Monday, February 11, 2013

ZIJUE NJIA ZA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


Wanaume Wengi Hapa Duniani Huamini Kuwa, Mwanaume Hasa Ni Yule Anayeweza Kufanya Tendo Hilo Kwa Muda Mrefu Na Mara Nyingi Ndio Maana Vijana Wengi Utawasikia Wakijisifu Kuwa, Mpenzi Wake Hakulala Usiku Mzima Kutokana Na Dozi Ya Maana Aliyompa Na Ukimuuliza Mtu Wa Namna Hii Atakwambia Kuwa Alikwenda Mizunguko Sita Usiku Mzima.

Hata Hivyo, Ukweli Ni Kuwa, Watu Wengi Hufikia Hatua Ya Kusema Uongo Ili Waonekana Kuwa Ni Wanaume Hasa Mbele Ya Wenzao Huku Wengine Wakigubikwa Na Nadharia Kuwa Ukubwa Wa Uume Unaashiria Jinsi Gani Walivyo Wanaume Kitu Ambacho Si Kweli.

Ni Mtazamo Huu Ndio Unaowafanya Wanaume Wakitaniwa Au Kuambiwa Kuwa Wako Kama Wanawake Wanaweza Waue Mtu. Tunaamini Kuwa Uanamke Ni Udhaifu Na Uanaume Ni Ushujaa Fulani Hivi.
Wakati Hali Ikiwa Hivyo, Hivi Sasa Wanaume Wengi Wamekuwa Wakihangaika Na Jambo Moja Kubwa, Kutafuta Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume Ili Kujiongezea Heshima Faragha!
Ukitaka Kuthibitisha Hili Jaribu Kuangalia Karibu Katika Kila Gazeti Utakalo Soma, Ni Nadra Sana Kukosa Tangazo Dogo La Biashara Lililotolewa Na Mganga Wa Kienyeji Anayejigamba Kuwa Anazo Dawa Za Kuongeza Nguvu Za Kiume, Na Matangazo Hayo Hayaishii Magazetini Tu, Bali Hata Redioni Pia Yapo.

Mbaya Zaidi Dawa Zinazoongelewa Hupewa Majina Mengi Ya `Kusisimua` Kama Kombora, Simba Na Nyati Siushasikia Mziki Wa Nyati Akikasirika Sasa Jenga Picha Nuvu Ya Hiyo Dawa, Hata Hivyo, Dawa Nyingi Ni Uzushi Tu Na Hupewa Majina Hayo Ili Kuwavuta Wateja Na Kuwashawishi Kuzijaribu, Enewei Ndivyo Biashara Zilivyo.

Wingi Huu Wa Matangazo Umeanza Kuonekana Katika Miaka Ya Hivi Karibuni, Na Kadiri Siku Zinavyozidi Ndivyo Idadi Ya Waganga Wanaojigamba Kuwa Na Dawa Hizo Inavyozidi Kushamiri, Kuna Waganga Wenye Dawa Za Kiswahili, Kiarabu Na Za Kichina Ndio Usiseme!
Binafsi Utitili Wa Matangazo Haya Umenifanya Niamini Kuwa, Kuna Tatizo Kubwa La Wanaume Kupungukiwa Nguvu Hizo, Na Ingawa Hakuna Utafiti Wa Kitaalamu Uliofanywa Rasmi, Lakini Inaonyesha Kuwa Tatizo Hilo Kwa Sasa Ni Kubwa Sana Na Si Tanzania Tu, Bali Ni Dunia Nzima.

Kutokana Na Hali Hiyo Ndipo Waganga Wa Kienyeji Pamoja Na Makampuni Mengi Makubwa Duniani Hujaribu Kuelekeza Nguvu Zao Katika Kufanya Utafiti Wa Kutengeneza Dawa Za Kusaidia Watu Wenye Tatizo Hilo, Na Bahati Nzuri Kwa Makampuni Na Waganga Hao Ni Kwamba Inaonekana Kama Biashara Inawaendea Vizuri.

SABABU ZA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME:

1. Kuna Wakati Pia Upendo Unapopungua Na Mvuto Unapungua Baina Ya Wanandoa, Mwanaume Anaweza Kujikuta Kila Akiwa Faragha Anashindwa Kuendesha Gari Kwa Muda Mrefu Na Anaweza Kudhani Kuwa Ana Matatizo Kumbe Hali Hiyo Inamkumbwa Kutokana Na Kutokuvutiwa Na Mwenzi Wake.

Tatizo Kama Hili Linaweza Kutatuliwa Kwa Kumueleza Wazi Mkeo Ama Mpenzi Wako Jinsi Gani Anaweza Kujipanga Na Kuonekana Na Mvuto Wa Hatari Utakaokufanya Uchanganyikiwe Kila Umuonapo Na Hata Mkiingia Kwenye Mambo Fulani Basi Kwa Hakika Utahamasika Na Kutoa Dozi Ya Maana.


2.Uchovu Wa Kazi Za Ajira

Mkufunzi Wangu Wa Saikolojia Katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Iringa Ambaye Ameshatangulia Mbele Za Haki, Pro. Samuel Mshana (Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi) Aliwahi Niambia Kuwa Wanawake Wanataka Security Kutoka Kwa Mwanaume Nami Nikamtania Pro. Sasa Mbona Mimi Na Mwili Mdogo Nitampa Ulinzi Gani Mwanamke Akacheka Kisha Akaniambia Ulinzi Naouzungumzia Ni Wa Jumla Ikiwa Ni Pamoja Na Kuhakikisha Mambo Yanakwenda Sana Ndani Ya Nyumba Yani Watoto Wanakwenda Shule Na Mambo Ya Mlo Wa Uhakika.

Hivyo Ni Wazi Kuwa Wanaume Huhangaika Kwa Kiasi Kikubwa Kuhakikisha Wanamudu Majukumu Yao Ya Kila Siku Na Huko Makazini Kuna Mauzauza Mengi Na Usiombe Ufanye Kazi Kwenye Kampuni Binafsi Kila Kukicha Wewe Upo Roho Juu Sasa Katika Hali Kama Hiyo Ukikutana Na Mwenzi Wako Kunako Majambozi Utahisi Una Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Kwani Mara Tu Baada Ya Kumaliza Mshindo Wa Kwanza Hutoweza Kurudia Tena! Hali Ni Hivyo Hivyo Kwa Watu Wanaofanya Kazi Nzito Zinazosababisha Wajikute Wanarudi Majumbani Wakiwa Wamechoka.

Hivyo Basi, Endapo Nawe Ni Miongoni Mwa Watu Wanaokumbana Na Tatizo La Kushindwa Kurudia Majambozi Kwa Sababu Ya Uchovu Na Msongo Wa Mawazo Kutoka Kazini Hakikisha Unapanga Muda Muafaka Na Mwenzi Wako Kupeana Raha.

Mfano Kama Jumamosi Unafanya Kazi Nusu Siku Ukitoka Usiende Kulewa Kama Ni Mtu Wa Kinywaji Bali Nenda Kapumzike Kisha Kesho Yake Waweza Kumtoa Out Mama Na Kwenda Mazingira Tofauti Kupeana Kitu Roho Inapenda Hakika Utajishangaa Jinsi Utakavyomudu Majambozi.


3. Kuchacha


’ Ebwana Usije Ukawa Katika Hali Mbaya Kifedha Na Kila Jambo Unalolipanga Linakwenda Ndivyo Sivyo Hali Inayokusababishia Uchache Kisha Mwenzi Wako Akakuomba Unyumba Hapa Kuna Mawili Ama Kuchelewa Sana Kufika Safari Yenu Ama Kumaliza Halaka Kisha Jamaa Analala Chapchap Na Hataki Tena Kuonesha Ushirikioano Hata Mamaa Akimbembeleza Vipi!

Hivyo Basi, Si Vema Kukutana Kimwili Na Mwenza Wako Kipindi Ukiwa Umechacha Kwani Wanaume Wengi Pindi Wanapokuwa Na Msongo Wa Mawazo Hukimbilia Kuomba Unyumba Kwa Wenzi Wao Wakiamini Kuwa, Wao Ndio Watawasaidia Kuwapunguzia Mawazo Badala Ya Kutafuta Njia Mbadara Ya Kumaliza Tatizo.4. Kuishiwa Hamu Ya Nyama Na Mapishi Yale Yale Kila Siku


Uzoefu Wangu Unanionesha Kuwa Wanaume Wengi Hujikuta Wakikosa Hamu Ya Kurudia Tendo La Ndoa Mara Bada Ya Kumnaliza Mzunguko Wa Kwanza Kutokana Na Wake Zao Kutowaonesha Ubunifu Yaani Kila Siku Ni Kifo Cha Mende Tu Hakuna Jipya Linaloongezwa Hata Nakshi Za Miguno Ni Ile Ile Hali Inayosababisha Wanaume Wakose Hamy Ya Kuendelea Mara Baada Ya Kumaliza Mzunguko Wa Kwanza.

Wanaume Wengi Hujikuta Wanalazimika Kutafuta Kimada Ili Kupata Radha Mpya Na Huko Mambo Huwa Mulua Kwani Hufanikiwa Kwenda Raundi Hadi Tatu Na Bado Akawa Na Hamu Kwa Vile Tu Amekutana Na Vitu Adimu Hivyo Basi, Mwanaume Anapaswa Kumueleza Wazi Mkewe Kuwa Anahitaji Wakutane Faragha Ambapo Anataka Vutu Hadimu Vya Kabatini Na Si Kumsaliti Mwenza Wako Kwani Uwezo Wa Kumfanya Awe Bora Kunako Majambozi Unao Wewe Mnwenyewe Mwanamme.

Mfano Siku Akikwambia Anakwenda Kwenye Kitchen Party Mruhusu Kisha Akiwa Huko Mtumie Meseji Kuwa, “Mpenzi Najiandaa Kumalizia Sehemu Ya Pili Ya Soma Ulilojifunza Yaani La Vitendo, Hakika Leo Nitafaidi” Asikdanganye Mtu Hapo Hata Kama Bi. Harusi Mtarajiwa Hakufundishwa Mambo Fulani Ya Kumpagawisha Mumewe Atahakikisha Hakuangushi Atakuja Na Mambo Mapya Na Hapo Ndipo Mwanaume Hujikuta Akiganda Kifuani.

Nimalize Kwa Kusema Kuwa, Hakuna Haja Ya Kukurupuka Na Kukimbilia Kununua Dawa Za Kuongeza Nguvu Ya Kiume Bila Kutafakari Kwa Kina Chanzo Cha Tatizo Lako Kwani Yawezekana Tatizo Ulilonalo Linaweza Kutatulika Kwa Njia Nyingine Ambazo Hazitakufanya Uwe Hatarini.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...