Sunday, November 18, 2012

Upatikanaji wa Katiba Mpya kabla ya 2015 wapingwa

 “Haya mambo hayawezi kukamilika 2014, ikumbukwe kuwa inahitajika miaka miwili baada ya Katiba Mpya kuzinduliwa kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuweka sheria zitakazosaidia utekelezaji wa Katiba husika,” alisema Kibamba

JUKWAA la Katiba Tanzania  limetaka sheria ya mabadiliko ya Katiba irekebishwe ili mchakato wa kupata Katiba Mpya  uendelea baada ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kwa kuwa inahitajika miaka miwili zaidi ya kuweka sheria zitakazosaidia utekelezaji wa Katiba hiyo mpya.
Limesema kuwa ili kuufanya uchaguzi wa  Mkuu ujao kuwa wa haki, bila malalamiko yoyote Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa inatakiwa kufanyiwa marekebisho kwa ajili ya kusuka upya upatikanaji wa watendaji wa Tume ya uchaguzi ili tume hiyo iwe huru na isifungamane na upande wowote.
Kauli hiyo imekuja wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba kesho ikitarajiwa kuendelea na awamu ya mwisho ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Simiyu, Geita, Mara na Mjini Magharibi.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Jukwaa hiyo, Deus Kibamba alisema ipo haja ya kutenganisha mchakato wa Katiba Mpya na ule wa uchaguzi mkuu, taifa lijipange  kutokuwa na Katiba hiyo kabla ya uchaguzi ujao.
“Mchakato huu unatakiwa kuendelea baada ya uchaguzi mkuu na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatakiwa kuongezewa muda ili ifanye kazi kisheria na sio kukimbiza mchakato huu ili kuwahi muda uliopangwa na Serikali” alisema Kibamba.
Alitaja hatua zinazohitaji muda zaidi ambazo zitafuata baada ya  tume hiyo  kukamilisha hatua ya ukusanyaji maoni ya wananchi kuwa ni, kuundwa kwa mabaraza ya Katiba, kuandaliwa ripoti ya ukusanyaji wa maoni, rasimu ya Katiba, Bunge maalumu la Katiba, kupigwa kwa kura za maoni pamoja na uzinduzi na utekelezaji.
“Haya mambo hayawezi kukamilika 2014, ikumbukwe kuwa inahitajika miaka miwili baada ya Katiba Mpya kuzinduliwa kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuweka sheria zitakazosaidia utekelezaji wa Katiba husika,” alisema Kibamba na kuongeza:
“Maana yake ni kwamba hata tungepata Katiba kabla ya uchaguzi ujao, hatutakuwa na muda wa kuweza kukamilisha maandalizi yote ili tuweze kutumia Katiba hiyo mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2015.”
Alisema ili kuepusha mvutano katika uchaguzi mkuu ujao Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili ipatikane Tume huru ya uchaguzi.
“Tume hii itakuwa na jukumu la kuandaa wapiga kura, kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi mkuu wa 2015, pia kusimamia uchaguzi wowote ule utakaofanyika wakati wa mchakato wa Katiba” alisema Kibamba.
Alisema kuwa unatakiwa kuandaliwa muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba utakaoifanya Katiba ya sasa kuzungumzia uandaaji, usimamizi na uratibu wa uchaguzi wa aina zote kwa mtitiriko mzuri na  kufafanua , “Tunataka tume kuwa na muundo kuanzia ngazi ya taifa hadi wilaya.”
Alisema kuwa muswada huo unatakiwa kuzingatia misingi ya uchaguzi mkuu kufanyika sambamba na uchaguzi wa Serikali za mitaa, maamuzi juu ya uchaguzi kufanyika lini yashirikishe wananchi, kuzuia vurugu katika uchaguzi,

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...