Tuesday, April 9, 2013

BAADA YA KUSUASUA NA KUSHINDA KESI YA UCHAGUZI SASA UHURU KENYATTA RAIS MPYA WA KENYA


Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapishwa hii leo na kuchukua uongozi kutoka kwa Rais anayeondoka mamlakani Mwai Kibaki.
Hii ni baada ya Uhuru kumshinda Raila Odinga katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe nne mwezi Machi .
Wageni mashuhuri wakiweno marais wa nchi kadhaa za Afrika akiwemo rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete pamoja na wanadiplomasia na maelfu ya wananchi walishuhudia sherehe hizo katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi.
Odinga hakuhudhuria sherehe hizo baada ya jitihada zake kutaka mahakama ya juu zaidi kubatilisha matokeo ya uchaguzi kukosa kufua dafu.
Kenyatta na naibu wake William Ruto wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC . Wanadaiwa kuwa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika miaka mitano iliyopita.
Wakati huo wawili hao walikuwa mahasimu wa kisiasa na wote wanakanusha madai dhidi yao.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye mahakama ya ICC imetoa kibali cha kumkamata, kuhusiana na vita katika jimbo la Darfur, hakufika nchini Kenya kwa sherehe hizo licha ya kuwa alialikwa.
Kenyatta ni mwanawe rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta, na amerithi mali nyingi sana .
Aidha Kenyatta ndiye rais mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuongoza nchi. Ana umri wa miaka 51 na ni mwanawe rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...