Thursday, April 11, 2013

BREAKING NEWS: DIAMOND AVUNJA RASMI NDOA YA UWOYA



Na Mwandishi Wetu
JAMBO limezua jambo, lile sakata la kunaswa hotelini kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Irene Uwoya limezaa matunda hasi kwa ndoa ya mwadada huyo ambayo sasa imevunjika rasmi, Amani limetonywa. 

 
Habari ya wawili hao kunaswa na kubainika kulala katika chumba kimoja namba 208 kwenye hoteli maarufu iliyopo katika Ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi Beach jijini Dar, ilichapishwa kwenye gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda, toleo namba 310 la Jumatatu ya Aprili 8-14, mwaka huu.
Mara baada ya habari hiyo iliyoshtua wengi kusambaa kama moto wa kifuu, watu mbalimbali waliliambia Amani kuwa hatimaye Diamond amemalizia kukata uzi wa mwisho wa ndoa ya Uwoya aliyofunga na msakata kabumbu, raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ mwaka 2009.

KAMERA ZA GLOBAL KIBOKO
Vyanzo mbalimbali vilikiri kuwa ama kweli kamera za Global Publishers ni kiboko katika kutafuta ukweli wa jambo kwani ilikuwa ni minong’ono tu kuwa Diamond anatoka na Uwoya ambaye ni mke wa mtu japokuwa hakukuwa na ushahidi, lakini sasa mambo hadharani.
“Hata kama Ndiku (Hamad Ndikumana) alikuwa haamini sasa kila kitu kipo wazi, sidhani kama hapo kuna ndoa tena. Anataka ushahidi gani zaidi ya huo? Habari ya Ijumaa Wikienda imemaliza kila kitu,” alisema rafiki wa karibu wa Uwoya.
Habari zilieleza kuwa hata wasanii wenzao nao walishtushwa na habari hiyo iliyoweka rekodi kwa mwaka huu kwani kila mmoja alikuwa na lake la kusema huku wakimtupia lawama Diamond.
“Dah! Aisee ninyi Global kiboko! Hivi huyu Diamond anaona raha gani kusambaratisha ndoa ya mwenzake? Alipotembea na akina Wema, Jokate, Wolper, Penny na Aunt Ezekiel haikuwa ishu sana kwa sababu hawakuwa kwenye ndoa. Lakini kwa Uwoya, amefanya kitu kibaya sana.
“Lakini hivi huyo dogo lengo lake ni nini? Au anataka kuwamaliza wote maana ameshapita nao sana na waliobaki ni wale ambao uzuri wao ni wa kumulika na tochi,” alisema staa mkubwa wa filamu wakati akisoma habari hiyo kwenye gazeti la Ijumaa Wikienda.

WEMA ANUNA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Wema, baada ya kusambaa kwa habari ya Uwoya kunaswa na Diamond, mwanadada huyo alinuna kwa kuwa wakati alipodai kuporwa mwanamuziki huyo na Jokate, Uwoya alikuwa mstari wa mbele kuponda kuwa jamaa huyo naye ni mwanaume gani huku akimwita Domo.
“Ukweli Wema amenuna maana hakuamini kama Uwoya anaweza kutembea na Diamond,” kilisema chanzo hicho.....
Chanzo: www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...