Tuesday, February 19, 2013

SASA WAWEZA KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAPA

CLICK HAPA CHINI KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE LINK-01: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2012 LINK-02: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2012 LINK-03: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2012

HAYA SASA MAAJABU ASILIMIA 60% YA MATOKEO KIDATO CHA NNE WAMEFELI, TUNAELEKEA WAPI?

Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne. Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806. “Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa. Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani. Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo. Ufaulu kwa madaraja Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997. Waliopata daraja la tatu ni 15,426, wavulana 10,813 na wasichana 4,613, waliopata wa daraja la nne 103,327, wavulana 64,344 na wasichana 38,983 huku waliopata sifuri wakiwa 240,903, wavulana 120,664 na wasichana 120,239. Shule 20 bora Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wizara ilitaja shule 20 zilizofanya vizuri badala ya 10 kama ilivyozoeleka, kati yake 18 zilikuwa za watu binafsi na mashirika ya dini na mbili za Serikali. Shule hizo ni pamoja na St.Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Boys ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Rosmini ya Tanga, Canossa ya Dar es Salaam, Jude Moshono ya Arusha, St. Mar’s Mazinde Juu ya Tanga, Anwarite Girls ya Kilimanjaro na Kifungilo Girls ya Tanga. Nyingine ni Feza Girls ya Dar es Salaam, Kandoro Sayansi Girls ya Kilimanjaro, Don Bosco Seminary ya Iringa, St. Joseph Millenium ya Dar es Salaam, St. Iterambogo ya Kigoma, St. James Seminary ya Kilimanjaro, Mzumbe ya Morogoro, Kibaha ya Pwani, Nyegezi Seminary ya Mwanza na Tengeru Boys ya Arusha. Shule 10 za Mwisho Kwa upande wa shule 10 za mwisho, iliyofanya vibaya zaidi ni Mibuyuni ya Lindi, Ndame ya Unguja, Namndimkongo ya Pwani, Chitekete ya Mtwara, Maendeleo ya Dar es Salaam, Kwamndolwa Tanga, Ungulu Morogoro, Kikale ya Pwani, Mkumba na Tongoni za Tanga. Matokeo yaliyofutwa Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu na kuandika matusi. Baadhi ya udanganyifu huo ni karatasi za majibu kuwa na mfanano usio wa kawaida, kukamatwa na simu za mkononi kwenye chumba cha mtihani, kukutwa na karatasi au madaftari pamoja na kubadilishana karatasi za majibu. Dk Kawambwa alisema matokeo ya watahiniwa 28,582 yamezuiwa kwa sababu ya kutolipa ada ya mtihani na wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja. Matokeo ya QT Dk Kawambwa alisema waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) walikuwa 21,310, wasichana 13,134 na wavulana 8,176 na waliofanya ni 17,137 sawa na asilimia 80.42... “Watahiniwa 5,984 kati ya 17,132 waliofanya mtihani huo wamefaulu.” Waziri akwepa Kabla ya kutangaza matokeo hayo, Waziri Kawambwa alitumia muda mwingi kuzungumza sababu za yeye mwenyewe kuamua kutangaza matokeo hayo badala ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mirihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako kama ilivyozoeleka. “Najua kila mtu ana shauku ya kusikia matokeo leo, naona mkimwangalia Katibu (Dk Ndalichako) hapa, lakini mimi kwa kujua jambo hili, nimeona kwa nini nimbebeshe jukumu hilo zito wakati waziri mwenyewe mwenye dhamana hiyo nipo! Ndiyo nimekuja niwape matokeo haya,” alisema Dk Kawambwa. Baadaye Dk Kawambwa aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na haraka hivyo asingekuwa na muda wa kujibu maswali, huku akitumia muda mwingi kuzungumza mambo yaliyokuwa nje ya matokeo aliyotarajiwa kuyasoma. Pia alikwepa kujibu maswali ya msingi likiwamo kutaja majina ya wanafunzi bora pamoja na majina ya shule 10 bora zenye wanafunzi chini ya 40 akisema anajua umuhimu wa kueleza mambo hayo, lakini wataalamu wake wamekwepa kuandika kila kitu katika taarifa hiyo kwa kile alichoeleza kukwepa kuwa na taarifa ndefu. Taarifa iliyosomwa na waziri kwa waandishi ilikuwa na karatasi nne. Ufaulu mwaka 2011 Kwa mujibu wa matokeo ya mwaka 2011, ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule ulionyesha kuwa watahiniwa 33,577 sawa na asilimia 9.98 walifaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu. Wasichana waliofaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 10,313 sawa na asilimia 7.13 na wavulana 23,267, sawa na asilimia 12.13. Waliopata daraja la nne mwaka huo walikuwa 146,639 sawa na asilimia 43.60. Wavulana 87,039 sawa na asilimia 45.40 na wasichana 59,600, sawa na asilimia 41.22 huku waliofeli wakiwa 156,089 sawa na asilimia 46.41, kati yao wavulana wakiwa 81,418 sawa na asilimia 42.47 na wasichana 74,667, sawa na asilimia 51.64.

JUKWAA LA KIKRISTO MBEYA LATOA TAMKO

Akina mama wakilia baada ya kifo cha ghafla cha Padri Evarist Mushi kilichotokea jana asubuhi kwa kupigwa risasi muda mfupi kabla ya kuanza misa ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki la Kigango cha Mtoni, Zanzibar. Picha na Martin Kabemba. JUKWAA la Kikristo Tanzania (TCF) katika Mkoa wa Mbeya, limetoa tamko la kuitahadharisha Serikali na kuitaka ichukue hatua za haraka za mata na kuwafikisha kwenye vyobo vya sheria wote waliohusika na mauaji ya Padri, Evarist Mushi. Akisoma tamko hilo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa na maaskofu, mapadri na wachungaji, Katibu wa Jukwaa hilo, Askofu Damianus Kongoro, alisema kuna mambo yanayotendeka waziwazi yakiwa na athari kubwa kwa amani na ustawi wa nchi na wananchi kwa jumla. Alisema mambo hayo ni pamoja na uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya watu wasiopenda amani lakini hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa na Serikali kuwashughulikia. Askofu Kongoro alisema kuuawa kwa wachungaji, mapadri na maaskofu kuanza kutoa matokeo mabaya. Alisema hatua zinazochukuliwa na Serikali haziridhishi wala kukidhi matakwa ya wananchi wapenda amani na badala yake, Serikali inakaa kimya au inachukua hatua ambazo kimsingi, hazitatui tatizo. *Habari na Salma Said na Elias Msuya, Zanzibar, Brandy Nelson, Mbeya na George Njogopa, Dar.

Monday, February 11, 2013

ZIJUE SIFA ZA "MWANAUME ANAYETAKA KUWA SERIOUS NA WEWE


Photo: ZIJUE SIFA ZA "MWANAUME ANAYETAKA KUWA SERIOUS NA WEWE
 


1. ANABADILIKA

 Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha 



2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA

Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari Kufunga Ndoa, Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza Kuwahudumia Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo Hapo Baadaye Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha Hali Yao Kiuchumi.

Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta Miradi Mingine Nje Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha Kujikimu Na Hali Ya Maisha. Kama Alikuwa Anaishi Na Wazazi Atapanga Chumba Na Ataanza Kujitemea.

3. ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA 

Njia Nyingine Ya Kugundua Mwanaume Aliye Tayari Kwa Ndoa Ni Pale Unapotembea Naye Barabarani, Anawafurahia Watoto Mnaokutana Nao Njiani Na Mara Kwa Mara Ataonekana Kukueleza Jinsi Atakavyowafanyia Watoto Wake Mara Baada Ya Kuwapata Hapo Baadaye.

Mwanaume Huyo Pia Huwa Na Tabia Ya Kufurahia Maisha Ya Ndoa Ya Watu Wengine Yaani Anapomuona Mke Na Mume Wakiwa Na Mtoto Wao Basi Hutamani Sana Mngekuwa Nyinyi. Mnapotoka Hukuita Mke Wake!

4. NI RAFIKI LAKINI NI MUME KAMILI

Mwanaume Anayetaka Kuoa Anakuwa Ni Rafiki Yako Tu Kwa Sababu Hamjafunga Ndoa, Lakini Matendo Anayokufanyia Hayana Tofauti Na Yale Ya Mtu Kwa Mkewe. Kwa Mfano Kupanga Mipango Ya Baadaye Ya Maisha Yenu, Kukutambulisha Kwa Ndugu Na Rafiki Zake. Huwa Na Hamu Ya Kutaka Kujua Matatizo Yako Na Kukusaidia Na Wakati Mwingine Kukushirikisha Katika Matatizo Yanayomkabili.


5. HUFURAHIA UKARIBU

Mwanaume Aliyetayari Kuoa Hupenda Kuwa Karibu Na Mpenzi Wake Na Asilimia Kubwa Ya Mazungumzo Yake Atayaelekeza Katika Maisha Si Ngono. Atajitoa Kusaidia Ndugu Wa Mke Kila Linapokuja Tatizo. Na Atalalamika Anapotengwa Na Familia Ya Mchumba Wake.

1. ANABADILIKA

Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha



2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA

Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari Kufunga Ndoa, Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza Kuwahudumia Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo Hapo Baadaye Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha Hali Yao Kiuchumi.

Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta Miradi Mingine Nje Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha Kujikimu Na Hali Ya Maisha. Kama Alikuwa Anaishi Na Wazazi Atapanga Chumba Na Ataanza Kujitemea.

3. ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA

Njia Nyingine Ya Kugundua Mwanaume Aliye Tayari Kwa Ndoa Ni Pale Unapotembea Naye Barabarani, Anawafurahia Watoto Mnaokutana Nao Njiani Na Mara Kwa Mara Ataonekana Kukueleza Jinsi Atakavyowafanyia Watoto Wake Mara Baada Ya Kuwapata Hapo Baadaye.

Mwanaume Huyo Pia Huwa Na Tabia Ya Kufurahia Maisha Ya Ndoa Ya Watu Wengine Yaani Anapomuona Mke Na Mume Wakiwa Na Mtoto Wao Basi Hutamani Sana Mngekuwa Nyinyi. Mnapotoka Hukuita Mke Wake!

4. NI RAFIKI LAKINI NI MUME KAMILI

Mwanaume Anayetaka Kuoa Anakuwa Ni Rafiki Yako Tu Kwa Sababu Hamjafunga Ndoa, Lakini Matendo Anayokufanyia Hayana Tofauti Na Yale Ya Mtu Kwa Mkewe. Kwa Mfano Kupanga Mipango Ya Baadaye Ya Maisha Yenu, Kukutambulisha Kwa Ndugu Na Rafiki Zake. Huwa Na Hamu Ya Kutaka Kujua Matatizo Yako Na Kukusaidia Na Wakati Mwingine Kukushirikisha Katika Matatizo Yanayomkabili.


5. HUFURAHIA UKARIBU

Mwanaume Aliyetayari Kuoa Hupenda Kuwa Karibu Na Mpenzi Wake Na Asilimia Kubwa Ya Mazungumzo Yake Atayaelekeza Katika Maisha Si Ngono. Atajitoa Kusaidia Ndugu Wa Mke Kila Linapokuja Tatizo. Na Atalalamika Anapotengwa Na Familia Ya Mchumba Wake.

9-Year-Old Girl, Gives Birth To Baby Girl In Mexico




 

A 9-year-old girl in Mexico has reportedly given birth.

The girl, identified as "Dafne" by The Telegraph, reportedly delivered a 5.7 pound baby by cesarean section on Jan. 27 in Zoquipan Hospital in Jalisco, an area in western Mexico.


The girl was 8 years old when she became pregnant. "This is a rape or child sex abuse case," Corona added, according to the Agence France-Presse. The age of sexual consent in Mexico is 12, according to UNICEF.


"The father is a boy who is 17, but we have not found him, since he ran away," the mother of the girl told officials, according to the AFP.


“Due to her young age, we don’t know if she is being entirely truthful,” Lino Ginzalez Corona, spokesperson at Jalisco State Prosecutor’s Office, said in a press conference, ABC reports.


The new mother is one of 11 children, according to ABC, and her parents were unable to watch her while they worked.

There have been only a handful of recent reported births among children this young, including a 10-year-old Colombian girl who gave birth last year, and a 9-year-old Chinese girl who gave birth to a healthy baby boy in 2010.

MWANAFUNZI AUAWA,ANYOFOLEWA VIUNGO

 
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro.


MWANAFUNZI wa darasa la sita Shule ya Msingi Kasumulu, Kata ya Ngana, wilayani Kyela, Kaselema Mpale (14)  ameuawa kikatili kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali, kisha kunyofolewa baadhi ya viungo vyake sehemu ya mwili.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Lucia Kamnyonge alisema tukio hilo lilitokea     Februari 8, mwaka huu saa 1:30 usiku, alipotumwa na baba yake kwenda nyumba ya jirani kuchukua mpunga ambao ungetumika kwa chakula usiku.
Kamnyonge alisema mtoto wake hakupatikanika hadi alipokutwa siku ya pili yake, akiwa amechinjwa na kunyofolewa baadhi ya sehemu zake za mwili ambazo ni pua, mdomo, jicho, kuondolewa sehemu zake za siri na kuchunwa ngozi ya kichwa karibu na utosi na mwili wake kutundikwa juu ya mti.
Aliendelea kuwa baada ya hali hiyo taarifa ilipelekwa ofisi ya serikali ya kijiji, uliitishwa mkutano wa wananchi wote na walitawanyika kuanza  kumtafuta mtoto huyo bila ya mafanikio.
Baadaye, baba yake alimkuta juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ibungumbati lilipotokea tukio hilo, Adam Mkese alidai tukio hilo limewashtua na kwamba, mkutano wa kijiji ulioitishwa kwa dharura wananchi walimhusisha baba mzazi wa mtoto huyo na mauaji hayo.
Mkese alidai watu wa kijiji hicho walimhusisha kutokana na mazingira tata ya kifo chenyewe na maelezo ya kujichanganya aliyoyatoa.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Naomi  Charles alidai kuna dalili za mzazi huyo kuhusishwa na mauaji hayo na kwamba, polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho,  Baruti Mwakasala alidai kuwa hali katika kijiji hicho siyo nzuri na kushukuru polisi kwa hatua za haraka walizochukua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kukiri kumshikilia baba mzazi wa mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi.

WAISLAMU, WAKRISTO WACHINJANA GEITA

Suala la nani achinje nyama limeibua vita kali kati ya wakristo na waislamu wilayani Chato mkoa wa Geita. Vyanzo vyetu vinatuambia mtu mmoja ameshafariki.
 

Majeruhi Abdalah Ibarihim akiwa amejeruhiwa vibaya baada ya kukatwa mapnga kichwani na watu wanaodaiwa kuwa ni Wakristo.


Steven Andrea (34) ambaye anadaia kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni waislamu.

Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi..

BABA MTAKATIFU, PAPA BENEDICT XVI ATANGAZA KUACHIA MADARAKA

 
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.
Katika taarifa yake, Papa amesema amefikia uamuzi huo ambapo sasa ana umri wa miaka 85.
Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe 28 Februari, mwaka huu saa mbili kamili asubuhi.
Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika.
Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki, linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima.
Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Bene

ZIJUE NJIA ZA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


Wanaume Wengi Hapa Duniani Huamini Kuwa, Mwanaume Hasa Ni Yule Anayeweza Kufanya Tendo Hilo Kwa Muda Mrefu Na Mara Nyingi Ndio Maana Vijana Wengi Utawasikia Wakijisifu Kuwa, Mpenzi Wake Hakulala Usiku Mzima Kutokana Na Dozi Ya Maana Aliyompa Na Ukimuuliza Mtu Wa Namna Hii Atakwambia Kuwa Alikwenda Mizunguko Sita Usiku Mzima.

Hata Hivyo, Ukweli Ni Kuwa, Watu Wengi Hufikia Hatua Ya Kusema Uongo Ili Waonekana Kuwa Ni Wanaume Hasa Mbele Ya Wenzao Huku Wengine Wakigubikwa Na Nadharia Kuwa Ukubwa Wa Uume Unaashiria Jinsi Gani Walivyo Wanaume Kitu Ambacho Si Kweli.

Ni Mtazamo Huu Ndio Unaowafanya Wanaume Wakitaniwa Au Kuambiwa Kuwa Wako Kama Wanawake Wanaweza Waue Mtu. Tunaamini Kuwa Uanamke Ni Udhaifu Na Uanaume Ni Ushujaa Fulani Hivi.
Wakati Hali Ikiwa Hivyo, Hivi Sasa Wanaume Wengi Wamekuwa Wakihangaika Na Jambo Moja Kubwa, Kutafuta Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume Ili Kujiongezea Heshima Faragha!
Ukitaka Kuthibitisha Hili Jaribu Kuangalia Karibu Katika Kila Gazeti Utakalo Soma, Ni Nadra Sana Kukosa Tangazo Dogo La Biashara Lililotolewa Na Mganga Wa Kienyeji Anayejigamba Kuwa Anazo Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume, Na Matangazo Hayo Hayaishii Magazetini Tu, Bali Hata Redioni Pia Yapo.

Mbaya Zaidi Dawa Zinazoongelewa Hupewa Majina Mengi Ya `Kusisimua` Kama Kombora, Simba Na Nyati Siushasikia Mziki Wa Nyati Akikasirika Sasa Jenga Picha Nuvu Ya Hiyo Dawa, Hata Hivyo, Dawa Nyingi Ni Uzushi Tu Na Hupewa Majina Hayo Ili Kuwavuta Wateja Na Kuwashawishi Kuzijaribu, Enewei Ndivyo Biashara Zilivyo.

Wingi Huu Wa Matangazo Umeanza Kuonekana Katika Miaka Ya Hivi Karibuni, Na Kadiri Siku Zinavyozidi Ndivyo Idadi Ya Waganga Wanaojigamba Kuwa Na Dawa Hizo Inavyozidi Kushamiri, Kuna Waganga Wenye Dawa Za Kiswahili, Kiarabu Na Za Kichina Ndio Usiseme!
Binafsi Utitili Wa Matangazo Haya Umenifanya Niamini Kuwa, Kuna Tatizo Kubwa La Wanaume Kupungukiwa Nguvu Hizo, Na Ingawa Hakuna Utafiti Wa Kitaalamu Uliofanywa Rasmi, Lakini Inaonyesha Kuwa Tatizo Hilo Kwa Sasa Ni Kubwa Sana Na Si Tanzania Tu, Bali Ni Dunia Nzima.

Kutokana Na Hali Hiyo Ndipo Waganga Wa Kienyeji Pamoja Na Makampuni Mengi Makubwa Duniani Hujaribu Kuelekeza Nguvu Zao Katika Kufanya Utafiti Wa Kutengeneza Dawa Za Kusaidia Watu Wenye Tatizo Hilo, Na Bahati Nzuri Kwa Makampuni Na Waganga Hao Ni Kwamba Inaonekana Kama Biashara Inawaendea Vizuri.

SABABU ZA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME:

1. Kuna Wakati Pia Upendo Unapopungua Na Mvuto Unapungua Baina Ya Wanandoa, Mwanaume Anaweza Kujikuta Kila Akiwa Faragha Anashindwa Kuendesha Gari Kwa Muda Mrefu Na Anaweza Kudhani Kuwa Ana Matatizo Kumbe Hali Hiyo Inamkumbwa Kutokana Na Kutokuvutiwa Na Mwenzi Wake.

Tatizo Kama Hili Linaweza Kutatuliwa Kwa Kumueleza Wazi Mkeo Ama Mpenzi Wako Jinsi Gani Anaweza Kujipanga Na Kuonekana Na Mvuto Wa Hatari Utakaokufanya Uchanganyikiwe Kila Umuonapo Na Hata Mkiingia Kwenye Mambo Fulani Basi Kwa Hakika Utahamasika Na Kutoa Dozi Ya Maana.


2.Uchovu Wa Kazi Za Ajira

Mkufunzi Wangu Wa Saikolojia Katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Iringa Ambaye Ameshatangulia Mbele Za Haki, Pro. Samuel Mshana (Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi) Aliwahi Niambia Kuwa Wanawake Wanataka Security Kutoka Kwa Mwanaume Nami Nikamtania Pro. Sasa Mbona Mimi Na Mwili Mdogo Nitampa Ulinzi Gani Mwanamke Akacheka Kisha Akaniambia Ulinzi Naouzungumzia Ni Wa Jumla Ikiwa Ni Pamoja Na Kuhakikisha Mambo Yanakwenda Sana Ndani Ya Nyumba Yani Watoto Wanakwenda Shule Na Mambo Ya Mlo Wa Uhakika.

Hivyo Ni Wazi Kuwa Wanaume Huhangaika Kwa Kiasi Kikubwa Kuhakikisha Wanamudu Majukumu Yao Ya Kila Siku Na Huko Makazini Kuna Mauzauza Mengi Na Usiombe Ufanye Kazi Kwenye Kampuni Binafsi Kila Kukicha Wewe Upo Roho Juu Sasa Katika Hali Kama Hiyo Ukikutana Na Mwenzi Wako Kunako Majambozi Utahisi Una Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Kwani Mara Tu Baada Ya Kumaliza Mshindo Wa Kwanza Hutoweza Kurudia Tena! Hali Ni Hivyo Hivyo Kwa Watu Wanaofanya Kazi Nzito Zinazosababisha Wajikute Wanarudi Majumbani Wakiwa Wamechoka.

Hivyo Basi, Endapo Nawe Ni Miongoni Mwa Watu Wanaokumbana Na Tatizo La Kushindwa Kurudia Majambozi Kwa Sababu Ya Uchovu Na Msongo Wa Mawazo Kutoka Kazini Hakikisha Unapanga Muda Muafaka Na Mwenzi Wako Kupeana Raha.

Mfano Kama Jumamosi Unafanya Kazi Nusu Siku Ukitoka Usiende Kulewa Kama Ni Mtu Wa Kinywaji Bali Nenda Kapumzike Kisha Kesho Yake Waweza Kumtoa Out Mama Na Kwenda Mazingira Tofauti Kupeana Kitu Roho Inapenda Hakika Utajishangaa Jinsi Utakavyomudu Majambozi.


3. Kuchacha


’ Ebwana Usije Ukawa Katika Hali Mbaya Kifedha Na Kila Jambo Unalolipanga Linakwenda Ndivyo Sivyo Hali Inayokusababishia Uchache Kisha Mwenzi Wako Akakuomba Unyumba Hapa Kuna Mawili Ama Kuchelewa Sana Kufika Safari Yenu Ama Kumaliza Halaka Kisha Jamaa Analala Chapchap Na Hataki Tena Kuonesha Ushirikioano Hata Mamaa Akimbembeleza Vipi!

Hivyo Basi, Si Vema Kukutana Kimwili Na Mwenza Wako Kipindi Ukiwa Umechacha Kwani Wanaume Wengi Pindi Wanapokuwa Na Msongo Wa Mawazo Hukimbilia Kuomba Unyumba Kwa Wenzi Wao Wakiamini Kuwa, Wao Ndio Watawasaidia Kuwapunguzia Mawazo Badala Ya Kutafuta Njia Mbadara Ya Kumaliza Tatizo.



4. Kuishiwa Hamu Ya Nyama Na Mapishi Yale Yale Kila Siku


Uzoefu Wangu Unanionesha Kuwa Wanaume Wengi Hujikuta Wakikosa Hamu Ya Kurudia Tendo La Ndoa Mara Bada Ya Kumnaliza Mzunguko Wa Kwanza Kutokana Na Wake Zao Kutowaonesha Ubunifu Yaani Kila Siku Ni Kifo Cha Mende Tu Hakuna Jipya Linaloongezwa Hata Nakshi Za Miguno Ni Ile Ile Hali Inayosababisha Wanaume Wakose Hamy Ya Kuendelea Mara Baada Ya Kumaliza Mzunguko Wa Kwanza.

Wanaume Wengi Hujikuta Wanalazimika Kutafuta Kimada Ili Kupata Radha Mpya Na Huko Mambo Huwa Mulua Kwani Hufanikiwa Kwenda Raundi Hadi Tatu Na Bado Akawa Na Hamu Kwa Vile Tu Amekutana Na Vitu Adimu Hivyo Basi, Mwanaume Anapaswa Kumueleza Wazi Mkewe Kuwa Anahitaji Wakutane Faragha Ambapo Anataka Vutu Hadimu Vya Kabatini Na Si Kumsaliti Mwenza Wako Kwani Uwezo Wa Kumfanya Awe Bora Kunako Majambozi Unao Wewe Mnwenyewe Mwanamme.

Mfano Siku Akikwambia Anakwenda Kwenye Kitchen Party Mruhusu Kisha Akiwa Huko Mtumie Meseji Kuwa, “Mpenzi Najiandaa Kumalizia Sehemu Ya Pili Ya Soma Ulilojifunza Yaani La Vitendo, Hakika Leo Nitafaidi” Asikdanganye Mtu Hapo Hata Kama Bi. Harusi Mtarajiwa Hakufundishwa Mambo Fulani Ya Kumpagawisha Mumewe Atahakikisha Hakuangushi Atakuja Na Mambo Mapya Na Hapo Ndipo Mwanaume Hujikuta Akiganda Kifuani.

Nimalize Kwa Kusema Kuwa, Hakuna Haja Ya Kukurupuka Na Kukimbilia Kununua Dawa Za Kuongeza Nguvu Ya Kiume Bila Kutafakari Kwa Kina Chanzo Cha Tatizo Lako Kwani Yawezekana Tatizo Ulilonalo Linaweza Kutatulika Kwa Njia Nyingine Ambazo Hazitakufanya Uwe Hatarini.

Friday, February 8, 2013

Haya Sasa Maajabu Hata Nyama ya farasi inauzwa madukani Uingereza


 Nyama ya Farasi

Maafisa wa afya nchini Uingereza wameanza kugundua kiasi kikubwa cha nyama ya farasi inayouzwa kama nyama ya ngombe katika maduka makubwa.
Mikebe kadhaa ya nyama inayouzwa na kampuni ya vyakula ya FINDUS imethibitishwa kuwa na nyama ya farasi.
Shirika la Afya la kitaifa nchini humo limesema kuwa hakuna ushahidi iwapo chakula hicho ni hatari kwa afya ya mwanadamu lakini uchunguzi ungali unaendelea.
Shirika hilo linasema kuna hatari kuwa heunda kuna wahalifu wanaohusika katika kupakia nyama hiyo ya farasi kiharamu.
Mwezi uliopita nyama iliyodhaniwa kuwa ngombe ilibidi iondolewe kwenye maduka baada ya kuonekana kuwa ilikuwa imechanganyishwa na nyama ya farasi na nguruwe.

NAJUA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WENGI HATUZIJUI ZIP CODE ZA MIKOA YETU SASA ZIJUE HIZI HAPA


Arusha(6)                            102
Dar es Salaam(3)              73
Dodoma(5)                         145
Iringa(7)                               138
Kagera(6)                            153
Kaskazini Pemba(2)         31
Kaskazini Unguja(2)        50
Kigoma(4)                           85
Kilimanjaro(6)                    123
Kusini Pemba(2)               41
Kusini Unguja(2)               55
Lindi(6)                                 119
Manyara(6)                        86
Mara(5)                                120
Mbeya(8)                            174
Mjini Magharibi(2)           69
Morogoro(6)                      139
Mtwara(5)                          107
Mwanza(8)                         174
Pwani(6)                              81
Rukwa(4)                             79
Ruvuma(5)                          100
Shinyanga(8)                      160
Singida(4)                            88
Tabora(6)                            138
Tanga(7)                              158
2 788

Thursday, February 7, 2013

RECHO - Nashukuru Umerudi Official Video [ BongoUnlock ]

DENI LA TAIFA; KILA MTANZANIA ANADAIWA SH450, 000

Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza matokeo ya sensa, inayokaribia watu 45 milioni, siku chache baadaye deni la taifa lilitangazwa kufikia Sh21 trilioni huku katika wastani kila mtu akidaiwa Sh467,404.

Fedha hizo zinatokana na mkopo baada ya Serikali kukopa kwa ajili ya kujenga miundombinu kama barabara, bomba la gesi, mishahara ya wafanyakazi, na miradi mingine.
Kwa mujibu wa taasisi isiokuwa ya kiserikali ya Tanzania Coalition on Debt and Development (TCDD), serikali inadaiwa ‘mzigo wa madeni’ unaofika Sh21 trilioni.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Hebroni Mwakagenda, anafafanua kwamba Serikali inakopa fedha hizo Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).
Mwakagenda anasema deni limeongezeka kwa dola 456.1 milioni sawa na Sh7.3 trilioni katika kipindi cha mwaka mmoja tu, tangu Oktoba 2011.

Akichanganua kuhusu deni hilo Mwakagenda abainisha kuwa mpaka kufikia Oktoba mwaka jana, deni la nje lilikuwa Sh15.9 trilioni, kiwango ambacho ni cha juu kabisa kwa nchi kukopa kutoka kwenye masoko ya kimataifa. Amesema taarifa za BoT zinaonyesha kuwa deni la ndani limefikia Sh5.1 trilioni hadi kufikia Oktoba mwaka jana na kwamba kiasi hicho ni sawa na ongezeko la Sh513 bilioni tangu mwaka 2011.

“Deni la ndani linakua kwa kasi kubwa kwa sababu Serikali imeanza kukopa kwenye benki za biashara ambazo zinatoza riba kubwa. Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi,” anasema Mwakagenda.

Vizazi vijavyo kulipa deni
Dk Prosper Ngowi, kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro anasema deni siyo kitu kibaya ila tatizo likuja endapo fedha zilizokopwa zimetumika vibaya.

“Deni hili ni kubwa na hali ni mbaya kwa kuwa litalipwa na riba na haliwezi kumalizika leo litaendelea hadi kizazi kijacho,” amesema Dk Ngowi.
Kwa upande wake Profesa Humfrey Moshi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema ni lazima tujiulize deni hilo linatokana na miradi gani.

“Tuangalie fursa za kukopa na tupunguze matumizi yasiyokuwa ya lazima kama magari ya kifahari, safari zisizokuwa za lazima, kuwa na wajumbe wengi katika mambo madogo,” ameshauri Profesa Moshi.

Wakati wataalamu hao wakizungumza hivyo, takwimu za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira, alipowasilisha bungeni taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2011 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2012/13— zilionyesha kwamba pato la Taifa lilikuwa kwa Sh37.5 trilioni.

Hii inatokana na idadi ya watu Tanzania Bara, ambao wanakadiriwa kufikia 43.2 milioni mwaka 2010 na watu milioni 44.5 mwaka 2011, na pato la wastani la kila mtu lilikuwa Sh869,436.3 mwaka 2011. Mbali na hayo ukuaji halisi wa pato la Taifa ulikuwa kwa asilimia 6.4 mwaka 2011 ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2010.

Hivi sasa idadi ya watu inaongezeka kwa asilimia 2.6 kwa mwaka, kwa kipindi cha mika kumi iliyopita Watanzania milioni 10 waliongezeka.
Rais Jakaya Kikwete anasema idadi ya watu inakuwa kwa kiwango kikubwa na kwamba ongezeko lijalo litakuwa mzigo mkubwa kwa Taifa.

Kwa mujibu wa Rais kama ongezeko hilo litaendelea, ifikapo mwaka 2016, Tanzania itakuwa na watu 51 milioni kiwango kisichokidhi mahitaji halisi ya uchumi na mipango mengine.
Ongezeko hilo lisiloendana na kiwango cha uzalishaji linatia shaka zaidi huku msongomano wa watu katika miji mikubwa ukiendelea kuwa mkubwa, kwa mfano Dar es Salaam ina watu 2, 294 kwa kilometa moja ya mraba, ikifuatiwa na Mwanza watu 186 na Kilimanjaro 126.

Wasiwasi wa Rais unakuja huku Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akitoa ripoti mwezi machi mwaka jana kwamba kiwango cha ukosefu wa ajira nchini ni asilimia 11.7 kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea.

Wasira anasema vijana walioajiriwa wenye umri wa miaka 15 hadi 34 ni milioni 9.5 sawa na asilimia 86.6 na vijana wasio na ajira ni milioni1.4 sawa na asilimia 13.4 ya nguvukazi yote ya taifa.
Mbali na hayo Dk Ngowi anasema watu 1.6 milioni tu ndiyo wanaolipa kodi, na wengine wasiolipa huku idadi kubwa iliyobaki ikiacha mzigo huo kwa watu wachache.

Dk Ngowi anasema ili kujinasua na janga hilo, serikali inatakiwa kukusanya mapato ya kutosha ya ndani, lakini pia ijiepushe na matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Kuhusu elimu kutolewa bure, Dk Ngowi anasema mpango huo unatia shaka kwa kuwa Tanzania nchi maskini hivyo huduma za elimu bure, itakuwa na uwalakini.
Anabainisha kwamba ni bora elimu iwe ya kulipia, lakini iwe ya kiwango kinachotakiwa.

Serikali ikope kwa nidhamu
Naye Profesa Moshi alitahadharisha kuwa kama nchi itaendelea kuwa na madeni makubwa kiasi hicho, basi itashindwa kupiga hatua katika maendeleo yake ya kiuchumi kwa miaka ijayo.
“Nchi inapokuwa na deni kubwa kama hili, inaweza kuzuia wawekezaji wasije, kwa sababu watalazimishwa kulipa kodi kubwa ili kupunguza deni la nchi. “Tukope endapo kuna suala la muhini na ni lazima kufanya hivyo,” anasema Profesa

Kauli za wataalamu hao wa uchumi zinaoana na ile ya Mwakagenda ambaye pia anasema serikali inapaswa kufikiri mara mbili kabla ya kuamua kukopa, na kuwapo kwa nidhamu katika kukopa kwa kuwa deni hilo limevuka kiwango cha kimataifa.

Katika mapendekezo yake Mwakagenda anasema umefikia wakati kwa Serikali iruhusiwe kukopa baada ya ya Bunge kujadili kwa sababu mikopo mingi haina faida zaidi ya kuwaumiza wananchi.
Profesa Moshi anatahadharisha serikali isije kuomba kufutiwa madeni kama mwaka 2000 kupitia Mpango wa Nchi Maskini zenye Madeni Makubwa (HIPC).

Wakati deni hilo likiwa kubwa kiasi hicho, malengo ya uchumi na mendeleo ya jamii kwa Serikali katika mwaka 2012/13 ni pato la taifa kukua kutoka asilimia 6.8 na kufikia asilimia 8.5 mwaka 2016.

TAIFA STARS YAFANYA KILE WALICHO KITEGEMEA WATANZANIA, SAMATTA AUTHIBITISHIA UMA WA WATANZANIA KUWA YEYE NI MZALENDO

 

TAIFA Stars jana ilifanya kile kilichosubiriwa na mashabiki wa soka Tanzania baada ya kuitia ‘adabu’ Cameroon kwa kuichapa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, shukrani kwa bao la ‘jioni’ kutoka kwa mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samata.

Samata anayecheza soka la kulipwa TP Mazembe ya DRC, alifunga bao hilo muhimu kwenye Uwanja wa Taifa dakika ya 89 baada ya kuusukumiza wavuni kirahisi mpira wa krosi ya Frank Domayo uliompita kipa wa Cameroon, Offala Komguep.

Bao la Samata lilikuja baada ya Stars inayoshika nafasi ya 124 kwa ubora wa viwango vya soka kufanya mashambulizi yasiyo na idadi lango kwa Cameroon.
Dakika 20 za mwisho wa kipindi cha kwanza, Cameroon haikuwa mchezo na badala yake jezi za rangi ya bluu ndizo zilizokuwa zikimili mpira.

Ni ushindi wa kwanza kwa Stars dhidi ya Cameroon, kwani matokeo mazuri waliyowahi kupata ni sare moja ya bila kufungana kwenye uwanja huohuo, na kisha kukubali kipigo cha mabao 2-1 nchini Cameroon.
Stars wangeweza kupata bao la kuongoza kipindi cha kwanza kama siyo beki Erasto Nyoni kushindwa kufunga penalti iliyochezwa na kipa.
Mechi hiyo ilianza taratibu na dakika 10 za kwanza zilionekana kama za wachezaji wa pande zote kusomana kimchezo.

Wenyeji Stars walitumia mfumo wa kushambulia pamoja na kukaba kwa pamoja kama alivyosema Kocha Poulsen kabla ya mchezo huo.
Cameroon, mabingwa wa zamani wa Mataifa ya Afrika, hawakuonekana kuwa wakali kama ambavyo mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo walitarajia.

Stars ikitumia mfumo wa 4-3-3, ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini hata hivyo Cameroon ndiyo walitawala mchezo, huku wakitumia mfumo wa 4-3-4.
Dakika ya 19, mpira ulisimama kwa muda baada ya kipa wa Stars Juma Kaseja kuumia kufuatia kugongana na Tchami Herve wa Cameroon.

Mabeki wa Stars,Aggrey Morris na Kelvin Yondan walifanya kazi ya ziada kuwazuia washambuliaji wa Cameroon sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza.

Cameroon waliokuwa wakicheza bila nahodha Samuel Eto’o walikaribia kufunga bao katika dakika ya 24, baada ya Aboubakar Vincent kupiga kiki iliyotoka nje kidogo la lango la Stars. Nyoni angeweza kubadilisha ubao wa matokeo, kama siyo kushindwa kutumbukiza wavuni kiki ya penalti dakika ya 26 iliyotolewa na mwamuzi kutokana na Ngoula kuucheza mpira kwa mkono ndani ya eneo la hatari. Beki huyo wa Stars alikwenda kupiga penalti hiyo akionekana kutojiamini kabla ya shuti lake kupanguliwa na kipa Effala. Kipindi cha pili Stars ilicheza kwa nguvu na hapana shaka ndiyo walitawala sehemu kubwa, wakifanya mashambulizi mara kwa mara.

Ngasa aliyeisumbua zaidi ngome ya Cameroon alimjaribu kwa shuti la mwendo mrefu kipa Offala ambaye alifanya kazi nzuri ya kulizuia.
Kiungo chipukizi Abubakary naye alikaribia kufunga kwa Stars kama siyo shuti lake kuchezwa na kipa wa cameroon ambaye sehemu kubwa ya kipindi cha pili hakupumzika kuokoa hatari.
Pamoja na kufanya mabadiliko mengi kipindi cha pili, Stars waliendelea kutawala mchezo na kuwafunika Cameroon sehemu ya kiungo.

Katika mchezo huo, Stars ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Mwinyi na kuingia Thomas Ulimwengu ambaye aliongeza nguvu ya mashambulizi.

HAYA NDIO MAGAZETI YA LEO TAR 07/02/2013, PATA HABARI ZA MICHEZO, HARDNEWZ NA STORY ZA UDAKU KWA SAANA


.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

Tuesday, February 5, 2013

WANAWAKE 7 WATALII WABAKWA MEXICO


Wanaume waliokuwa wamejihami wamewabaka wanawake saba watalii karibu na hoteli moja ya kitalii nchini Mexico ijulikanayo kama Acapulco.
Polisi wanasema kuwa wanaume hao waliokuwa wamejifunika nyuso zao, walivamia makaazi ya wanwake hao kkusini mwa mji mapema aasubuhi.
Sita kati ya wanawake hao ni raia wa Uhispania, wa saba akiwa raia wa Mexico.
Hii ni moja ya visa vibaya zaidi vya uhalifu wa kijinsia kuwahi kuripotiwa na kufanyika dhidi ya watalii tangu hali ya usalama kuanza kudorora mwaka .2006.
Hoteli ya Acapulco ni salama lakini magenge ya walanguzi wa madawa ya kulevya huendesha biashara zao hapo sawa na makundi mengine madogo ya wahalifu.

MR LOVE LOVE HII INAKUUHUSU


Did you know that studies show that 88% of women say that they prefer "really good" oral sex over intercourse?
I've been married over 20 years and let me just be frank that the first few years with my wife was less than thrilling for her in the bedroom.
But I never really knew it at the time.  Women are good at hiding that sort of thing.  They want to make you feel like a stud so they will tell you it was great and will even fake the orgasm.
I'd go down on my wife (I knew about the study above) and she'd be all polite about it but it was pretty clear to me that I was not giving her the intense pleasure I was aiming for. Cunnilingus tips
So I sucked it up and did the smartest thing ever.... I sought help.  Yes, I know that is the last thing we men want to do.  We NEVER ask for directions do we ;)
Fortunately I have access to over 100,000 men and women who read my newsletters and I asked them to give very specific details and advice on what (in their personal experience) created the most enjoyable and pleasurable sexual experience FOR HER.
87% of the responses that came in had to do with going down on her.  Women said that nothing came even close to the pleasures they got from being "eaten out" (the right way). They also said their most powerful orgasms were as a result of a man going down on her.
I also received a lot of emails from women saying that if a man was not a master of the lick, then the experience was not all that enjoyable and sometimes was quite uncomfortable for her.  I could relate with that.  I thought I knew what I was doing but the reactions I was getting (or not getting) from my wife made me realize I needed to learn A LOT more. Cunnilingus tips
Several women made the comment in their emails that basically said "if she is not BEGGING you to go down on her then you aren't doing it right!".  Women with multiple partners said only about 20% of the guys they were with were any good at eating pussy. 
So I made it my mission to become an expert at cunnilingus.
In addition to compiling all the tips and suggestions from my readers I did a lot of technical and scientific research on the female anatomy, nerve endings, hormones and anything that can contribute to giving women the most outrageous of orgasms.
In my research I can across this study that said that less than 25% of women actually reach orgasm from vaginal sex. And 40% of women don't even enjoy vaginal sex AT ALL.
Scary or what?!
It was time for me to do my own "personal research".  During lovemaking I slipped my headCunnilingus tips down between my wife's legs and tried out some of the tips and technique my subscribers had shared. I soon heard an "Oh WOW" from my wife.   Clearly, she had never had this pleasure from me before.
After minutes of sighing and moaning and squirming with pleasure she broke out in a heavy sweat all over, arched her back and begged me to keep going.  She said she had 4 orgasms in a row. Two is her typical max.
Giving her that experience was satisfaction enough for me but she wanted to return the favor and she lunged onto my manhood (she doesn't usually like giving blow jobs) and gave me the most wonderful head. Score!
Now that I know how to lick her like a pro, 69 is one of her favorite positions. 
Don't be an idiot like me and go through years of giving mediocre head because you think you know more than you do. Sure, you can spending years "practicing" to try to learn how to give fantastic oral pleasure but it is much easier to learn from the shared tips and ideas of others.  I just wish that I had been more humble and sought advice earlier on. 
Look at these hard facts:
81% of women reach orgasm from receiving oral sex*
88% of married women prefer cunnilingus as their preferred sex act*
the clitoris has 8000 nerve endings ready for pleasure (twice the amount of the penis)*

Friday, February 1, 2013

MBOWE AMLIPUA PINDA SAKATA LA GESI MTWARA


Mboye 
SAKATA la gesi limetua rasmi bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe kuitaka Serikali iweke hadharani mikataba ya utengenezaji wa bomba la kusafirishia gesi hiyo kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam ili kuondoa usiri uliogubika mradi huo.
Mbowe alitoa wito huo jana alipokuwa akimuuliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda maswali bungeni katika kipindi cha Maswali na Majibu kwa Waziri Mkuu.
“Mheshimiwa Waziri ni dhahiri kuwa vurugu za Lindi na Mtwara zimesababishwa na mawasiliano hafifu kati ya Serikali na wananchi, ikiwamo kauli za viongozi wa Serikali na CCM je, ni kwa nini Serikali isiwachukulie hatua za uwajibikaji watumishi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama ambao wanaonekana dhahiri kuhusika,” alihoji Mbowe.

Kiongozi huyo wa upinzani alimtaka Waziri Mkuu kueleza ni kwa nini Serikali isiweke wazi mikataba yote ya gesi ili kuondoa hofu iliyojengeka kwa wananchi kwamba kumekuwa na hali ya ufisadi.

Akijibu swali hilo, Pinda aliwataka wabunge kutumia utaratibu mzuri wa kupata mikataba hiyo akisema haiwezekani ikawekwa hadharani.

Mbali na jibu hilo, Pinda alivitupia lawama vyama vya siasa akisema vimechangia kwa kiasi kikubwa mgogoro wa gesi mkoani Mtwara.
Licha ya juzi kueleza kuwa kulikuwa na mgogoro wa viongozi ndani ya mkoa huo pamoja na CCM, jana alikwepa swali la kutaka wahusika wawajibike na badala yake akasema suala hilo liko juu yake.

Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali lingine la Mbowe ambaye alimtaka Pinda kutoa kauli juu ya nani aliyesababisha mgogoro wa Mtwara uliosababisha maafa.

Hata hivyo, alitangaza neema kwa waathirika kwamba Serikali inaangalia namna ya kuwapunguzia gharama wale wote waliopatwa na matatizo hayo ikiwamo kuwalipa fidia.
“Vyama vya siasa vimechangia kwa kiasi kikubwa katika kupotosha jambo hilo, ushindani wa chaguzi zinazokuja umejitokeza pia,” alijibu Pinda.

Kiongozi huyo alisema wanaofanya uchochezi huo wanafanya bila ya kujua kwamba unaweza kuwakumba watu wote wakiwamo hao wanaofanya hivyo.
“Tutalaumiana wengi lakini ni vyema kuweka mambo hadharani na kwamba ni hatari kufanya mambo kama hayo kwani amani ya nchi ni lulu ambayo ikipotea inaweza kuwa tabu kuipata.”

Alipinga hoja ya Mbowe kuwa Serikali inatekeleza majukumu yake baada ya shinikizo na maandamano ya wanasiasa.
Alilieleza Bunge kuwa wananchi wa Mtwara wanaweza kupoteza fursa nyingi kutokana na wawekezaji kuanza kuondoka wakikwepa vurugu na kukimbilia Msumbiji ambako kuna dalili za gesi pia.

Kamati ya Makinda yayeyuka
Jana, Spika wa Bunge Anne Makinda aliliambia Bunge kuwa Kamati aliyotarajia kuiunda haitakuwapo kutokana na ukweli waliokuwa wakiutaka kutoka Mtwara kuelezwa na Waziri Mkuu.

Akiahirisha Bunge mchana wa Januari 29, mwaka huu, Makinda alitangaza kuwa angeunda kamati ya Bunge kwenda Mtwara kuangalia mgogoro huo.
“Kutokana na ukweli uliotolewa na Waziri Mkuu leo bungeni, naomba nimshukuru sana kwa dhati kwa kulishughulikia tatizo la Mtwara, lakini nieleze kuwa nilikusudia kuunda tume kwa ajili ya kwenda kutazama suala hilo, lakini tayari tumepata ukweli hivyo naona haina haja ya kuunda tume hiyo,” alitangaza Makinda.

Moto bungeni
Hoja binafsi ya Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia inayokosoa mfumo wa elimu Tanzania kwa shule za msingi na sekondari kuwa ni dhaifu na hauleti matumaini kwa wanafunzi, ilizua mjadala mzito bungeni jana baada ya Serikali kukataa pendekezo lake la kuunda kamati maalumu ya kutafuta chanzo cha tatizo hilo.

“Kutokana na hayo, ninaliomba Bunge lako tukufu kuunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza kina cha udhaifu huo wa kimfumo katika sekta ya elimu hapa nchini na kupendekeza hatua za kuchukua ili taifa liondokane na aibu ya udhaifu huo,” alisema Mbatia.

Baada ya hoja hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alipangua hoja moja baada ya nyingine na kuliomba Bunge lisikubali kuundwa kwa kamati teule, bali liiagize Serikali kushughulikia suala hilo.

Baada ya Dk Kawambwa kutoa hoja hiyo, Mbatia alisimama na kuikataa akisema kile alichokiainisha juu ya udhaifu hakifanani na kutaka kuundwa kamati kupitia kila hatua yenye udhaifu.

Baada ya Mbatia kusema hayo, ulizuka ubishi baada ya Spika Makinda kutaka kujadiliwa kwa mabadiliko ambayo Serikali inataka au hoja ya Mbatia iendelee.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alisema kuna kila sababu ya kuunda kamati lakini iwe teule ya Bunge.
“Tunatakiwa tujadili kwanza hoja iliyoko mezani na si kujadili mabadiliko ya hoja Mheshimiwa Spika, hoja aliyotoa Mbatia isibadilishwe kwa kuwa ni kinyume na kanuni za Bunge lako tukufu,” alisema Lissu.

Baadaye walisimama wabunge zaidi ya watatu wakitaka kuchangia lakini Spika Makinda alitoa nafasi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi ambaye alisema: “Tukiunda tume itachukua muda... Hoja iliyotolewa na Mbatia ni ya msingi, sasa kamati za Spika zishirikiane na Wizara ya Elimu kufanya kazi hiyo.”

Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje alisema haiwezekani Bunge likakubali Serikali ijichunguze yenyewe kwa kuwa ni kitu ambacho hakikubaliki na ni kinyume cha kanuni za Bunge.

Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM) alisema kuna matatizo katika sera, mitalaa na muhtasari na kusema sasa ni kazi ya Bunge kupata tume stahiki.
0
Share


LAIBONI; MIAKA 103, WAKE 40, WATOTO 113, WAJUKUU LUKUKI!



ASILIMIA 60 ya watu duniani huamini kuwa hadhi ya mtu kwenye jamii ni kuwa na fedha, magari au nyumba.
Hata hivyo , kwa Mzee Meshiko Mapi, Mmasai mwenye umri wa miaka 103, kwake maisha mazuri na yenye hadhi ni wake zake wengi, watoto, wajukuu na ng’ombe wengi wa kutosha.
Unapoingia katika eneo lake unamkuta mzee huyu akiwa  katika himaya yake ya kifahari, katika Kijiji cha Esilalee, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Himaya hiyo ipo katikati ya eneo la Miji midogo ya Makuyuni na Mto wa Mbu.                  
Magari yote ya abiria yanayopita  kijijini Esilalee kwenda maeneo mengine, yanakifahamu kituo  maarufu  cha kwa ‘Laiboni.’
Laiboni, ni jina  maarufu la Mzee Mapi na  yeye ndiye mmiliki wa kijiji hicho kwani wakazi wote wa kijiji hicho  ama ni watoto au wajuku zake.
Si hivyo tu, bali Shule ya Msingi Laiboni iliyopo katika kijiji hicho nayo ni ya kwake na  baadhi ya wanafunzi  wa shule hiyo ni watoto na hata wajukuu zake.  Kijiji hiki kimepambwa kwa mandhari yenye nyumba ndogondogo za msonge. Ni nyumba tatu tu kati ya hizo, ndizo zilizojengwa kwa matofali na kuezekwa kwa bati.
Nyumba ya  Laiboni, ambayo ni ya kisasa, ipo katikati ya kijiji, zizi la mifugo limejengwa mbali kidogo, kiasi cha hatua 100 kutoka zilipo nyumba nyingine.
Ingawa ni siku ya Jumapili, lakini kijiji hicho kimetawaliwa na ukimya mwingi. Shinini Mapiko Mapi, mtoto wa 82 wa Laiboni, ambaye ndiye mkalimani wangu anasema wanafamilia wengi wamekwenda katika shughuli zao, zikiwamo za kuchunga mifugo na nyinginezo. Karibu wakazi wote katika kijiji hiki hawafahamu Kiswahili, baadhi  wanayafahamu maneno machache na kuelewa lugha hiyo kwa kiasi kidogo.
Hata hivyo, Shinini peke yake ndiye anayeielewa  lugha ya Kiswahili ukilinganisha na wengine na yeye anakuwa msaada mkubwa kwangu, kama mfasiri.
Nzi, wadudu ambao hupenda mazingira yenye majimaji, maziwa au wanyama ndiyo wanaokukaribisha mahali pale, bila shaka wanasababishwa na wingi wa ng’ombe zaidi ya 2500  mali ya  Laiboni, ni kero kwa wageni na pengine hata kwa wakazi hao.
Unakutana na Laiboni, ameketi na watoto wake wa kiume 11, ambao ni sawa na timu ya mpira wa miguu.
Wengine wanacheza bao, baadhi wamejilaza huku wakiendelea kuwafukuza nzi waliokithiri.
Laiboni, mwenyewe ameketi kwenye kiti cha ngozi naye akifukuzana na nzi kwa kutumia usinga wa mkia wa ng’ombe.
Mwenyeji wangu, Shinini ananiambia nimsalimie kwa kumpa kichwa. Ninafanya hivyo naye anaweka mkono kichwani mwangu. Hizo ni salamu za Kimasai.
Laiboni anasema  alizaliwa mwaka 1910, katika Kijiji cha Olaleni, wilayani Ngorongoro.
Alikulia katika mazingira yaliyoheshimu mila na tamaduni. Alifundishwa kuthamini mifugo, alifundwa kuwa shupavu na jasiri kwa kuwa yeye ni mwanamume.
“Mwanamume usipokuwa jasiri, unadharaulika, unailetea familia yako aibu,” anasema akiendelea kuwafukuza inzi.
Laiboni anasema alioa mke wa kwanza akiwa na miaka 21, na anamkumbuka vyema mke huyo ambaye aliitwa Naitiame Ngishwa. Kwa bahati mbaya,  Naitiame hivi sasa ni marehemu.
“Hilo ndilo lilikuwa chaguo langu la kwanza… Naitiame Ngishwa,” anasema Laiboni.
Anasema kwa kuwa alibahatika kuwa na ng’ombe kiasi alioachiwa na baba yake mzazi mzee Mapi, hakuona sababu ya kuwa na mke mmoja- aliongeza wa pili.
“Fahari ya Maasai ni kuwa na wake wengi, kama una ng’ombe, unaoa mpaka ushindwe mwenyewe,” anasema mzee huyo ambaye pamoja na umri wake, meno yake mengi bado ni imara.
Shinini anasema mila za Maasai zinamtaka mwanamume mwenye wake wawili au zaidi kuwa na nyumba yake mwenyewe, kisha wake zake nao kuwa na nyumba zao.
“Unajua wanawake wanajenga ‘manyata’ zao wenyewe, na mzee wa boma anakuwa na nyumba yake,” anasema. Laiboni anasema   kadri siku zilivyokuwa zikikimbia Mungu alimbariki  na mifugo yake iliendelea kuongezeka. Kadri mifugo ilivyokuwa ikiongezeka ndivyo naye alipata ari ya kuoa zaidi. “Fahari yetu ni wake, mifugo na watoto, hakuna kitu kingine,” anasema.
Anasema aliendelea kuoa hadi sasa ana wake 40, ingawa baadhi wamefariki na wengine wamezeeka. Anajaribu kuwataja baadhi ya wake zake ambao ni pamoja na Naitiame, Nakaaye, Meeki, Ndemero, Supana, Mosipa, Naishooki, Meshi, Siyama na Mama Saunya.
Mke mdogo wa Laiboni ni  Meshi, ambaye kwa sasa ana miaka 42.
Laiboni anasema  kutokana na yeye kuwa na wake wengi, alibahatika kupata watoto wengi pia. Watoto wa Laiboni kwa  hivi sasa wanakadiriwa kuwa ni zaidi ya 103, hao ni baada ya wengine kufariki dunia.
“Kila mwanamke lazima azae watoto wengi, kila mwanamke ili aheshimike ni lazima awe na watoto saba na zaidi,” anasema.  Hata hivyo, anasema mke wake wa kwanza, Naitiame, hakuweza kuzaa watoto wengi, bali watatu tu.
Mtoto wa kwanza wa Laiboni, ambaye ni mwanamke, hivi sasa ana umri wa miaka 72 na anaishi   Wilaya ya Karatu.
Ratiba yake  Laiboni hula katika kila nyumba  ya mke mmoja kila siku. Asubuhi hunywa chai katika nyumba moja, mchana nyingine na jioni hula na kulala katika boma nyingine.
“Ninahakikisha nawatembelea wote, siwezi kusahau au kupitiwa,” anasema huku akicheka. Anasema kila mwanamke ana ng’ombe wake, ambao hutakiwa kuwachunga, hata hivyo dhamana ya kuuza ipo kwa watoto wake wa kiume . Shinini anasema:”Kila inapofika siku ya mnada, ng’ombe au mbuzi hupelekwa kuuzwa, hata hivyo bado idadi yao inazidi kuongezeka kwani wanazaliana,”
Rafiki wa Lowassa na Sokoine
Laiboni, pengine kutokana na utajiri wake wa mifugo, alipata kujuana na watu mashuhuri, akiwemo  aliyekuwa Waziri Mkuu katika uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, Edward Sokoine (marehemu). Si hivyo tu, bali  Laiboni anasema yeye ni rafiki wa karibu wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa. “Lowassa ni rafiki yangu mkubwa, aliwahi kunichukua tukaenda wote nchini Uganda kwa Rais Yoweri Museveni,” anasema
Shule ya Msingi Laiboni
Kwa kutumia utajiri wake wa ng’ombe, Laiboni alichukua uamuzi wa kujenga shule ya msingi kwa ajili ya watoto na wajukuu zake.
Kwa bahati nzuri, hakufanya kazi hiyo peke yake, bali alipata msaada toka kwa Shirika la Kusaidia Watu la Marekani,USAID. Laiboni kwa kuwa hakuwahi kusoma, hafahamu vyema kuhusu USAID, lakini anawashukuru kwa msaada wao, uliowezesha kizazi chake kupata elimu. “Niliuza ng’ombe, tukapata fedha za kuanzisha shule ingawa nilisaidia na USAID, nia ni kutaka watoto wangu wasome, hapa hakuna shule nyingine zaidi ya hii,” anasema
Shule ya Msingi Laiboni ina vyumba saba vya madarasa. Inao wanafunzi 130, kati ya hao 25 ni watoto wake 17, wajukuu na wanafunzi  wengine wanatoka vijiji vya jirani.
Shinini anasema  walimu wa shule hiyo wanalipwa na Laiboni mwenyewe kwa kusaidiwa na USAID.
“Walimu wengine wanatoka serikalini na wengine wanalipwa na mzee mwenyewe,” anasema kijana huyo. Laiboni anasema:  “namshukuru Mungu kwani kila kitu nilichotamani kukipata duniani nimekipata, haja zangu kuu zilikuwa ni ng’ombe, wake na watoto… na vyote nimepata.”
Picha hapana!
Lakini, Laiboni anakataa kupiga picha na wake zake akidai kuwa mila za Wamasai haziruhusu wanawake kuchangamana na wanaume.
Mzee huyo akaruhusu kupigwa picha na watoto wake saba, wakubwa wa kiume ambao anaeleza kuwa ndio wasaidizi wake.

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...