Wednesday, April 17, 2013

BREAKING NEWZ; MSANII MKONGWE WA MUZIKI BIBI KIDUDE AFARIKI DUNIA SABABU YA KIFO CHAKE HII HAPA


Mwanamuziki maarufu na mwenye umri mkubwa kuliko nchini Tanzania, Bi Kidude, amefariki dunia leo hii akiwa Zanzibar, alikuwa anaumwa na alipowahishwa hospitali haikuwa rizki tena



Bi kidude akiwa na Prof Jay
 Fid Q akizungumzia jinsi alivyofanya collable na Bi kidude

Marehem Bi Kidude alipotembelea offisi za clouds mwaka 2010
Kidude
Mjukuu wake aitwaye Omar ameiambiaHansmbeduleblog kwa simu muda mfupi uliopita kuwa Bi. Kidude alikuwa amelazwa kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukari na uvimbe kwenye kongosho.
“Kwa ufupi alilazwa kipindi kirefu na baadaye akatolewa, lakini baadaye akaja kuendelea kuumwa tena tukampeleka hospitali tukawa tunampeleka kwenda na kurudi hapa juzi akaanza kuzidiwa tena tukampeleka hospitali moja inaitwa Keeni (???) Kwaajili ya matibabu zaidi na drip na vitu vingine lakini baadaye baada ya siku ya tatu mwenyezi Mungu akachukua roho yake,” amesema Omar.
 
Omar amesema mazishi yanaweza kufanyika kesho. Mungu ailaze roho ya marehemu Fatuma binti Baraka mahala pema peponi. Amen

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...