Saturday, November 10, 2012

Watu wazima vikojozi


Kikojozi, au Nocturnal enuresis kwa kiingereza
kikojozi ni jina analipowa mtoto anayekojoa kitandani-kikojozi hasa wakati wa kulala.
Ni kawaida kwa watoto walio na miaka 6 kukojoa wakiwa usingizini.
..............
Lakini unajua kuwa watu wazima, akina baba na masharubu yao, au hata akina mama na vyeo vyao ni vikojozi?
Wataalam wanasema karibu watu wazima wote wamewahi kukoja vitandani wakiwa usingizini.
Utafiti unaonyesha kuwa yengi ya watu vikojozi ni wanaume. Wanaume wengi hujikojolea usiku.
...........

Baba ajikojolea akiwa usingizini
Afadhali ukojoe kitandani lakini sio kukojoa njee,
mama mmoja huko Oklahoma , Marekani anajuta kwanini alimwambia mtoto wake wa miaka 3 kukojoa njee.
Mtoto huyo Dillan Warden alikuwa amekabwa sana na mikojo, hivyo mamake akamuonya asikojoe kwenye suruale yake. alipofika mahali kando palipojificha , bi Ashley Warden akimvua mwanawe suruale ili ajisaidie.
Mara polisi wakafika pale, maskini mtoto huyo wa miaka 3 akakatwa na kutozwa faini ya dola elfu 2, mia 5 kwa kukojoa hadharani.
Ni huko Oklahoma , Marekani.
..........
Lakini kwanini mtu mzima na heshima zake au msichana mrembo au na matatizo ya kukojoa kitandani?
Daktari Zaki Almallah , mtaalam wa vibofu vya mikojo anasema taiba ya watu wazima kuwa vikojozi inarithishwa, kama baba au babu alikuwa kikojozi basi kuna uwezekano wa asilimia 40 kwa mtoto au mjukuu kuwa kikojozi ukubwani.
Wataalam katika Hospitali ya Birmingham nchini Uingereza wanasema sababu nyengine ni kutokomaa kwa tezi pituitary gland inayopatikana ndani ya ubongo chini ya sikio.
tezi hii hutoa homoni yakje a chembe cheme zake wakati wa usiku hivyo kuzuia utengenezaji wa mikojo. hivyo tezi hiyo ya pituitary gland ikiwa dhaifu au haikukomaa basi chembe chembe hizo zitatuma ujumbe kuwa mikojo zaidi itengenezwe, hivyo basi mtu kuwa na baala ya kujikojolea akiwa amelala maana ni lazima zitoke.
Mtu kuwa na stress,au msongo kuna weza kumsababishia mtu matatizo ya ukojozi.
Mheshimiwa mmoja , mkuu fulani serikalini, afrika mashariki ni kikojozi, lakini anamshukuru mkewe kwa kumvumilia?
Wewe unaweza kumvumilia mkeo au mumeo akiwa kikojozi?
............
Jee unafahamu kuwa kula kucha ni ugonjwa?
Kuna watu walio natatizo la kuuma kucha zao au kula kucha zao.
Japo utafiti unaonyesha kuwa watoto wengi hutafuna kucha zao lakini watu wazima wengi pia wana tatizo hilo la kula kucha.
Mtunzi wa kibao hicho "one more time....Mwanamuziki, Britney Spears ni mmoja ya watu wanaokiri kwamba wana matatizo ya kula kucha au kutafuna kucha zake wakiwa amekaa.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron pia yumo kwenye kundi hilo la watafunaji kucha.
................
Ugomvi ndani ya nyumba ni kawaida, ndivyo wasemavyo waswahili.
Lakini bwana Verman kutoka kijiji cha Sendhwa huko india , amezidi.
Mhindi huyo alikuwa amemchosha mkewe kwa matusi ya kila siku. Kila mara bwana Verma alikuwa akipenda kumtukana bibi yake. Bi Hema.
Gazeti la Hindustan Times limeripoti kwamba hivi majuzi Bi Hema alishindwa kuvumilia matusi ya mumewe na kuamua kumchukua binti yake mdogo na kumuachia mumewe nyumba pamoja na matusi yake.
Hivyo akasikitika sana na akaamua kukomesha tabia hiyo yake ya kumtukana mkewe kila mara.
Bwana Verma akanunua Mkasi au makasi kama wasemavyo wengine na kuukata ulimi wake.
Sasa ana ulimi nusu. Na matusi hayamtoke vizuri mdomoni.
............
Unajua kuwa Tanzania inaidadi kubwa zaidi ya watu wazima wanaokojoa vitandani kuliko kenya na hata Uganda?
Tanzania ina watu wazima vikojozi, laki 5 ! Kenya inafuata karibu kabisa kwa kuwa wanaume na wanawake laki laki 4.
Wanasayansi wanasema tatizo hilo la watu wazima kukojoa ni kubwa na linasumbua wengi lakini kwa sababu ni jambo la aibu wengi hawataki kulijadili.
Kuna mameneja wabunge na hata mawaziri ambao ni vikojozi
Takwimu zinasema kwamba katika kila watu wazima 100, mmoja wao ni kikojozi.
hivyo nchini ikiwa na idadi ya watu milioni 50 kama Tanzania, basi jua kuwa watu wazima laki 5, yaani watu nusu milioni wanaokojoa wakiwa usingizini.
Jee unajua kuwa nchini uingereza kuna chama cha vikojozi? Watu wazima wanaokojoa wakiwa usingizini mjini London wameanzisha chama kinachoitwa The Bladder And Bowel Foundation.
......
Simu ya Blackberry ni mashuhuri sana, hata Rais wa Marekani Barack Obama ana simu hiyo ya Black berry.
Lakini unajua kuwa simu hiyo ya Blackberry ina madhara? Utafiti umethibitisha kuwa Simu hii inaweza kusababisha matatizo ya kujikuna kuna. hii nikutokana na madini yaliotengenezewa simu ya Blackberry.
Mtumiaji wa simu ya Black berry pia anaweza kuwa na uvimbe au vipele mshavuni, usoni.
Wanasayansi wanasema yeyote mwenye matatizo ya Allergy basi aepuke kutumia simu ya Blackberry.
Habari ndio hiyo!
Hii ni BBC na Mimi ni Odhiambo Joseph

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...