Friday, November 9, 2012

HUYU NDIE MSHINDI WA SHINDANO LA EPIQ BONGO STAR SEARCH- 2012

Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 usiku wa kuamkia ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi, mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar).
Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura.
Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi
---
Mshiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 kutoka Dar es Salaam Walter Chilambo usiku wa kuamkia leo amekuwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi za Milioni 50 za Kitanzania.

Walter aliibuka kidedea mbele ya Salma Yusuf kutoka Zanzibar ambaye walifaikiwa kuingia naye pamoja fainali ya washiriki wawili tu kati ya watano ambao walianza fainali hiyo hapo awali. Walter ambaye dalili za ushindi wake zilianza kuonekana tangu awali mwa fainali hiyo ameweka historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kujinyakulia kitita kikubwa katika mashindano ya kusaka vipaji vya muziki.

Aidha katika shindano hilo mshiriki Walter pamoja na wenzake walipitia hatua tatu ambapo ya kwanza ilikuwa kuimba na msanii mmoja mmoja waliowachagua ambapo yeye aliimba na msanii Ditto kabla ya kuimba mwenyewe katika raundi mbili zilizofuata huku wakipigiwa kura na mashabiki katika raundi zote. Walter alitumia nyimbo moja ya Steve R n B “One Love”, na Nikikupata ya Ben Pol katika raundi zote mbili zilizofuata.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...