Sunday, April 28, 2013

ANGALIA PICHA ZA MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKIZINDUA TAASISI YA 'CONFUCIUS' YA CHUO KIKUU CHA DODOMA LEO, PIA AKAGUA UJENZI WA CHUO CHA AFYA UDOM



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezana na Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof. Idris Kikula, wakati akitembele kukagua majengo ya Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina, baada ya uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha 
Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu Lugha na Tamaduni za Kichina, kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya 'Confucius', Zheng Xueyu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia michoro ya picha zinazochorwa na wanafunzi wa Taasisi ya Confucius inayotoa elimu ya Lugha na Tamaduni za Kichina, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua ujenzi wa Chuo cha Afya cha UDOM.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma


 Picha ya pamoja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kuhitimu mafunzo ya Lugha ya Kichina, mmoja kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Jamillah Dauda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 28, 2013 Chuo Kikuu cha Dodoma. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof. Idrs Kikula.

Friday, April 26, 2013

BAADA YA KUZUSHIWA KAISHIA FORM TWO, HII NDO CV YA MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA JISOMEE HAPA MWENYEWE UPATE UKWELI

Member of Parliament CV

GENERAL
Salutation
Honourable
Member picture
First Name:
Godbless
Middle Name:
Jonathan
Last Name:
Lema
Member Type:
Constituency Member
Constituent:
Arusha Mjini
Political Party:
CHADEMA
Office Location:
Office Phone:
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Current Member
Date of Birth
26 October 1976
EDUCATION
School Name/Location
Course/Degree/Award
Start Date
End Date
Level
Cambridge International College
Degree
2010
Todate
NOT COMPLETED
Cambridge International College
Diploma
2008
2010
DIPLOMA
Kolila Secondary School
A-Level Education
1991
1993
SECONDARY
Geita Secondary School
O-Level Education
1989
1991
SECONDARY
Kalangala Primary School
Primary Education
1983
1989
PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name
Position
From
To
The Parliament of Tanzania
Member - Arusha Urban Constituency
2010
2015
PTN
Chief Executive Officer (CEO)
2007
2008
Tanzania Labour Party, TLP
District Secretary General
2005
2008
DENETRIA
Director
2005
2008
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location
Position
From
To
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
Member of Parliament
2010
Todate
Tanzania Labour Party, TLP
District Secretary General
2005
2008
Tanzania Labour Party, TLP
Candidate, Member of Parliament
2005
PUBLICATIONS
Description
Date
Lema Godbless: Msaada wa haraka kutoka katika Biblia, Arusha
2008
Godbless Lema: Wisdom Time, Arusha
2008
Lema Godbless: Msaada wa haraka kutoka katika Biblia, Arusha
2008
Godbless Lema: Wisdom Time, Arusha
2008
Lema Godbless: Msaada wa haraka kutoka katika Biblia, Arusha
2008
Godbless Lema: Wisdom Time, Arusha
2008
Lema Godbless: Msaada wa haraka kutoka katika Biblia, Arusha
2008
Godbless Lema: Wisdom Time, Arusha
2008

KUMBE ROLNADIHNO BADOO YUMOO CHEKI HILI BONGE LA GOAL


NEYMAR another amazing goal (Santos 3x1 Internacional) LIBERTADORES DA A...

HUYU NDIYO NEYMAR WA YOUTUBE VIP ULIPOMWONA ANASADIFU HIZI VIDEO?

[NEYMAR'S AMAZING GOAL] Neymar Jr - Winner The FIFA Puskas Award 2011 Be...


ANGALIA PICHA MBALI MBALI ZIKIONESHA JINSI MAZISHI YA MWANAFUNZI ALIYEUWAWA HUKO ARUSHA


HAPA NDIPO ILIPOISHIA SAFARI YA MAREHEMU HENRY KOGA
 MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI 



HATIMAYE YANGA YATAWAZWA KUWA MABINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE 2012/12

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati klabu ya YANGA leo imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania katika msimu wa 2012/13. 

Yanga imefanikiwa kutangaza ubingwa huo huku ikiwa imebakiwa na michezo na michezo miwili baada ya Azam FC ambao wanashika nafasi ya pili kutoka sare ya 1-1 na Coastal Union leo hii katika dimba la uwanja wa Mkwakwani.
  
Matokeo hayo yanamaanisha, Azam FC ambao walikuwa wakiikimbiza Yanga kwa karibu katika mbio za ubingwa, hawawezi kuzifikia pointi za Yanga yenye pointi 56, huku Azam ambao wamebakiwa na michezo miwili vilevile wakiwa na pointi 48 - hivyo hata wakishinda mechi zao zilizobakia watakuwa na pointi na poinri 54.

MSIMAMO WA LIGI ULIVYO HIVI SASA

                                    P W D L GF GA GD Pts
1 Yanga SC        24 17 5 2 44 13 31 56
2 Azam FC          24 14 5 5 42 20 22 48
3 Kagera Sugar   23 11 7 5 25 18 7 40
4 Simba SC         22 9 9 4 32 21 11 36
5 Mtibwa Sugar   24 9 9 6 27 23 4 36
6 Coastal Union   24 8 10 6 24 21 3 34
7 Ruvu Shooting  22 8 6 8 21 21 0 30
8 JKT Oljoro 24 7 7 10 22 27 -5 28
9 Prisons            24 6 8 10 14 21 -7 26
10 JKT Ruvu 24 7 5 12 20 37 -17 26
11 Mgambo JKT   23 7 4 12 16 23 -7 25
12 Toto African     25 4 10 11 22 34 -12 22
13 Polisi Moro      23 3 10 10 12 22 -10 19
14 African Lyon 24 5 4 15 16 36 -20 19

Wednesday, April 24, 2013

The only moment Barcelona might want to remember from their 4-0 loss to Bayern Munich


(Getty)
Bayern Munich absolutely dismantled Barcelona in the first leg of their Champions League semifinal, winning 4-0 at the Allianz Arena. Though Barca maintained their trademark possession advantage, Lionel Messi, who is still recovering from a hamstring injury, was rendered mostly irrelevant as Barca only managed four shots with just one on target during the game.
Another round of misleading obituaries for Barcelona is likely to follow this display, but the true takeaway from the match should be what Germany already knows: Bayern, who have been confirmed as this season's domestic champions for weeks now, have reached that transcendent level. To varying degrees of justifiability, Barca can blame the waterlogged center of the pitch, their injury plagued backline and a hobbled Messi daring to go a whole match without scoring eight goals. But if they could, they would still like to erase the entire match from their memory.
The one moment when Barcelona did stick it to Bayern, it was in a very childish way and resulted in Jordi Alba getting the yellow card that will keep him out of the second leg for accumulation. With Barca down 4-0 in the 89th minute, Bayern winger Arjen Robben, who put in a fine performance and scored his team's third goal, was knocked down in an off the ball incident. As he did his signature fetal-position roll, a frustrated Jordi Alba kicked the ball into his back before the ref could blow the whistle. Alba then fetched the errant ball and tossed it off Robben's face to earn a booking (video below).


The fragile Robben clutched his nose and the slog to the final whistle, then an excruciating week until the formality of a second leg back in Barcelona continued.
Come the start of next season, Barcelona will still be La Liga champions, reloaded with healthy players and world-class new additions. Until then, their shows of strength are a bunch of fruitless possession and making Robben's nose sting a bit.

TANZANIA INA HALI MBAYA KUELEKEA 2015


Wakati Tanzania ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wasiwasi umeanza kuzuka kwamba taifa hilo lililosifikana kuwa kisiwa cha amani katikati ya mataifa mengine yenye machafuko, nalo linaelekea kwahala kubaya.
Watu, jamii na mataifa katika pembe zote za dunia daima hubadili mielekeo, tabia na matarajio yao kulingana na mabadiliko ya nyakati. Watanzania hawako tofauti na hilo.
Nchi hii ya Afrika ya Mashariki, kwa miongo mitano ya utaifa wake, imepita katika mabadiliko ya kitamaduni, kisiasa na kiuchumi, mbali ya yale yanayozungumzwa sana katika tasnia ya hali ya hewa kama mabadiliko ya tabia nchi.
Kila mabadiliko kwa njia moja au nyingine hugusa tabia za watu, mara nyingine huleta wasiwasi kuhusu mambo yawezayo kutokea hapo baadaye.
“Tunajifunza kutokana na uzoefu na kama tumesalimika miaka yote hii, kwa nini tuwe na wasiwasi kuhusu yajayo kesho?” alisema Mtanzania mmoja akieleza kuwa uzoefu ndio mwalimu mkuu wa maisha.
Hali inatia wasiwasi
Miongoni mwa vijana wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania.Miongoni mwa vijana wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania.
Lakini wengine wenye wasiwasi hupata ujumbe tofauti kutokana na matukio ya karibuni na kutahadharisha kuwa jamii ya Tanzania huenda inaelekea katika kipindi cha balaa kama siyo mwanzo wa kuteketea kabisa.
Maendeleo katika sayansi ya tiba yamewezesha dunia kugundua na kutibu au kuzuia maradhi yasienee. Lakini katika uelewa wangu mdogo bado sijaamini kuwa ipo dawa ya kuondoa kabisa matatizo yatokanayo na mienendo isiyofaa ya binadamu.
Mienendo hiyo imekuwa chanzo cha uhalifu usiolezeka nchini Tanzania kama vile kuwachuna ngozi binadamu, kukata viungo na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, na hivi karibuni tu limezuka wimbi la uharamia wa utekaji na mashambulizi ya kinyama dhidi ya watu.
Mashambulizi dhidi ya Daktari Steven Ulimboka na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, jijini Dar es Salaam yamezua maswali mengi ambayo bado hayajapatiwa majibu ya kuridhisha kuhusu usalama wa raia mmoja mmoja.
Uchunguzi uliofanywa na walinzi wa sheria kuhusu mazingira ya matukio hayo haukuonyesha madhumuni wala utambuzi wa watu waliofanya makosa hayo ya kiharamia.
Mitaani, katika vilabu au mahali popote watu wanapokutana na kufanya maongezi matukio hayo yanazungumzwa lakini kwa unyonge kwa sababu baadhi ya watu wanahofu kwamba mjadala wake unaweza kuwaletea matatizo ya kisiasa. Lakini kuna kosa gani kama watu watazungumzia matukio kwa utulivu bila hisia zozote za kisiasa?
Kwani hakuna umuhimu wa kuchunguza mandhari ya Tanzania kisiasa na mazingira ambamo matukio kama hayo ya kusikitisha yalitokea?
Kuibuka kwa siasa uchwara
Watoto wakitoka kuchota maji kwenye kijiji cha Kemogemba, nchini Tanzania.Watoto wakitoka kuchota maji kwenye kijiji cha Kemogemba, nchini Tanzania.
Mbali ya hayo kuna minong'ono kwamba nchi imepoteza muelekeo na siasa uchwara zinazidi kuenea ambapo viongozi wa kuchaguliwa wameshindwa kwenda na malengo ambayo yangekuwa ya manufaa kwa wananchi na vizazi vijavyo.
Hapa kila mtu anaelewa kitu angalau kidogo kuhusu Malengo ya Mandeleo ya Milenia ya 2015, lakini mwaka huo unavyokaribia kila mafanikio yaliyopatikana katika nchi hii yanafunikwa na kitambaa cha kisiasa ili kukifagilia chama tawala kipate ushindi.
‘Mafanikio' hayo yanahusishwa na hata miradi iliyokamilishwa kwa fedha za wafadhili ikiwa pamoja na ile ya Millennium Challenge ambayo serikali ya Marekani ilitolea dola zipatazo milioni700 miaka mitano iliyopita ili kupunguza umaskini kupitia sekta za uchukuzi, maji na nishati.
Tamaa za kisiasa huwapotosha wale wanaotaka kuwania uchaguzi kuamini kwamba watu wote wameungana kutokana na chama wanachofuata au wanachosingizia kukiunga mkono.
Lakini umoja wa Watanzania unaonekana zaidi kuwa upo katika kusudio lao moja la kusimamisha kuporomoka kwa uchumi kuliko kitu kingine chochote.
Kukawia kwa uchumi kuchanua kumeungana na kushuka kwa elimu ambapo watahiniwa wanafeli kwa wingi, huduma za afya hazitoshelezi mahitaji na raia hawapati vitu muhimu kuwawezesha wawe na uhakika wa maisha bora.
Kitu muhimu kinachokosekana, kama mchambuzi wa hali hii alivyoeleza, ni utaratibu wa kuishinikiza serikali iliyopo kutekeleza sera zenye muelekeo wa maendeleo ya uchumi.
Uchaguzi pekee si kigezo cha mabadiliko
Harakati za uchaguzi wa mwaka 2010 nchini Tanzania.Harakati za uchaguzi wa mwaka 2010 nchini Tanzania.
Chaguzi peke yake hazitabadilisha hali kama rushwa inazidi kuwa muhimu katika kuamua nani apate ushindi. Uzoefu wa chaguzi zilizopita umewafanya wapiga kura wasijali tena nani ashinde hapa au kule.
Mbali ya lawama zinazoelekezwa kwa chama tawala kwa kushindwa kwake kuwa wazi kwa mawaidha tofauti, vyama vya upinzani pia vina matatizo ambayo yanaonekana dhahiri kutokana na kushindwa kujipanga na udhaifu wa kupambana na changamoto za kilojistiki katika ushindani na chama tawala ambacho kina mizizi katika vyombo vyote vya dola.
Tanzania ina uhaba wa viongozi bora wenye upeo, dhamira na msukumo. Wengi wameshika nafasi kutumikia malengo yao binafsi kwani wameshindwa kutimiza ahadi walizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.
Ikiwa uchaguzi ujao hautatoa viongozi ambao hawawezi kuuza mioyo ya kwa ajili ya kipande cha mkate au kujiachia waendeshwe na uroho wa mali, wananchi watakuwa wamejiweka pabaya kuumia kutokana na madhara zaidi.
Ukosefu wa ajira ni suala muhimu na la muda mrefu tangu chaguzi kuu mbili zilizopita na hali itakuwa iko vile vile mwaka 2015 kwa sababu makundi makubwa ya vijana wa kike na kiume yanaingia katika kundi la watu wasio na ajira kila mwaka.
Hata hivyo, kwa kutambua changamoto hiyo, serikali inasemekana kuwa inaandaa mpango wa mabilioni ya shilingi kutoa mikopo kupitia benki ya CRDB kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu ambao hawana ajira, kama watakuwa na mapendekezo ya miradi ya kuwekeza.
Je, mpango huu hautakuwa mfereji mwengine wa kupoteza fedha za serikali na kuwa mzigo wa ziada kwa walipakodi? Kama haukufaulu nchi itakuwa imetoswa katika hali ngumu.
Mwandishi: Anaclet Rwegayura/ DW Dar es Salaam
Mhariri: Iddi Ssessanga

MAN UNITED ILIVYOTWAA NA KUSHANGILIA UBINGWA WA ENGLAND 2012/2013


 Saluti Jembe Letu: Wachezaji wa Manchester United wakimpongeza mshambuliaji wao Robin van Persie (kushoto) baada ya kufunga moja ya mabao yake matatu, yaliyoipa United ushindi wa 3-0 dhidi ya Aston Villa na kutawazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England, taji lililokuwa likishikiliwa na mahasimu wao Man City.
 Kiduku cha Ushindi na Utamu Wake: Mholanzi, Robin van Persie (katikati), akishangilia kwa staili ya kucheza muziki baada ya kuiwezesha timu yake kushinda dhidi ya Aston Villa na kutwaa jtaji la 20 katika historia ya Man United, ambalo ni la 13 chini ya Mskochi Sir Alex Ferguson.
 Ubingwa wa Uzeeni Mtamu Bana: Beki mkonngwe Rio Ferdinand (kulia), akiongoza ushangiliaji na wachezaji wenzake wakiwa wamejifunika bendera ya Man United
 Duuh, Hawa Watoto Noma Aisee: Alex Ferguson (wa pili kulia) akishangilia na jopo lake la Maofisa wa Benchi la Ufundi na wachezaji wa akiba, mara baada ya filimbi ya mwisho ya mechi dhidi ya Aston Villa.
 Furaha ya Nahodha Mfaransa: Beki wa kimataifa wa Ufaransa anayeiongoza Man United kwa sasa, Patrice Evra, akishangilia huku akiwa amejifunga bendera ya timu yake kichani.
 Pozi la Picha na Shujaa wa Msimu: Ferdinand, akiwa na nyota wengine wakipozi kwa picha na Robin van Persie aliyeibuka shujaa wa msimu wa klabu hiyo, ambapo jana alifunga mabao yote matatu 'hat-trick.'
 Utu Uzima Dawa: Yoso Mbrazil wa Man United, Rafel da Silva (kushoto) akipiga picha na beki mkongwe wa klabu hiyo, Rio Ferdinand.
 Bao la Kwanza Nalifunga kama Ifuatavyo: Van Persie (kushoto) akipiga shuti kufunga bao la kwanza katika mechi hiyo iliyowapa ubingwa wa Ligi Kuu.
 Fundi Kazini: Van Persie akipokea na kupiga kufunga bao la pili la Man United dhidi ya Aston Villa.
 Huwezi Kuzuia Mvua Weweee!! Van Persie hapa anaonekana akimaliza kazi kwa kufunga bao la tatu la United.
 Sisi Ndio Sisi, Wengine Mafisi: Wachezaji wa Man United wakishangilia ubingwa wa Ligi Kuu.
 Jezi ya Mtaalam Wenu Hii Hapa: Van Persie akionesha jezi yake, ambayo pia inawakilisha idadi ya vikombe vya Ligi Kuu vilivyobebwa na Man United.
 Shampeni ya Ushindi Hiyoooo!! Rio Ferdinand akitingisha na kuwamwagia wenzake shampeni ya kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu.
 Nina Furaha Kuliko Nyie Wote: Ferdinand akiruka juu kwa furaha wakati wa zoezi la kufungua shampeni ya kushangilia ubingwa.
 Hii Yangu Pekee: Ferguson akifungua shampeni yake ya kusherehekea ubingwa na kisha kuanza kuinywa kama anavyoonekana katika picha ya chini.

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...