Saturday, January 19, 2013

MSHITAKIWA WA KESI YA WIZI WA FEDHA KATIKA AKOUNTI YA MADENI YA NJE (EPA) AJIU KWA KUJIPIGA RISASI

 
Suleiman Kova 

MSHTAKIWA wa kesi ya wizi wa Fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania, Ajay Somani
amefariki dunia baada ya kujipiga risasi.
Habari zilizolifikia Mwananchi Jumamosi wakati tunakwenda mitamboni na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, zinasema kuwa Jay alijipiga risasi jana asubuhi, maeneo ya Upanga karibu na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
“Alijipiga risasi saa 2 asubuhi nyumbani kwake Upanga, karibu na Hospitali ya Muhimbili.”, alisema Kamanda Minangi na kuongeza kuwa haijajulikana tukio hilo kwa kwa hakuacha ujumbe wowote.
Jay alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa pesa hizo kiasi cha Sh5.9, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yeye pamoja na ndugu yake Ajay Soman, ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatika na hatia katika kesi nyingine ya EPA.
Mbali na ndugu hao wawili, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kanda wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na binamu yake Frijala Hussein, ambao tayari wanatumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kesi nyingine tatu za EPA.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni waliokuwa wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni na Bosco Kimela aliyekuwa Kaimu Katibu wa BoTna Imani Mwakosya, ambapo walisomewa maelezo ya awali Julai 26, 2012 na kesi hiyo iko katika hatua ya usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...