukio hilo  alithibitisha na kueleza kuwa alifariki dunia juzi usiku.
“Tumekuwa tukipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakihitaji kufahamu ukweli kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa mtumishi wa Takukuru, Bhoke Ryoba,” imesema sehemu ya taarifa hiyo ya Dk Hoseah iliyotolewa na ofisi ya habari ya Takukuru.
Iliendelea, “Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Dk Edward Hoseah, anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hili kwamba ni kweli mtumishi Bhoke Ryoba amefariki dunia jana usiku, Jumamosi Desemba 22, 2012 baada ya kupigwa risasi. Uchunguzi wa Polisi kuhusu chanzo cha tukio hilo bado unaendelea”.
Baadaye ofisa habari wa Takukuru Doreen Kapwani alifafanua kuwa ofisa huyo mchunguzi alifikwa na umauti wakati anajumuika na marafiki zake katika moja ya tafrija iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Kigamboni.
Alisema akiwa katika hafla hiyo, ghalfa walitokea watu wasiojulikana na kumiminia risasi hadi kufa.
“Hawa watu walimvamia Ryoba aliyekuwa kwenye sherehe moja na kumshambulia kwa risasi na kisha wakatokomea kusikojulikana,” alisema na kuongeza:
“Watu hao hawakutambulika kwa kuwa baada ya kutekeleza azma hiyo walitoweka haraka na kutokomea.”
Alipotakiwa kueleza pengine kumekuwepo matukio yoyote katika siku za hivi karibuni yanayoweza kusababisha tukio hilo, Kapwani alijibu “ni mapema mno sasa kudadisi suala hilo.”
Kapwani alisema Ofisi ya Takukuru kwa sasa haiwezi kueleza chochote kwani tukio hilo limeripotiwa polisi kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova alipotakiwa kuelezea hatua  zilizochukuliwa na jeshi hilo baada ya tukio hilo, alisema kuwa hangeweza kuzungumzia chochote kwa vile alikuwa nje ya ofisi.
“Naomba mtafute Kamanda wa Temeke, nafikiri atakuwa kwenye nafasi ya kukupa taarifa zaidi kwa sasa mimi siko ofisini, hivyo nakushauri ufanye hivyo,”alisema Kamanda Kova.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo pia hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo kwani kila simu yake ya kiganjani haikupatikana kila alipopigiwa.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) wa mkoa huo wa Temeke aliyejulikana kwa jina moja la Ame alipoulizwa kuhusu tukio hilo hakukiri wala kukataa, lakini alisisitiza kuwa anayeweza kulizungumzia ni bosi wake, Kiondo.
”Nimefika hapa ofisini hapa kwa bahati mbaya hayupo, halafu nimejaribu kumtafuta kwenye simu zake zote sikuweza kumpata, na kama unavyojua hapa protocol (itifaki) lazima izingatiwe kwahiyo siwezi kukusaidia zaidi ya hapo, pole sana ndugu yangu,”alisema Ame.

MBOWE ASEMA HATUWEZI KUWA NA KATIBA MPYA ILIHALI TUNATUMIA SHERIA ZA ZAMANI, NINI MTAZAMO WAKO MSOMAJI WETU?


FREEMAN MBOWE, MWENYEKITI CHADEMA


WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwaapisha wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Aprili 13 mwaka huu alionya kuwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya usifanywe kwa kuegemea udini, ukabila, ubinafsi, siasa ama kulenga kuvunja Muungano.
Anasema maoni ya wananchi lazima yaheshimiwe hata kama hayataweza kuingizwa yote katika katiba hiyo, huku akiwataka wajumbe hao kuweka pembeni maslahi ya makundi wanayotoka kwa kuwa kazi wanayoifanya ni kwa maslahi ya taifa..
Tume hiyo ilianza kazi yake  ya miezi 18, Mei mosi mwaka huu, ambapo mpaka sasa imeshakusanya maoni katika mikoa takribani 15.
Mbali na kukusanya maoni ya wananchi na kutengeneza rasimu ya katiba, baadaye zitafuata  hatua mbili muhimu ambazo ni kuundwa kwa Bunge Maalumu la kuchambua rasimu hiyo, kisha wananchi kupiga kura ya maoni.
Tume hiyo ya Katiba leo ndio inamaliza kukusanya maoni ya Wananchi na kuanza kujipanga kwa taratibu nyingine za kumaliza kazi yake.
Pamoja na maelezo hayo ya Rais Kikwete watu wa kada mbalimbali likiwemo Jukwaa la Katiba Tanzania walipinga kwamba Katiba mpya haiwezi kupatikana Aprili 18, 2014 kama serikali inavyoeleza.
Wakipendekeza kwamba ili Katiba iweze kutumika ni lazima sheria nyingine zirekebishwe, zoezi ambalo huchukua miaka miwili.
Walisema kinachotakiwa kufanyika ni kurekebishwa kwa Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa  katika vipengele vinavyohusiana na Tume ya Uchaguzi, ili uchaguzi wa mwaka 2015 uwe huru na wa haki, kuacha  mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya ukiendelea  kwa utaratibu mzuri.
Hoja hiyo ilinaonekana kuwagusa wengi na sasa,  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anasema jambo hilo linatakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
“Chadema tunaingiwa na hofu kwamba huenda Katiba mpya isiwe tayari kabla ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu mwaka 2015” anasema Mbowe.
Anasema hakuna ulazima wa kupatikana kwa Katiba mpya katika kipindi hicho, badala yake mchakato huo uendelee lakini yafanyike marekebisho katika Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 ambayo ndani yake kuna Tume ya Uchaguzi (Nec) na daftari la kudumu la wapigakura.
“Kuna mambo yanatakiwa kufanyiwa kazi, kwanza ni kuwa na Tume huru ya Uchaguzi na mchakato wa kupata tume hii ufanyike bila kuathiri mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.
“Tukienda katika chaguzi hizi mbili bila kubadili sheria nyingine zinazogusa maisha yetu ya kila siku ikiwemo hii ya uchaguzi ni wazi kuwa tutaingia katika machafuko, uchaguzi hauwezi kuwa huru na wa haki kama ukisimamiwa na muundo wa Nec hii inayoteuliwa na Rais” anasema Mbowe.
Anasema vyama vya upinzani haviwezi kujiandaa na Uchaguzi Mkuu ujao kwa sababu mpaka sasa havijui mfumo wa uchaguzi huo utakuwa wa namna gani.
“CCM wao wanajua kila kitu na ndio maana hawana wasiwasi, pia daftari la kupigia kura nalo ni tatizo kwa kuwa halijafanyiwa maboresho,” anasema Mbowe.
Anasema  licha ya mchakato wa Katiba kuendelea huku serikali ikieleza wazi kwamba Katiba itapatikana kabla ya mwaka 2015, wao hawaiamini kwa kuwa siasa ni mchezo mchafu.
“Hatuna sababu ya kukiamini chama tawala katika hili kwa sababu wanachokizungumza ni tofauti na wanachokifanya. Chama chochote makini lazima kianze kujipanga mapema lakini kwa utaratibu wa sasa hatuwezi kufanya hivyo,” anasema Mbowe na anaongeza;
“Tutafanya maandalizi kwa sheria ipi, hatujui Muungano utakuwa wa aina gani, lakini pia hatujui tutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya aina gani na wala hatujui majimbo yatakuwa mangapi.”
Anasema kuwa kwa mara ya kwanza ilipotungwa sheria ya mabadiliko ya Katiba, chama hicho kiliipinga na kutaka ifanyiwe marekebisho katika sehemu tatu ambazo ni, muundo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge la Katiba na Kura ya Maoni.
“Pamoja na sheria hiyo kufanyiwa marekebisho lakini yaligusa sehemu moja tu kati ya hizo tatu,” anasema Mbowe.
Anasema hata kama Tume hiyo itamaliza kazi yake ya miezi 18, bado kuna ulazima wa mchakato wa kubadili sheria mbalimbali kuanza kufanywa.
“Chadema hatupingi mchakato wa Katiba Mpya, tume iendelee na zoezi lake lakini wakati huohuo ufanyike mchakato wa mabadiliko ya sheria mbalimbali ambazo zinaweza kutuletea matatizo katika uchaguzi,” anasema Mbowe.
Anasema wanaipinga sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 kwa kuwa ilitungwa wakati nchi ikiwa katika mfumo wa chama kimoja na hata Tume ya Uchaguzi  nayo iliundwa kwa mfumo huo huo.
“Ili nchi iwe na uchaguzi huru ni lazima vyama vyote vya siasa viwe na imani  na Tume ya Uchaguzi,  hata katika mechi ya mpira wa miguu lazima timu ziwe na imani na refa, tusikubali kuendelea kuwa na sheria mbovu kwa kigezo cha mchakato wa Katiba,” anasema Mbowe

Saturday, December 22, 2012

MWAKYEMBE AWANG'OA VIGOGO 16 BANDARI YA DARESALAM KWA TUHUMA ZA WIZI

Raymond Kaminyoge na Bakari Kiango
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewasimamisha kazi vigogo 16 wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa tuhuma za ufisadi.

Idadi hiyo inafanya waliosimamishwa kazi katika bandari hiyo hadi sasa kufikia 23.
Akizungumza na wafanyakazi wa TPA Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe alisema vigogo hao wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali.

“ Bodi imewasimamisha kazi kutokana na tuhuma mbalimbali za wizi na migongano ya kimaslahi, hawa wamesimamishwa baada ya bodi kuichambua ripoti ya uchunguzi iliyotolewa na tume niliyoiunda,” alisema.

Waliosimamishwa kazi na nyadhifa zao kwenye mabano ni Bakari Kilo (Mkurugenzi Uhandisi), Raymond Swai (Meneja Uhandisi), Frolence Nkya (Mkurugenzi wa Mipango) na Mahebe Machibya (Meneja Ununuzi na Ugavi).

Wengine ni Teophil Kimaro (Meneja Ununuzi), Mary Mhayaya (Afisa Uhandisi Mkuu), Ayoub Kamti (Mkurugenzi wa Tehama), Mathew Antony (Meneja Kitengo cha Kontena) Maimuna Mrisho (Mkurugenzi wa Mifumo wa Menejimenti).

Wengine ni Fortunatus Sandalia (Askari kitengo cha Ulinzi), Fadhili Ngolongo (Kitengo cha Marine), Mathew Antony (Meneja Kontena), Mohamed  Abdullah (Kitengo cha Mafuta), Kilimba (Idara ya ulinzi) na Owen Rwebu.

Mwakyembe alisema katika ripoti ya uchunguzi imegundulika kwamba baadhi ya vigogo wa Bandari wanamiliki kampuni ambazo zinafanya kazi za TPA.

“Tumebaini kuwa kuna mgongano mkubwa wa kimaslahi ndani ya bandari, kuna wafanyakazi wengine wana kampuni za mkononi ambazo hazijasajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) lakini zimepewa kazi za TPA,” alisema.

Alisema kampuni hizo zinapomaliza muda wa mikataba yao huongezewa muda wa mikataba mingine.
Dk Mwakyembe alisema kuna mtandao mkubwa unaofanywa kwa watu mbalimbali kwa kushirikiana na vigogo wa bandari ili kufanikisha wizi katika bandari.

“Kontena zinayeyuka, zinaibwa kama Twiga walivyopandishwa kwenye ndege, ninaapa mtandao huu nitaumaliza hapa bandarini,” alisema Mwakyembe huku akishangiliwa na wafanyakazi.
Aidha Mwakyembe amepiga marufuku utaratibu wa kuingia bandarini na kulipia kiingilio cha Sh200 unaojulikana kama potipasi.

“ Utaratibu huo ndiyo umekuwa ukisababisha wizi bandari, ni marufuku watu wasiohusika kuingia bandarini, Sh200 wanazotoa zitatusaidia nini,” alihoji Mwakyembe.

Hata hivyo alipongeza juhudi ambazo zimeanza kuonekana katika mamlaka hiyo ya kuongeza mapato kila mwezi tangu alipoisimamisha bodi hiyo.

Alisema mamlaka hiyo kabla ya mageuzi ilikuwa inakusanya mapato ya Sh28 bilioni lakini sasa inakusanya Sh50 bilioni kwa mwezi.

Aidha, Mwakyembe alisema watumishi wa bandari waliajiriwa kwa njia za ujanja ujanja watachunguzwa na hatimaye kufukuzwa kazi.

“Bandari tumebaini kwamba kuna wafanyakazi wengi ambao wameajiriwa kwa undugu, ujomba ujomba, tutawashughulikia katika siku chache zijazo,” alisema.

DK SLAA AMWAMBIA LEMA AMBANE PINDA BUNGENI WATAKAPO RUDI


KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa 

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemuagiza Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Godbless Lema wakati atakapokwenda Bungeni, kufufua hoja kuhusu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kulidanga Bunge Febuari 10 mwaka huu.

Dk Slaa alitoa agizo hilo jana makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wafuasi walioandamana wakishangilia Lema kurejeshewa ubunge wake jana na Mahakama ya Rufaa.

Dk Slaa alisema huu ni wakati wa Lema kwenda kufufua hoja ya kwamba Waziri Mkuu alilidanganya Bunge kwani tayari udhibitisho wa jambo hilo ulikuwepo.

“Nakuagiza sasa Lema utakapo kwenda Bungeni uende ukambane Waziri Mkuu kwa kulidanganya Bunge kwani Spika wa bunge alisema hoja hiyo imefungwa kwa sababu ya wewe kutokuwepo bungeni,” alisema Slaa.

Waziri Mkuu Pinda akijibu swali bungeni aliseme chanzo cha vurugu zilizosababisha vifo mjini Arusha ni ni uamuzi wa madiwani wa Chadema  kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa jiji hilo.

Pinda alitoa kauli hiyo Febuari 10 mwaka huu wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe  aliyetaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu mauaji ya raia yaliyofanywa na Polisi wakati wa vurugu zilizotokea Arusha.

Kutokana na majibu hayo, Lema kabla ya ubunge wake kutenguliwa na mahakama, aliomba kupewa mwongozo wa spika akidai kwamba Pinda alikuwa amelidanganya Bunge.

Spika wa Bunge Anne Makinda hajawahi kutoa mwongozo kuhusu suala hilo na aliwahi kusema kuwa suala hilo limefungwa kwani aliyeuliza hayupo tena bungeni.

SHEHENA YA KONDOM FAKE KUTOKA INDIA YAKAMATWA BANDARI YA DARESALAAM, JE TUTAPONA KWELI?

  Mipira ya Kondom
KONTENA lililosheheni kondomu za kiume kutoka nchini India imekamatwa na kuzuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1   milioni zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa taratibu zaidi za kisheria.
“Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika.
Tulipokwenda bandarini tukabaini kwamba bado zipo katika hali ile ile, kumbe  zimeingizwa nchini kwa njia ya panya, kwa kweli ni mbovu na ndiyo maana tumelazimika kuwajulisha wanahabari ili muwape taarifa wananchi wawe makini,” alisema Kinabo.
Alifafanua zaidi kwamba kondomu hizo ni mbovu kwani zimebainika kuwa na vitundu, pia zinapasuka haraka, hazina kabisa viwango vya ubora wa bidhaa unaotakiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO).
Kinabo alisema kuwa TBS bado wanaendelea kufanya mawasiliano na kampuni iliyotengeneza kondomu hizo, lakini kwenye kasha  lake inaonyesha kuwa inaingizwa nchini na kampuni ya Fair Deal Exim ya Dar es Salaam.  

MAHAKAMA YAMRUDISHA LEMA BUNGENI, NI SHAMRASHAMRA ZA KUTOSHA ARUSHA MJINI, PATA UNDANI ZAIDI BOFYA HAPA!


Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema John Mnyika akifurahi na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema baada ya kushinda katika rufaa yake jana jijini Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Rufani imemrejesha bungeni Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ikiwa ni miezi tisa tangu alipovuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
Mahakama hiyo ilimrejesha Lema bungeni, baada ya kushinda rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Arusha iliyotolewa Aprili 5, mwaka huu.
Hukumu hiyo iliyosomwa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu imemtambua Lema kuwa mbunge halali wa Arusha Mjini na kuwaamuru wajibu rufaa kumlipa gharama za rufaa hiyo.
Katika hukumu hiyo iliyoandikwa na Jaji Bernard Luanda kwa niaba ya wenzake wawili waliokuwa wakisikiliza rufaa hiyo, Mahakama ya Rufani ilisema kuwa wajibu rufani hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi dhidi ya Lema kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi.
“Rufaa imefanikiwa na tunatengua hukumu, tuzo na amri  ya Mahakama Kuu. Tunamtangaza mrufani kuwa Mbunge wa Arusha Mjini,” ilisema Mahakama ya Rufani katika hukumu yake hiyo.
Uamuzi huo uliwafanya wanachama na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika ndani ya ukumbi wa Mahakama hiyo, kulipuka kwa furaha huku wakiimba kibwagizo cha “People’s Power!” na wengine wakiongeza kwa kuimba “Lema! Lema! Lema!”
Wanachama na wafuasi hao wa Chadema walianza kusukumana kwenda kumkumbatia Lema, huku wengine wakipanda kwenye viti (mabenchi) ya mahakamani.
Tukio hilo lilisababisha taharuki kutokana na kusukumana, huku wengine wakianguka kwenye mabenchi, hali ambayo pia iliwapa wakati mgumu viongozi wa Chadema akiwamo, Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kutoka nje ya ukumbi huo.

Hoja mpya
Katika rufaa yake, Lema kupitia kwa mawakili wake, aliwasilisha hoja 18 za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, lakini katika uamuzi wake, Mahakama ya Rufani iliibua na kutolea uamuzi hoja mpya ambayo haikuwa imetolewa na upande wowote mahakamani hapo.
Hoja hiyo ambayo iliibuka kwa mara ya kwanza kabisa siku ya kusikiliza rufaa hiyo ni kama warufani walikuwa ni wapiga kura waliojiandikisha.  
Katika uamuzi wake kuhusu hoja hiyo, Mahakama ilisema kuwa wajibu rufaa hao, hawakuwa wapiga kura kwa kuwa katika kumbukumbu za Mahakama hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa ni wapiga kura waliosajiliwa.
Mahakama ilipoibua hoja hiyo, Wakili wa warufani, Mughway alijibu kuwa wajibu rufaa hao ni wapiga kura halali waliosajiliwa na kwamba hata Mahakama ilijiridhisha kwa kuangalia kadi zao za kupigia kura.
Wakili Mughaway alidai kuwa suala hilo lilijitokeza Mahakama Kuu na wajibu rufaa hao wakawasilisha kadi zao mahakamani ambazo ilinakili majina na namba zao na kisha kuzirejesha kwa wenyewe.
Lakini Wakili wa Lema alidai kuwa hata kama kadi hizo ziliwasilishwa mahakamani, utaratibu ambao ulitumika haukuwa wa kisheria, akidai kwamba zilipaswa ziwasilishwe kama vielelezo vya ushahidi na si jaji kuziangalia na kisha kuzirejesha kwa wahusika.
Katika hukumu yake jana, Mahakama ya Rufani ilikubaliana na hoja za mawakili wa warufani, ikisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi mahali ambako kadi hizo zimepokewa mahakamani kama vielelezo vya ushahidi.
Mahakama ilisema kwamba kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajibu rufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.
“Katika kesi hii, Wakili Alute (Mghway) aliwasilisha kadi za wajibu rufaa kwa Jaji (Aloyce Mujuluzi) kuthibitisha kuwa wajibu rufaa walikuwa wapiga kura halali,” ilisema Mahakama katika hukumu yake hiyo.
Mahakama hiyo ilisema utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na mmiliki wa nyaraka hizo.
Pia Mahakama hiyo ilisema kumbukumbu hizo hazionyeshi kama mrufani alipewa fursa ya kuzungumza lolote kuhusiana na utaratibu huo wa kuwasilisha hati hizo.
Hata hivyo, Mahakama hiyo ilisema kuwa hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake.
Ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni maslahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba, kanuni ya haki ya kisheria kufungua kesi ni kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au maslahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
“Hivyo mpiga kura hana haki ya kisheria kufungua kesi kuhoji matokeo ya uchaguzi pale ambako haki zake hazikukiukwa,” ilisema Mahakama ya Rufani.
Ilisema kwa mujibu wa Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Tanzania, raia anakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi kwa maslahi ya jamii, kama ilivyotokea katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya mwaka 1995.
Mahakama ilisema kuwa shauri hilo halikufunguliwa chini ya Ibara ya 26 (2) ambayo inampa fursa na haki raia yeyote kufungua shauri mahakamani lenye maslahi ya umma, huku ikisisitiza kuwa madai ya wajibu rufani katika kesi hiyo hayagusi maslahi ya jamii yote.
Katika hoja hiyo, Wakili wa wajibu rufani, Mughway alitumia kesi ya William Bakari na mwenzake dhidi ya  Chediel Mgonja na AG, namba 84 ya mwaka 1980.
Katika kesi hiyo Mahakama Kuu iliamua kuwa inapothibitika kuwa mpiga kura amejiandikisha ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo.
Mahakama ya Rufaa ilisema kwa uamuzi huo wa Mahakama Kuu katika kesi hiyo ina maana kuwa mpiga kura ana haki zisizo na mpaka kufungua kesi hata kama haki zake hazijakiukwa kwa namna yoyote.
Hata hivyo, Mahakama ya Rufani ilisema kuwa Mahakama Kuu katika kesi hiyo iliamua kwa makosa na kwamba haidhani kuwa sheria haikukusudia kusema kuwa mtu yeyote bila kujali mahali alipojiandikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo katika jimbo lolote nchini.
Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake ilisisitiza kuwa katika kesi kama hiyo ilikuwa ni wajibu wa yule tu ambaye anaona haki zake zilikiukwa.
Kutokana na kuamua hoja ya kwamba mpiga kura hana haki ya kufungua kesi, mahakama haikushughulika na hoja nyingine zilizowasilishwa na warufani, wala rufaa iliyofunguliwa na wajibu rufaa.

Friday, December 21, 2012

YAFAHAMU MATOKEO YA UTAFITI WA WANAWAKE WANAOFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE TANZANIA.



.
Mwandishi wa BBC John Solombi ameripoti kwamba utafiti mpya unaonyesha asilimia 27 ya wanawawake Tanzania wanafanya ngono kinyume na maumbile.
Mtafiti Mwanasayansi Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa NIMR amesema katika utafiti walioufanya umebaini asilimia 26.5 ya wanawake hukubali kuingiliwa kinyume.
Baadhi ya wanawake kutoka Kinondoni Dar es salaam, Tanga, Makete na Siha wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile ambapo Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
Amekaririwa akisema “ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo”
facebook.com/UdakuSpecialBlog

.
Wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambapo Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.
Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ni hafifu kwani wakitumia mipira (Condom) inapunguza raha.
Wanawake pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana akiuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo likichukua nafasi.
Watafiti hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana, wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto.
John Solombi anapatikana pia kupitia kishindoleo.blogspot.com

Diamond - Kesho FULL HD

MATOKEO YA DARASA LA SABA YAMETOKA, HII NI TATHIMIN YA UFAULU NA CHANGAMOTO ZAKE

 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambw

SERIKALI imetangaza matokeo ya darasa la saba mwaka huu, huku takwimu za matokeo hayo zikionyesha kuwa zaidi ya nusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 ni wale waliopata asilimia 40 ya alama kwenda chini katika matokeo hayo.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa wananfunzi 294,833 sawa na asilimia asilimia 52.58  waliopata daraja ‘D’ wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Hao wanaungana na wenzao 265,873 waliopata madaraja ya A,B na C ambao ni sawa na asilimia 47.41. Kwa mujibu wa taratibu za mitihani ya darasa la saba, jumla ya alama zote ni 250 ambazo zimegawanywa katika madaraja matano ambayo ni A mpaka E.

Mchanganuo wa madaraja hayo ni alama 201 hadi 250 kwa daraja la A, alama 151 – 200 kwa daraja B, alama 101 hadi 150 kwa daraja C, alama 51 – 100 kwa daraja D na alama 0 – 50 kwa daraja E.

Waziri Kawambwa alisema wanafunzi 560,706 walichaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari kati ya 865,534 waliofanya mtihani huo wa siku mbili; Septemba 19 na 20 mwaka huu na kwamba mwaka huu wasichana wamefanya vizuri katika mtihani huo kuliko wavulana.

“Wasichana waliofaulu ni 281,460 sawa na asilimia 50.20 ya  wanafunzi 560,706 wakati wavulana waliofaulu ni 279,246 sawa na asilimia 49.80,” alisema Kawambwa alipokuwa akitangaza matokeo hayo na kuongeza:

“Matokeo yanaonyesha kuwa jumla ya wahitimu 3,087 walipata daraja A, wakati 40,683 walipata daraja la B. Wanafunzi 222,103 walipata alama za daraja C wakati  526,397 walipata daraja D. Watahiniwa waliobaki 73,264 walipata E”.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013, imeongezeka kwa asilimia 8.8 ikilinganishwa na wanafunzi 515,187 waliochaguliwa mwaka jana.


“Mtihani wa mwaka huu, kwa mara ya kwanza watahiniwa walifanya kwa kutumia teknolojia mpya ya Optical Mark Reader (OMR) na ulisahihishwa kwa kutumia kompyuta,” alisema.

Alisema matokeo haya yanaonyesha alama ya juu kabisa ilikuwa 234 kati ya 250 kwa wasichana na wavulana.

Kabla ya matokeo, wasichana waliofanya mtihani walikuwa 456,082 sawa na asilimia 52.68 na wavulana ni 409,745 sawa na asilimia 47.32,” alisema Dk Kawambwa.

“Watahiniwa 29,012 sawa na asiliamia 3.24 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, vifo na ugonjwa,” alisema.

Dk Kawambwa alisema, kati yao, ambao hawakufanya mtihani wasichana walikuwa 12,501 sawa na asilimia 2.67 na wavulana ni 16,511 sawa na asilimia 3.87.

Waziri huyo  alisema,  udanganyifu katika mitihani kwa mwaka huu umepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana.

“Waliofutiwa matokeo mwaka huu ni watahiniwa 293 ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliofutiwa matokeo yao kwa udanganyifu mwaka jana,” alisema Dk Kawambwa.

Hata hivyo, itakumbukwa serikali ilionya mwaka jana kuwa mwanafunzi atakayebainika kujiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi hizo, Mwalimu Mkuu wa shule alikotokea mwanafunzi huyo na Msimamizi wa Mtihani wakumaliza elimu ya msingi watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Katika mkutano huo wa jana na Waandishi wa Habari, Dk Kawambwa hakutaja  viwango vya ufaulu kwa kila somo kama ambavyo imezoeleka katika mitihani iliyotangulia wala mkoa uliofanya vizuri au vibaya.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alipotangaza matokeo ya mwaka jana aliweka wazi viwango vya ufaulu wa masomo ya Kiingereza, Sayansi na Hisabati, ikilinganishwa na mwaka juzi.

Mulugo alisema viwango hivyo vilikuwa vimepanda kwa mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2010 ambavyo ni Kiingereza kutoka asilimia 36.47 hadi asilimia 46.70, Sayansi asilimia 61.33 kutoka asilimia 56.05 na Hesabu asilimia 39.36 kutoka asilimia 24.70.

Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo akizungumzia matokeo hayo jana alisema: “Hili janga, kwa sababu ukifanya uchambuzi wa haraka utabaini kuwa wanafunzi waliopata alama za daraja la A ni asilimia 0.35 tu”.

Lyimo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), alisema upo uwezekano mkubwa kukawa na idadi kubwa ya wanafunzi wasiojiweza waliochaguliwa kwenda Sekondari, hivyo akashauri iandaliwe program maalum ya kuwawezesha wanafunzi hao kumudu masomo ya kidato cha kwanza.

“Kama wanafunzi zaidi ya nusu waliochaguliwa kwenda sekondari ni wale wa daraja la D, hapo kuna kazi kubwa sana, tunaweza kuwa na mbumbubu wengi Sekondari kwahiyo nashauri Serikali iandae walau mpango wa wiki mbili kabla ya shule kufunguliwa ili kuwasaidia hawa watoto,”alisema.

Lyimo alisema ofisi yake itaendelea kufanya utafiti ili kubaini sababu za kufanya vibaya kwa wanafunzi katika mtihani huo na kwamba itatoa taarifa baada ya kupata matokeo ya kitaalamu kuhusu suala hilo.

DK SLAA ASEMA TUNASUBILI TAARIFA YA ARFI


KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa amesema chama hicho kinasubiri kupokea taarifa ya mgogoro unaofukuta ndani ya chama hicho mkoani Katavi na kusababisha Makamu Mwenyekiti wake Taifa , Said Arfi, kutupa kadi yake ya uanachama.

Ameeleza kuwa Katiba ya chama hicho inaeleza wazi kwamba unapoibuka mgogoro, unatakiwa kuripotiwa katika ofisi ya Katibu Mkuu Taifa ndani ya siku 14.

Tukio la Arfi kutupa kadi ya Chadema lilikuwa la pili ndani ya wiki moja, kwani juma lililopita uliibuka mgogoro mwingine wilayani Karatu ambako pamoja na mambo mengine uliishia kwa Kamati Kuu kuusimamisha uongozi wote wa chama hicho wilaya.

Arfi ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini, alitishia kujitoa Chadema juzi, katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya chama hicho Mikoa ya Katavi na Rukwa kilichoketi Namanyere, Nkasi na kufikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Rukwa, Laurent Mangweshi.

Katika kikao hicho, Arfi anadaiwa kuichukua kadi yake ya Chadema na kumtupia Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, John Mallack akitangaza kuachia nyadhifa zote alizonazo, kisha kuondoka ukumbini, kabla ya kufuatwa na wazee wa chama hicho na kumsihi aichukue kadi yake hiyo.

Hata hivyo, Mangweshi jana aliliambia Mwananchi kwamba hajapewa barua hiyo mpaka sasa na kwamba yeye bado ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Rukwa, kauli ambayo ilipingwa na Katibu wa chama hicho mkoani Rukwa na Katavi, Ozem Chapita aliyesema kuwa ipo tayari na wameisafirisha kwa basi jana mchana ili imfikie.

Akizungumzia tukio hilo jana Dk Slaa alisema  taarifa hizo amezisikia ila hawezi kutoa maamuzi kwa kuwa Chadema kinafuata taratibu za vikao pamoja na Katiba yake.

“Utaratibu wa chama ni kwamba malalamiko yeyote ni lazima yawasilishwe katika ofisi ya Katibu Mkuu ndani ya siku 14” alisema Dk Slaa na kuongeza;

“Mimi kama Katibu Mkuu ni lazima nifuate taratibu za chama na sio kufanya vinginevyo.”

Alisema kuwa taarifa hizo amezisikia kupitia vyombo vya habari na kwamba anachokisubiri ni taarifa rasmi ya maandishi ili kama chama kiweze kukaa vikao na kujadili mgogoro huo.

Alipoulizwa kuna taarifa kwamba baadhi ya makada wa chama hicho wanatumiwa kukivuruga, Dk Slaa alisema kuwa inawezekana hilo likawa na ukweli lakini kama kawaida ya chama hicho, hakitoi maamuzi bila ya kukaa vikao.

“Hizo ni taarifa ambazo zipo na zinaandikwa kila siku katika vyombo vya habari, zikija rasmi katika ofisi ya chama zitajadiliwa” alisema Dk Slaa.

Arfi alifikia hatua hiyo baada ya kutokea sintofahamu kati ya wajumbe wa kikao hicho katika uamuzi huo uliofikiwa kwa kupiga kura za ndiyo na hapana.


Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilifafanua kuwa Arfi alikerwa na kauli iliyotolewa na Mangweshi kuwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alipokea rushwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Vyanzo hivyo vya habari vimeeleza kuwa kutokana na hali hiyo, Arfi alipandwa na hasira na kuamua kumrushia kadi Mallack kisha kutoka nje ya ukumbi.

“Hatua hiyo ilifanya wajumbe wa kikao hicho nao kutoka nje ya ukumbi na kuanza kumbembeleza ili asichukue uamuzi huo na kisha wakamwekea kadi yake ya uanachama katika mfuko wake wa shati,” alisema mmoja wa makada hao.

Arfi mwenyewe hakupatikana juzi kuzungumzia tukio hilo na hata jana alipotafutwa simu zake zote zilikuwa zimezimwa.

Mangweshi aeleza ya moyoni

Akizungumzia kitendo cha kuvuliwa madaraka
Mangweshi alisema mara baada ya kukabidhiwa barua yake atakata rufaa kwa maelezo kuwa haki haikutendeka katika kikao hicho.

Alisema mpaka sasa taarifa za kuwa amevuliwa uongozi anazisikia katika vyombo vya habari, huku akisisitiza kuwa yeye bado ni Mwenyekiti wa Bavicha wa mikoa  ya Rukwa na Katavi.

Alipohojiwa juu ya kuonywa mara kadhaa katika vikao kutokana na utovu wake wa nidhamu alisema, “Katika maisha yangu sijawahi kuonywa na hata Chadema sikuwahi kuonywa tangu nilipojiunga mwaka 2001, hakuna kikao cha baraza la uongozi kilichokaa kunijadili.”

Alifafanua kwamba hata Baraza la Usuluhishi halina mamlaka ya kumvua mtu madaraka na kuongeza kuwa  kikao kilichofanyika  Namanyere kilikuwa ni cha Baraza la Usuruhishi na si cha Baraza la Uongozi ambalo alidai kuwa ndio lenye mamlaka.

Alisema ameshangazwa na kitendo cha viongozi  wa Chadema mkoani Katavi kukimbilia katika vyombo vya habari kutoa tamko la kumfukuza kabla ya kukamilisha taratibu za kichama.

“Mimi ndio nilitakiwa kukimbilia katika vyombo vya habari kudai haki yangu kama wangenikabidhi barua yangu, kinyume chake wao ndio wamekimbilia huko tena bila kufuata taratibu” alisema na kuongeza;

“Kama hawatanitendea haki sitahama Chadema, nitafia hapa hapa kwa sababu chama hiki lengo lake ni kulikomboa taifa kutoka mikononi mwa CCM.”

Katibu wa chama hicho mkoani Rukwa na Katavi, Ozem Chapita alikiri kuchelewa kwa barua ya kumvua madaraka  Mangweshi  na kusema kuwa tatizo ni kwamba  mwenyekiti huyo anaishi mkoani Katavi  huyu yeye ambaye ni mtendaji mkuu wa chama hicho akiwa anaishi mkoani Rukwa.

Alisema barua hiyo ipo tayari na wameisafirisha kwa basi ili iweze kumfika Mangweshi.



Tanga kwazidi kufukuta

Katibu wa Bavicha mkoani Tanga, Deogratius Kisandu ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kubatilisha Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2010  kwa kuwa ulikuwa na wagombea wawili kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kitendo hicho kinatakiw akufanywa haraka baada ya Dk Slaa ambaye aligombea urais mwaka 2010 kwa tiketi ya Chadema kukiri  kwama mpaka sasa bado anayo kadi ya CCM.

“Katika hili ni  ni wazi kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ulikuwa batili na kulikuwa na wagombea wawili kutoka chama kimoja” alisema Kisandu.

Kisandu aliyasema hayo jana wakati akijibu tuhuma alizotupiwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tanga, Said Mbweto  kwamba amekurupa kutoka tamko la kumtaka Dk Slaa ajiuzulu.

“Mara baada ya Dk Slaa kukiri kuwa na kadi ya CCM , Nec inastahili kubatilisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuitisha upya uchaguzi wa Rais ili wajitokeze wagombea wapya wa nafasi hiyo” alisema Kisandu.

Alisema kwa maana hiyo ni kwamba hata Rais Kikwete kwa sasa hastahili kuwa katika nafasi hiyo kwa sababu kauli ya DK Slaa imebatilisha nafasi yake.

Alisema hakukurupuka kutoa kauli hiyo na kwamba yalikuwa mawazo yake binafsi na kusisitiza kuwa msmimamo wake uko palepale.

Karatu wapitisha bajeti

wilayani Karatu Kamati ya Ushauri ya wilaya ya hiyo (DCC), juzi imepitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya  mwaka 2013/14 ya Halmashauri ya wilaya hiyo, ambapo kiasi cha Sh 20.6 bilioni kinatarajiwa kukusanywa.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Clementi Berege akiwasilisha taarifa ya mapendekezo hayo,katika kikao hicho, kilichoongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Felix Ntebenda, alisema bajeti hiyo ya 20.6 bilioni ni ongezeko la  sh 51.7 milioni ya bajeti iliyopita ya mwaka 2012/13.

Alisema mapato ya ndani ya halmashauri hiyo yanatarajiwa kufikia 1.9 bilioni,Ruzuku ya matumizi ya kawaida 17.3 bilioni na ruzuku ya miradi ya maendeleo 2.1 bilioni.

Hata hivyo, alisema bajeti hiyo, inaweza kubadilika kutokana na maoni na vyombo vingine vya maamuzi, ikiwepo baraza la madiwani na vyombo vingine kabla ya kufikishwa kwenye bajeti kuu.

Akichangia taarifa hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Ntibenda aliwataka wadau wa maendeleo katika wilaya hiyo, kuendelea kushirikiana na serikali katika kuifanikisha bajeti hiyo.

Hata hivyo, Ntibenda aliwataka watendaji na halmashauri na wanasiasa kushirikiana kwa pamoja kuisaidia wilaya hiyo, kwani wakati wa siasa umekwisha na kazi iliyombele yao wote ni kusaidia maendeleo ya wakazi wa wilaya hiyo.

"sitaki kusikia kuna miradi imekwama kwa ajili ya mambo ya siasa, chaguzi zimekwisha sasa tuchape kazi"alisema Ntibenda.

Awali wajumbe hao pia walipitisha mapendekezo ya kupeleka kwenye kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa wa Arusha(RCC), kuomba barabara ya kutoka Ayasi-Endabash hadi Manyara kibaoni.

Mkuu wa wilaya hiyo, alisema barabara hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya wilaya hiyo lakini halmashauri imeshindwa kuitengeneza kutokana na gharama kubwa kuhitajika ikiwepo ujenzi wa daraja.

Akizungumza katika kikao hicho, mbunge wa jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse, aliwataka watendaji wa halmashauri ya Karatu kuacha kuwa vikwazo vya maendeleo.

Natse alisema hivi sasa wilaya hiyo, inakabiliwa na migogoro kadhaa  na kukwama kwa miradi ya maendeleo kutokana na baadhi ya watendaji wa halmashauri, wakiwepo watendaji wa vijiji kuwavuruga wananchi.

Kikao hicho, lichofanyika ukumbi ya maendeleo Karatu,pia kilishirikisha wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, vyama vya siasa, wakuu wa idara wa halmashauri ya karatu na viongozi katika ngazi mbali mbali za wilaya hiyo.

Imeandaliwa Fidelis Butahe, Dar na Juddy Ngonyani, Katavi, Burhani Yakub, Tanga na Mussa Juma, Arusha


Thursday, December 20, 2012

MAKUNDI YA UEFA 16 BORA HAYA HAPA

Galatasaray vs FC Schalke

Celtic vs Juventus

Arsenal vs Bayern Munchen

Shaktar Donetsk vs Borussia Dortmund

AC Milan vs FC Barcelona

Real Madrid vs Manchester United

Valencia vs Paris Saint Germain

Porto vs Malaga

PATA KUJUA JUU YA TUHUMA KWA ZITTO NA KUNDI LAKE KUTOKA KWA MAMUYA...


Bahati mbaya nimekuja wakati mjadala ukiwa tayari umefungwa na sikuweza kupata fursa ya kujibu baadhi ya hoja ambazo kimsingi zilikuwa zinatakiwa kupewa majibu. Mwanzoni sikutaka kushiriki kabisa mjadala huu lakini baada ya Mhe. Zitto kushiriki imenilazimu walau niseme machache.

Katika thread hiyo - Huyo ndiye Ben Saanane na majibu ya Zitto Mhe. Zitto aliandika hivi:


Quote By Zitto View Post
Ninasikitika sana kuona wanachama wa CHADEMA wanavyoweza kutumika kwa maslahi ya kundi fulani kuharibu heshima ya viongozi wao mbele ya jamii.

Ninaomba ndugu Ben Saanane aje hapa jukwaani kuthibitisha maelezo haya ya Bwana Mamuya kutoka Arusha. Mimi binafsi nikikutana na Ben Saanane leo naweza kupishana naye maana sijawi kumwona, wala kukutana naye. Ndugu Ben Saanane nimewasiliana naye kwenye simu mara mbili au tatu kuhusu masuala yake ya kitaaluma au pale alipohisi kuonewa ndani ya chama. Sijawahi kukutana naye hata siku moja. Kama nasema uwongo yeye binafsi aje hapa kukanusha.

Mimi pamoja na wenzangu tumejenga chama hiki mpaka hapa tulipofika. Tumeingiza watu kwenye chama hiki ili kwa pamoja tuweze kujenga asasi imara kabisa ya kidemokrasia. Chama hiki kina damu yangu. Chama hiki kina muda wangu. Chama hiki kina jasho langu. Nitakuwa mtu wa mwisho kusaliti chama hiki. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sitarajii kuwa mwanachama wa chama zaidi ya CHADEMA.

Ninawasihi wana CHADEMA tuache propaganda za kuchafuana. Nguvu kubwa inayotumika kumchafua Zitto ielekezwe kwenye kujenga taasisi imara ya CHADEMA, chama chenye demokrasia, kisicho na upendeleo, chenye uwakilishi wa kitaifa na chenye kuthamini nafasi ya kila mwanachama.

Mamuya, mara kadhaa umetaka kuniona kwa sbaabu nisizozijua na imekuwa ikishindikana. Unapata dhambi kubwa sana kumwaga sumu unayomwaga kwa mtu usiyemjua wala hujawahi kukutana naye.Acha kutumika. Jisimamie. Simamia chama.

Vijana, wote wa vyama vyote, siku zote simamieni misingi (principles) na sio kusimamia watu. Watu sio mawe. Mtaja juta. Misingi inadumu. Watu hawadumu. Acheni kuramba miguu ya watu. Simamieni misingi ya chama. Misingi ya nchi yetu. Misingi ya demokrasia. Kataeni kutumika.

Angalieni, wanaozungumzia sana usaliti waweza kuta ndio wasaliti wakubwa. wanazungumzia usaliti kama 'defensive mechanism'.

Tuacheni ujinga huu. Tufanye kazi. Kazi tu ndio kipimo cha ukamanda na sio kurambaramba visigino vya watu.

Mwisho, nasikia sikia sana habari za kuchinjana. Kuuana nk. Nasikia habari hizi kwa watu wale wale wa kikundi kile kile. Moja, natoka Kigoma. Nimeaga kwetu. Nitakufa kwa amri ya Mungu. Siogopi kufa. Iwapo kifo changu kitatokana na mkono wa mtu, sidhani kama kwa mtu huyo kama hata panya atabaki nyumbani kwao. Underline this.

Pili, revolutioneries don't talk about deaths. Only cowards do.
Ndugu Zitto na Wanabodi,

Kama nilivyosema awali, sikutaka kuchangia mjadala huo tangu jana kwakuwa niliamini mambo nyeti yaliyopo yataelekezwa kwenye vikao ndani ya Chama.

Ingawa hawezi kuwa sahihi kwa asilimia 100 kwa alichoandika, lakini Exaud Mamuya amekuwa na haraka kidogo kutokana na kushindwa kuvumilia yeye alichoona kama ‘uchafu na hujuma’ vinayoendelea dhidi ya CHADEMA na viongozi wake.

Katika kundi hili alilolitaja Mamuya karibia wote tumeshakaa nao na mara ya kwanza Mamuya alishtuka sana aliposikia kilichokuwa kikijadiliwa kwenye kundi hilo. Pamoja na kushtuka lakini hakushangazwa sana maana hata kwenye sakata la madiwani wa Arusha anajua jinsi Mhe. Zitto alivyohusika na kumuahidi kwamba utamuunga mkono. Tulipotoka kwenye kikao kile alisononeka sana na aliniuliza mambo mengi sana kuhusu kundi hili na mengine nilipanga kuyasema ndani ya vikao hasa yale mambo ambayo ni very very sensitive.

Sasa kwa sababu kiongozi wangu Zitto Kabwe ameibuka na kujaribu kukanusha na kupotosha imebidi nije niweke sawa upotoshaji huu japo kwa kifupi:

Ndugu Zitto,

Mosi:
Sishangazwi na kauli yako kwamba hunifahamu. Ni muendelezo wa siasa zile zile za kutosimamia ukweli na kuendekeza siasa za uongo na upotoshaji. Nimemkumbuka Mwanasiasa Mzee Stephen Wassira (Aliyekitabiria CHADEMA kwamba kitasambaratika) aliposimama na kumkana Mwanafamilia wake mbele ya vyombo vya habari kwa sababu ya siasa na katika mkakati wa kuendeleza ghiliba. Kama mwanasiasa wa Tanzania anaweza kumkana hata mwanafamilia au kusema chochote hakuna la kushangaza.

Sasa, kwa kuwa ushahidi ninao wa jinsi tunavyofahamina na jinsi tulivyoshirikiana kuwashughulikia viongozi wa juu wa chama pamoja na uhusika wetu katika hujuma dhidi ya chama nitaomba chama changu sasa kiitishe kikao cha dharura ili nimwage mambo yote nyeti na ushahidi nilio nao ndani ya vikao. Naamini katika vikao kwa kuwa napenda kuona CHADEMA kikikua kama Taasisi imara ya mabadiliko.

Jana nilimwambia Dr. Kitila haya mambo baada ya wewe kuongea nae na kunitaka mimi niingie JF nikanushe thread hii iliyoanzishwa na Mamuya. Kumbe shinikizo lote ulitaka nikusafishe tu, kitu ambacho sikuwa tayari kufanya. Ushahidi nianao pia! Ulipoona imeshindikana mimi kumkana Exaud Mamuya, wewe ukaamua kuja huku kuja kunikana. Hizo rhetorics unazotumia katika dhana ya kujenga ukabila kwa kufanya ulinganisho wa Mamuya na Ben Saanane ni muendelezo wa propaganda chafu dhidi ya chama ambazo mimi na wewe tulikuwa tukizitumia kuhalalisha kazi yetu hii ambayo kimsingi niliamua kuachana nayo na sikuwa tayari kuendelea kuishiriki.

Pili:

Nigusie kidogo hizi tuhuma za ‘kuuana na kuchinjana’. Tafadhali sana naomba uwe mkweli na usimamie kauli yako ya ‘siasa za ukweli na uwazi’. Hizi siasa za uzandiki hazitufikishi popote. Hizi ni tuhuma ambazo zimekuwa zikisambazwa na kundi la akina ‘TUNTEMEKE’ ambao sote tunawajua yaani mimi na wewe. Hawa tumefanya nao kazi kubwa tangu uchaguzi wa BAVICHA. Madai haya yamekua yakitolewa na Habibu Mchange na Mtela Mwampamba wakishirikiana na Gwakisa baada ya kuona mimi sitaki kushiriki hujuma kwa chama changu.

Wamekuwa wakiandika haya hapa JamiiForums kwamba nimetumwa kukuua. Wamekuwa wakiandika walinikamata na sumu ya kutaka kukuua wewe. Leo unaleta mambo haya hapa! Pia wamekuwa wakinipigia na kunitumia message za kunituhumu kwa haya na kunitisha. Hii ni 'pre-emptive attack'.

Mmekuwa frustrated baada ya kuona jitihada zenu za kunitumia kufikia malengo yenu kwa kutumia mwanya mlioupata baada ya mimi kutoridhishwa na mchakato ule wa BAVICHA zinagonga mwamba. Chama hiki watu wamekifia. Kama kuna damu yako hata mimi na wengine tuna damu yetu hapo pia!

Kazi hii ya kuzusha tuhuma kwa mtu ambaye tunaona anatuvurugia malengo yetu tuliifanya sana na ninaijua kaka! Mmesahau tumekuwa tukifanya jitihada za kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu kwanza ili tuweze kuwashinda kwa pamoja? Hili unalijua moyoni mwako . Sasa naomba kama hutanithibitishia tuhuma hizi nitaomba kwa kuwa wewe ni kiongozi wa chama kikao kiitishwe na nitamwaga yote huko. Kama hutafanya hivyo, mimi nitaandika Barua kwa katibu mkuu ili uje unithibitishie tuhuma hizi pamoja na kundi zima la ‘Masalia’. Sitaogopa chochote na nipo tayari kwa lolote kwa kuusema ukweli. Sikutaka kujibu thread hii lakini tuhuma za kutaka kuuana ni serious allegations kwa kuwa zinahusu maisha ya mtu. Kuliko nifanye siasa za aina hii, ni bora niache siasa kaka.

Pia, vitisho vya kuaga kwenu havinihusu na wala havinitishi. Siamini kama ushirikina una nguvu kwangu na hilo unalijua na kundi lote la masalia linajua ndiyo maana ilishindikana mimi kwenda kula viapo kwa mganga wa kienyeji na unakumbuka vizuri! (Ati kula kiapo kwa kundi la masalia ili tusisalitiane katika kazi ya kukihujuma chama chetu). Afadhali Juliana Shonza na rafiki yangu Emmanuel Mwakajila waliniunga mkono katika kukataa hili. Ninaye Mungu anayenipigania na sitaogopa vitisho vyovyote. Mnanifahamu kwa hili, I dare you to challenge me! Twende kwenye vikao.

Mwisho:

WanaJF,
Mambo mengi sitaweza kuyaweka hapa kwa kuwa ni nyeti sana, nitasubiri vikikao ndani ya chama ili kikao kiitishwe nimwage huko. Nadhani safari hii tutakomesha tabia hii chafu ya baadhi ya wanasiasa kujaribu kuwatumia vijana kwa maslahi binafsi. Naamini itakuwa ni kikomo cha siasa za uzandiki na uongo ndani ya vyama vyetu vya siasa.

Wale wanaosema mimi ni mtu wa kutumika, nitapata fursa ya kuwathibitishia hayo. Sinunuliki na sina price tag. Wanaosema haya, ukweli wanaujua moyoni. Ninajiamini kwa kuwa nina taaluma yangu na miradi yangu na sinunuliki labda bei yangu ni Ukweli ambao nipo tayari pia kuulipia in return kwa gharama ya damu yangu.

Brave people, given the opportunity and even under any oppression or threat to life, stay and defend their comrade in arms and their entity....not run away and abandon it....unless something hinders their dignity and pride. Wanamapinduzi wote hufanya haya!

Nyongeza ya Mamuya:
Quote By Exaud Mamuya View Post
Nawasalimu sana ndugu zangu hapa jamvini,

Kwa kweli tokea asubuhi ya leo nimekuwa nikipitia michango mbalimbali ya wana janvi hapa na kuona ni jinsi gani ambavyo njia ya muongo huwa ni fupi.

Kwanza kabisa napenda kumwambia naibu katibu wangu mkuu ya kwamba asifikiri vijana wa miaka hii ni sawa na wale wa mfumo wa chama kimoja kipindi kile! Ameweza kujitutumua kwa kujaribu kujitetea pasipo kujibu hoja ya msingi.

Bwana Zitto Zuberi Kabwe ulichokifanya hapa ni kujaribu kuwaonyesha wana jamvi ya kuwa hatufahamiani na kuonyesha ya kwamba tunatumika na baadhi ya watu flani pasipo kujibu hoja ya msingi ya kwamba WEWE NI MFADHILI WA KIKUNDI CHA WAASI WA CHADEMA!

Bwana Zitto labda nikukumbushe na nadhani utakuwa unakumbuka vizuri siku ambayo tulikuwa wote pale MOUNT MERU HOTEL Arusha pamoja na RUGE wa Clouse Radio, Shyrose Bhanji na baada ya kuachana mlielekea NAURA SPRING HOTEL kwa ajili ya tamasha la miss Arusha na baada ya pale tulipanga kukutana lakini ulipokuja kuniuliza niko wapi nilikwambia niko TRIPLE A Club na ukaniambia umechoka unaenda kupumzika so tuonane kesho yake lakini kesho yake hatukutafutana tena. Sasa unaposema hunifahamu mimi nakushangaa sana kamanda!

Bwana Zitto ikumbukwe vizuri ya kwamba wewe ndo uliyekuwa UKICHOCHEA MGOGORO WA MADIWANI kwa lengo la kumdhoofisha mh Lema kisiasa na mipango na mikakati yote ilikuwa ikifanywa baina yangu mimi, wewe Dr Kitila Mkumbo pamoja na madiwani waliofukuzwa Chadema.

Wewe ndio uliokuwa ukiwapa moyo madiwani wa Chadema kwamba wagome mpaka dakika za mwisho na wasikubali kuomba msamaha hata mbele ya kukao cha ngazi ya juu cha chama yaani KAMATI KUU na hata ulipokuwa ndani ya kikao cha kamati kuu na madiwani wale wapo nje ya ukumbi wa kikao ulikuwa ukiwasiliana nao kwa sms ambazo walinifowardia baadae.

Nilikubali kukusikiliza kama kiongozi wangu wa juu wa chama na kutekeleza yale yote ya usaliti niliyoyafanya na hata ndiyo maana mara nyingi nilikuwa Dar nikikutana na Mchange, Mwampamba, Juliana Shonza, Gwakisa, Festo Sanga kwa ajili ya kupanga mikakati thabiti ya kuwadhoofisha viongozi wakuu wapigania ukweli ndani ya chama sana sana mh Mbowe na Dr Slaa kwa lengo la kuwagombanisha na kupata upenyo wa wewe kuwa juu kisiasa zaidi yao ( divide and rule).

Na hata Dr Kitila mkumbo alikuwa akitupa kila kitu ili kufanyikisha mkakati wa kuwafanya madiwani wa Arusha wawe juu ya mh Lema zaidi zaidi diwani Estomih Mala awe na nguvu kisiasa zaidi ya Lema.

Na hata report ya uchunguzi wa mgogoro wa madiwani wa Arusha ambao waliokuja kuchunguza alikuwa ni Dr Kitila Mkumbo na Advocate Mabere Marando pamoja na Ester iliwafikia madiwani wa chadema hata kabla ya kufikishwa kamati kuu na ndio maana madiwani wale pamoja na mimi tulikuwa tukilalamika kuna baadhi ya pages ambazo zimenyofolewa zilizokuwa zikionyesha hakuna rushwa yeyote madiwani waliyokutwa nayo. Lakini hii ni kutokana na kupata report kabla ya kuifikisha kwa kikao kilichoazimia kuunda kamati ya kuitafuta na kuiwasilisha.

Hivyo basi pasipo kuwa na kumumunya maneno ni kwamba msaliti namba moja ndani ya Chadema ni Zitto Zuberi Kabwe na hapa hawezi kupinga ukufuatilia kwenye thread niliyoandika na kufuatilia utetezi wake utaona jinsi ambavyo ndio yeye amekuwa akiwafadhili viajana hawa wasaliti ( masalia) kwa kwa kujikita kueneza propaganda za zinazotolewa na ccm za UDINI, UKABILA na UKANDA.

Rai yangu kwako bwana Zitto ni kwamba CHADEMA ni chama kinachopigania HAKI, USAWA na UKWELI, hivyo basi nakusihi urudi katika mstari ulionyooka na uungane na wapigania USAWA wenzako na uachane na njama zote za USALITI.

Na kwa tahadhari tu ni kwamba mimi tayari najihesabu TAYARI NIMESHAKUFA. Hivyo basi vitisho vyote mnavyonitumia ni kwamba haviniogopeshi hata kidogo maana katika kupigania UKWELI na HAKI najua lazima kuna kufa na mimi sintokuwa wa kwanza so niko tayari kufa bro!

Nawasilisha.

MAHAKAMA YAMBADILISHIA MASHTAKA 'LULU' ELIZABERTH MICHAEL


Mwigizaji Lulu 

MSANII Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, ameepuka adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kumbadilishia mashtaka, ambapo sasa anatuhumiwa kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo, Lulu ameepuka adhabu hiyo kwani hata kama atapatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha maisha au kuachiwa huru.
Hii inatokana na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu ya kosa la kuua bila kukusudia, ambapo anayepatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.
Hata hivyo, baadhi ya wanasheria waliliambia gazeti hili kwamba uzoefu wa adhabu nyingi za kuua pasipo kukusudia zilizowahi kutolewa nchini, ni kati ya miaka 15 na wengine waliachiwa huru.
Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Aprili 11, mwaka huu akikabiliwa na tuhuma za kumuua Kanumba Aprili 7, 2012.
Alikuwa akidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), shtaka ambalo mshtakiwa anayepatikana na hatia adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Hata hivyo, jana upande wa mashtaka ulieleza mahakamani kuwa kwa sasa imebadilisha mashtaka kutoka kuua kwa kukusudia na kuwa kuua bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha CP.
Mshtakiwa huyo alitarajiwa kusomewa mashtaka hayo mapya jana pamoja na maelezo yote ya kesi, ambapo angesomewa ushahidi wa mashahidi wote pamoja na vielelezo muhimu katika kesi hiyo.
Hata hivyo, hatua hiyo ilikwama kutokana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka anayeiendesha kesi hiyo kutokuwapo mahakamani na badala yake aliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Ofmedy Mtenga.
“Upelelezi wa shauri lako umeshakamilika na tungeweza kukusomea comital (maelezo ya kesi) leo, lakini kwa kuwa waendesha mashtaka hawapo basi tunaliahirisha mpaka tarehe nyingine.”, alisema Hakimu Mkazi Agustina Mmbando, anayesikiliza kesi hiyo katika hatua hiyo ya awali.
Taarifa hizo za kukamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo zilipokewa kwa furaha na shangwe na msanii huyo, kiasi kwamba alishindwa kujizuia kuonyesha furaha yake.
Wakili wake Peter Kibatala aliiomba mahakama itoe ahirisho fupi hadi Ijumaa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka haya mapya pamoja na maelezo ya awali.
Hakimu Mmbando alikubaliana na ombi hilo la Wakili Kibatala na akaahirisha kesi hiyo hadi Ijumaa
Baada ya Mahakama ya Kisutu kukamilisha taratibu hizo kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu ambako ndiko itakaposikilizwa.
Lulu alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 11, 2012 na kusomewa shtaka moja la mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...