Saturday, November 17, 2012

KAULI YA SUMALEE KUHUSU KUTOPATA HILI GARI LAKE LILILOIBIWA, PIA KUGOMBANA NA MKEWE SABABU YA MAWAZO.



0
.
Staa wa hit single ya ‘Hakunaga’ Sumalee amesema bado hajalipata gari lake lililoibiwa octoba 29 2012 Coco beach Dar es salaam ambalo thamani yake inakaribia milioni 70 za kitanzania.
Kwenye exclusive interview na millardayo.com amekaririwa akisema “gari kusema ukweli sijaipata mpaka sasa, gari imechukuliwa na nahisi kabisa walioiba ni watu wanaonijua kwa hiyo mambo mengine siwezi kusema mpaka sasa askari wamefikiwa wapi lakini mi najua kwamba inapatikana hivi karibuni”
.
Kwenye line nyingine Sumalee amekiri kwamba mawazo ya kuibiwa gari yake yanafanya agombane mpaka na mke wake, namkariri akisema ” yani we acha tu mshkaji wangu yani mpaka nagombana na wife kwa sababu nimejikuta sasa hivi nachelewa sana kurudi nyumbani, navuta sana masigara nafanya hivi kwa sababu ya kuchanganyikiwa lakini nitarudi katika hali yangu na kusahau hichi kitu, najitahidi kufanya mambo mengine sababu nahisi naweza kupoteza kila kitu nikapoteza maisha yangu kwa sababu ya hii gari, inabidi nipambane tu mwenyewe”
Sumalee amesema sasa hivi ndio amegundua kwamba marafiki zake wengi walikua wanafiki manake wakati huu hawapo nae kabisa, hakuna anaempigia simu.
Namkariri akisema “kwa hiyo yani unakua unawajua wanafiki wako wanahisi yani kupotelewa na gari sijui ndio umeishiwa hela au umefilisika, watu wa mbali kabisa ndio wananipa support.. bora hata wangekuja kupiga mizinga hata wasema ebwana Suma hebu tukaulizie hivi, tufanye hivi kuhusu hii gari…. hakuna kitu kama hicho”
Kwa kumalizia Sumalee amesema “ndio ujue kwamba binadamu nuksi yani lakini mi nawaambia kwamba imepotea gari tu jamani sio kwamba nimepoteza maisha yangu na wala sitachanganyikiwa kwa sababu ya hiyo gari yani sitaweza tena kufanya chochote, hamna kitu kama hicho”

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...