Hatimaye chaguzi za CCM katika ngazi mbalimbali ndio umemalizika, Idodomya. Ifuatayo ni tathmini yangu:

1. MAAMUZI MAGUMU
Kwa utaratibu ulioanza mwaka huu, kundi la kifo la NEC lilipunguzwa toka 20 na kubaki 10 huku wagombea wakiwa ni 31. Kutokana na woga wa viongozi wengi waliamua kukimbilia mawilayani ambako kupita ni almost guaranteed labda uwe na mpinzani wa haja kama ilivyokua kwa Mh Sumaye.

Wale WOTE 20 walioshinda NEC 2007 walikimbilia huko mfano Laighwanan, Chenge, Sumaye etc kasoro B. Membe PEKE YAKE. Katika uchaguzi wa 2007 nafasi nne za juu zilikua
1. Chenge
2. Lowassa
3. Makamba Sr
4. Membe

Membe alifanya uamuzi MGUMU, NA WA HATARI wa kujipima ubavu kama alioufanya Mwl JK Nyerere tar 12.7.1955 kuamua kuendelea kuwa Mwalimu au Siasa. Membe angeshindwa ingekuwa tabu sana kuibuka tena.Kwahiyo MH YOU DESERVE A MASSIVE PAT ON THE BACK! HATS OFF, SIR!

2. MAKUNDI
Uchaguzi umedhihirisha kuana makundi mawili. Kundi la Kwanza ni la MAFISADI ambao ni wazee wa kupiga dili za mjini na wana pesa nyingi linaongozwa na DON LA KIMASAI LAIGHWANAN TEDDY LOWASA. Kundi la pili ni la WAPINGA UFISADI likiongozwa na Mwanadiplomasia Bernard Membe. CCM ina kazi ya ziada kuyaunganisha makundi haya baada ya uchaguzi huu maana kuna chuki kali baina yao.


3. RUSHWA
Rushwa ilitawala SANA katika chaguzi hizi. Kundi la mafisadi lilitumia hela nyingi mno na kufanikiwa kujaza watu wao mawilayani pamoja na kwenye Jumuia zile 3. Hii inaonyesha kwamba kwa kiasi fulani bado kuna watu wanakubali kuuza utu wao na kununuliwa ili kumchagua kiongozi.

4. PCCB
Licha ya rushwa kugawiwa WAZIWAZI maeneo mengi eg Mahotelini, guest, ukumbini, vyooni, kwa mama ntilie, kwa wauza vocha. Kinachosikitisha SANA ni kwamba licha ya Rushwa kugawiwa WAZIWAZI lakini hakuna mtu aliyekamatwa na kushitakiwa wakati hata vyombo vya habari viliandika bila kificho kua kiwango kilikua 40,000, 70,000 na 100,000. Ipo haja kubwa ya PCCB kufumuliwa maana IMESHINDWA KAZI.

5. MAGAZETI
Katika kipindi chote hiki waandishi wengi waliweka pembeni ethics zao na kuamua kwa makusudi kabisa kumpamba LAIGHWANAN na haihitaji kua na Rocket scientist kujua kilichopelekea waandishi ambao wengine wanaheshimika sana katika jamii kumnadi TEDDY kiasi kile ndo maana vichwa vya habari vilikua "Lowasa awatimulia vumbi ccm(kana kwamba yeye si ccm), "Lowasa amtimulia vumbi Membe", 'Lowasa ni maji marefu" "Lowasa hashikiki" etc. Waandishi tuwe wazalendo jamani!

6. KUMPINGA JK KWA VIPEPERUSHI
Kundi la TEDDY kwa kuwatumia akina BASHE lilitengeneza vipeperushi ili kutaka JK asichaguliwe kua Mwenyekiti na abaki kua Rais. Hili lilifanywa kwakua kundi hilo linaamini JK yuko kwa Membe hivyo lilitaka "Mtu wao" ndie aikwae nafasi hiyo. Matokeo yake ni kuaibika kwani JK ameshinda kwa KISHINDO!

7. MANGULA
Mafisadi ambao walikua wanataka S. Wasira ndie awe M/Mwenyekiti walipigwa butwaa kuona mpinga ufisadi hodari Mh Philip Japhet Mangula ndie aliechaguliwa. Kwa hakika uteuzi huu uliwaduwaza sana akina Bashe!

8. KURA ZA ITIFAKI
Poroja kwamba chaguzi za CCM zina kura za Itifaki zilizikwa rasmi Kizota. M/Mwenyekiti mstaafu alitangaza na wote tulimuona katika runinga zetu akisema wagombea wote 31 wa kundi la kifo wanaruhusiwa kwenda kushuhudia kura kuhesabiwa au kutuma wawakilishi wao. Wagombea 25 kati ya 31 walienda wenyewe na 6 walituma wawakilishi na kura zilihesabiwa chini ya Spika Mh. A. makinda.

9. KURA 1,455 ZA MEMBE
Suala kubwa la kujiuliza ni wapi zilitoka kura hizi. Teddy kwa kumtumia Bashe alieleza wazi kua juhudi yao kubwa ni kumchinjia baharini Membe ili asiwemo kwenye TOP TEN kwa hali yoyote. Walitumia kila njia waliyoijua na kila hila na pesa nyingi lakini Membe, kama alivyoahidi kabla ya uchaguzi kua atawashangaza, akaibuka kidedea! Je hoja kwamba TEDDY ana watu wengi vikao vya ccm ni porojo tu? Je watu walikula hela na kumpigia Membe? Bashe baada ya kuona Membe KAWATIMULIA VUMBI bila aibu akabadili "goal posts" na kudai eti "Membe mwenyewe kashinda kwa kura kiduuuuchu, hakuwemo tatu bora wala tano bora na kwanza kashindwa na watoto eg January, Nchemba ".

Membe hakusema atakuwa wa kwanza wala tano bora ila alisema atawashangaza wabaya wake na kweli amewashangaza na kubaki WAMEDUWAA! Kua wa kwanza au wa mwisho haina impact yoyote kwenye kuteuliwa na chama kupeperusha bendera. 2002 kundi la akina Sumaye lilolkua likimwogopa sana JK lilimfanyia mizengwe SANA JK ili asifanye vizuri kundi la kifo NEC la wagombea 20. Matokeo yake JK akawa wa 18 kati ya 20 ambapo akina Sumaye, Malecela walingara. JK ndiye akaja kuwa mgombea wa ccm 2005 licha ya kuibuka wa 18 NEC!!!

10. KUBADILISHWA SIKU YA UCHAGUZI WA TOP TEN NEC
Uchaguzi wa wajumbe 10 wa kundi la kifo ulikua ufanyike sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti na M/Mwenyekiti siku ya tarehe 13.11.2012. Baada ya kushtukia kwamba LAIGHWANA na kundi lake la mafisadi wameandaa dina jumapili ili kugawa mikwanja kwa wajumbe, CCM ilibadili na Mh Msekwa akatangaza kwamba uchaguzi huo utafanyika mapema. Kitendo hiki kilikua ni pigo kwa Mafisadi. CCM INA WENYEWE!!

11. THINKTANKS WA MAFISADI
Ni dhahiri mafisadi wana mbumba za kufa mtu but tatizo washauri wanaomzunguka TEDDY ni waganga njaa wasio na mikakati kwani kwao wanadhani ukiwa na hela kila kitu kinawezekana mf M. Mahanga, P. Serukamba, Bashe, etc. Lazma mjue mikakati.

USHAURI KWA TEAM LAIGHWANAN:

"Mgombea" wenu ana madoa makubwa SANA mawili ie 1. Mwalimu Nyerere alimkataa 2. Fisadi. Haya ni madoa makubwa sana ambayo yanahitaji JIKI special ili kumsafisha na sidhani kama itawezekana. Suala la kwanza ni Nyerere PEKEE ndie angemsafisha but sasa hayupo. Mwaka 2005 wakati Malecela anagombea niliandika makala kwenye RAI kua Malecela hatapita kwenye CC maana Nyerere alimkataa. Nilibezwa na kutukanwa sana na wapambe wake waliokua na uchu wa kwenda magogoni, THE REST IS HISTORY! Suala la pili nalo ni gumu mno maana migao ya pesa inayoenda miskitini, makanisani, etc vyote ni hongo tu.
Sasa nashauri MJIPANGE vinginevyo itakula kwenu.

MATOKEO YA UCHAGUZI YAMEDHIHIRISHAPASINA SHAKA KUWA
1. HAMUMUWEZI MEMBE
2. KUWA NA PESA BILA MIKAKATI THABITI NI KUPOTEZA MUDA.