Monday, November 12, 2012

PATA HABARI ZILIZO JILI NDANI YA MKUTANO MKUU WA CCM KAULI NA SENTENSI ALIZOZITOA SHIBUDA WA CHADEMA NDANI YA MKUTANO WA CCM.


0

.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane wa Chama cha Mapinduzi unaoendelea katika Ukumbi wa Kizota nje kidogo ya Mji wa Dodoma jana usiku walisahau tofauti zao juu ya wagombea wanaowapigia debe kushinda nafasi wanazowania kufuatia hotuba ya kusisimua iliyotolewa Mbunge wa Maswa Magharibi JOHN MAGALE SHIBUDA.
Licha ya SHIBUDA kuwa na kofia ya Ubunge amefanikiwa kuhudhuria Mkutano huo wa CCM kufuatia mwaliko alioupta kupitia wadhifa wake wa Ujumbe wa Mpango wa Utathmini Kiutawala Bora kwa nchi za Afrika APRM  ambao unasimamia pia masuala ya demokrasia safi.
Akizungumza na Wajumbe zaidi ya 2000 na waalikwa takribani 4000, Shibuda amemtaka Rais JAKAYA KIKWETE kusimamia elimu ya uraia ili kuondoa dhana ya chuki inayoendelea ndani ya vyama vya siasa pale mwanasiasa mmoja anaposhirikiana na Watanzania wenzake walio katika vyama pinzani.
SHIBUDA pia hakusita kusikitishwa kwake na mdororo wa kisiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi unaochangiwa na baadhi ya viongozi kutowafikia wananchama na badala yake kutumia vyombo vya habari kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani ambayo hayana msingi.Kuhusiana na viongozi kutowajibika katika kutekeleza majukumu yao.
Mjumbe huyo pia anashindilia hoja msumari kwa Rais KIKWETE na Serikali yake kuwa wasikifu pale wapinzani wanapoibua changamoto za kimaendeleo na kuitumia fursa hiyo kwenda kuzifanyia kazi ili kuwaondolea wananchi umaskini.
Kama anavyomalizia kwa kusema ‘Kaa la Moto Haliwekwi Mfukoni’ akatumia fursa hiyo pia kubainisha azma yake ya kumtumia Rais KIKWETE na Rais wa Zanzibar DK ALLI MOHAMED SHEIN katika kampeni zake za kuwania urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...