Friday, February 1, 2013

HII NI BALAA MAHAKAMA YAWAHUKUMU WATU 7 KIFUNGO CHA MIAKA 196

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi  Wilaya  ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, imewahukumu  watu saba kutumikia kifungo cha miaka  196  pamoja na  kazi nzito,mara baada ya kupatikana na hatia ya  kuharibu mali pamoja na kujeruhi na kusababisha kifo cha  mzee mwenye umri wa miaka 68.
Waliohukumiwa kutumikia kifungo cha miaka  28 kila mmoja  na adhabu  nzito  ni Oden  Msongela(40),Gilbeth Mwanandenje(43),Philibeth Abel(20),Meres Namazali(68), Edwin Masimba(30), Sabas  Alfred(18),Wenseslaus Kakwale(30) pamoja na Michael  Simfukwe(33) wote wakazi wa  kijiji cha Lusaka kilichopo  Tarafa ya Laela,Wilaya ya Sumbawanga.
Ilidaiwa  mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi ,Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Shani  mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo,Manase  Goroba  kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo  Mei 13  mwaka jana majira ya usiku  mara baada ya washtakiwa hao kuvamia  nyumba tatu  za wakazi wa Kijiji cha Lusaka, na kisha kuzibomoa   kwa kile walichowatuhumu  wenye nyumba hizo kuwa ni wachawi.
Mwendesha mashtaka huyo wa polisi aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa  katika tukio hilo washtakiwa hao kwa pamoja walimpiga na kisha kumuua Mzee mwenye umri wa miaka 68 aitwae Michael George, mkazi wa kijiji hicho  na kisha kumjeruhi  kwa kumkata na panga mguuni Vestina Mwananzumi (29).
Mara baada ya maelezo  ya ushahidi yaliyotolewa na upande wa mashtaka  yakiongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi ,Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Shani yaliiridhisha mahakama hiyo  jambo lililosababisha Hakimu Manase Goroba kutoa adhabu ya miaka saba kwa  kila mmoja na kwa kila kosa la washtakiwa hao walilofikishwa nalo mahakamani  hapa.
Hata Hivyo,hakimu huyo pia aliifafanulia mahakama hiyo kuwa adhabu hiyo ya miaka saba kwa kila kosa waliloshtakiwa nalo,hivyo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka saba tu kwa vile adhabu hizo zinaambatana .
Hakimu Goroba  alisema kuwa pia washtakiwa hao wataendelea  kukabiliwa na kesi nyingine ya mauji ya  Mzee Michael George  ambayo bado upelelezi wake unaendelea.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...