Thursday, November 15, 2012

Kinyang'anyiro cha Urembo EAC chaja



Kenya, Rwanda zataja warembo wa East Afrika

KENYA na Rwanda zimetangaza warembo watakaowawakilisha kwenye mashindano ya Miss East Africa yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 7.

Umwari Neema (22) ndiye atabeba bendera ya Rwanda kwenye mashindano hayo wakati Joan Mwambui Ndicho (18) ataiwakilisha nchi ya Kenya.

Kwa mujibu wa muandaaji wa mashindano hayo, Rena Callist alisema warembo hao wamepatikana baada ya kufanyika mchujo maalumu uliofanyika kwenye nchi zao.

"Neema mwenye urefu wa futi 5.9 ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Kigali Institue of Education ( KIE) na pia ni mfanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo jijini Kigali," alisema Callist.

Alisema Joan ana urefu wa  futi 5.8 na anatarajia kujiunga na Chuo cha Machakos kwa ajili kusomea mambo ya utalii.

Callist alitaja nchi zitakazochuana kwenye kinyang'anyiro hicho kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoro, Seychelles, Mauritius na wenyeji Tanzania.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...