Thursday, November 8, 2012

RAY C ANAHITAJI KUSAIDIWA, MAMA YAKE AZUNGUMZA


Mwanamuziki wa kike Rehema Chalamila maarufu kama Ray C kwasasa anaishi maisha magumu baada ya kuathiriwa na kinachosemekana  kuwa ni matumizi ya madawa ya kulevya kwa muda mrefu.
Mwanadada huyo maarufu kama kiuno bila mfupa hivi karibuni alihamishia makazi yake mjini Nairobi , Kenya, na aliporejea nchini hali yake ilikuwa mbaya.
Akizungumza na Mo blog kwa njia ya simu, mama mzazi wa Ray C,  Bi Margret Mtweve amesikitishwa na kitendo cha vyombo vya habari kuandika tu hali ya Ray C bila kuhamasisha msaada..
“kwa kweli mwanagu ninae nyumbani kwasasa nalala nae kabisa, na nimeokoka namuombea sana kwa Mungu, na ninaamini Mungu ni mwema atamsaidia” alisema Bi Margret nakuongezea.
“Mwanangu aliwasaidia watu wengi lakini sasa hivi anamatatizo sioni mtu hata mmoja wakuja kunipa msaada, zaidi ni simu za waandishi kutaka habari za kumchafua”
Mama Ray C yuko tayari kupokea msaada wowote kutoka kwa wanajamii na namba yake ya simu ni 0655 999 700 waweza mtumia hata kwa Tigo Pesa.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...