Saturday, January 19, 2013

YANGA YAFANYA KWELI, TEGETE NI BALAAA


Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Yanga Frank Domayo,akiwatoka mabeki wa Black Leopard yaAfrika Kusini katika mechi inayoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Picha na Jackson OdoyoDar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga,Jerry Tegete ameanza kuonyesha matunda ya Uturuki, baada ya kufanikiwa kuipatia timu yake bao la kuongoza kwa njia ya penalti,Tegete alifunga bao hilo  baada ya mabeki wa timu ya  Black Leopard ya Afrika Kusini kumchezea rafu kiungo mshambuliaji wa Yanga Haruna Niyonzima katika eneo la hatari.

Tegete alifunga bao hilo katika kipindi cha kwanza cha mchezo,Yanga ambayo imeonyesha uwezo mkubwa katika kipindi cha kwanza baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika mechi hiyo.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa na dakika 15 baadaye Didier Kavumbagu akapachikia bao la pili.
Tegete ambaye ameanza kuishawishi benchi la unfundi pamoja na mashabiki wa Yanga kwamba hakubahatisha kufunga mabao Ulaya,alipachika bao la tatu na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kulipuka kwa shangwe Uwanjani
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Haruna Niyonzima akiwa chini baada ya kuchezewa rafu katika eneo la hatari na mabeki wa Black LeopardYanga ilicheza soka safi ya kitabuni hasa baada ya kufanikiwa kutawala sehemu ya kiungo.
Mbali na Tegete kuipaisha Yanga katika mechi hiyo kiungo Adhuman Iddi alikuwa nyota ya mchezo baada ya kuwa nguzo ya kati katika mechi hiyo.
Hata hivyo Black Leopard ilipata bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penalti. baada ya beki ya Yanga kumchezea rafu mbaya mshambuliaji wa timu ya Black Leopard kutoka Afrika Kusini.



No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...