Tuesday, January 8, 2013

Hatari: Mke amfumania mumewe akilawitiwa!!!

SOURCE JAMII FORUMS


Nianze kwa kuwatakia heri na fanaka katika mwaka mpya wa 2013.

Hili ninaloliandika limemtokea jirani yangu, ambaye pia tuna mahusiano ya kiofisi zaidi - niliwafanyia kazi fulani ofisini kwao hivyo tukajenga mawasiliano ya kikazi, na kwa vile ni majirani basi kukawa na kaukaribu fulani hivi.

Juzi nikapata taarifa kwamba amelazwa hospitali anaumwa. Kiungwana nikaenda kumjulia hali hospitali; si nikamuuliza nini kinamsumbua, lol alichonijibu ndiyo kilichosababisha nianzishe huu uzi.

Siku ya tukio bidada aliondoka asubuhi kwenda kazini kama kawaida yake, huwa anawahi kutoka kabla ya mumewe ambaye ofisi yake ipo karibu zaidi na nyumbani. Muda wa saa nane hivi akalazimika kurudi nyumbani kwa kuwa alikuwa hajisikii vizuri akahitaji kupumzika (kawaida hutoka kazini saa 11 na kufika home around saa 12). Anasema alipokaribia mlango wa mbele wa nyumba yao akawa anasikia sauti za miguno ambazo si za kawaida, akaingia kupitia jikoni, akamuuliza housegirl ni nini hicho nakisikia, binti anamtolea macho tu bila kumjibu. Kumbe binti alikuwa anajua kinachoendelea ila akashindwa amwambieje boss wake!

Kuingia chumbani alichokikuta hakukiamini, anamwona mumewe ameinamishwa analawitiwa na rafiki wa mumewe ambaye anamfahamu vizuri na kumheshimu kama shemeji! Akazirai hapohapo, kushtuka ndio anajikuta yupo hospitali.

Huyu dada yupo kwenye ndoa na mumewe kwa miaka tisa sasa na wana watoto wawili. Anasema hakuwahi hata kuhisi kama mumewe ni shoga. Hana hamu tena kuendelea na ndoa.

Ushauri wenu wana MMU tafadhali dada afanyeje? Ndio ameshamkuta mumewe akiliwa na mwanaume mwingine, tena chumbani kwao, juu ya kitanda chao anacholala yeye na mumewe! Tena mume mtu ndio kanogewa na anatoa miguno na sauti za mahaba!

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...