Wednesday, April 10, 2013

ZITTO NA DIAMOND WAIPONDA SERIKALI LAIVU LAIVU, HIKI NDO WALICHOKISEMA. SOMA HAPA



Zitto Kabwe na Diamond wameamua kuzungumza kila wanachoona sio sawa na kinachofanywa na serikali yetu huku wote wakionyesha uchungu walionao kutetea maslahi ya jamii inayowazunguka, kupitia ukurasa wake wa facebook, hiki ndicho alichokiandika Mbunge Zitto Kabwe. 
 
Zitto Kabwe
Serikali inasema kampuni za simu zinalipa kodi nyingi. Kodi gani? VAT! Nani kasema VAT inalipwa na kampuni? Hii Ni kodi ya walaji kama ilivyo ushuru wa bidhaa (excise duty). Serikali inasema kampuni za simu hazilipi kodi ya mapato Kwa kuwa zimewekeza sana, tshs 2.5 trilion! Nani kakagua huo uwekezaji? Eti Kwa miaka 5 kodi ya makampuni iliyolipwa Ni tshs 64bn, wastani wa tshs 12bn Kwa mwaka. Rwanda yenye idadi ya watu sawa na wateja wa Vodacom peke yake mwaka 2010 walikusanya corporate tax $14m, Tanzania ilikusanya $1.4m tu. Serikali iache blah blah, ikusanye kodi. TCRA ipewe Nguvu ya kukagua uwekezaji wa makampuni kama ilivyo TMAA kwenye madini. Inatosha sasa

Wakati huohuo Diamond nae alionyesha machungu aliyonayo kwa serikali kwa kushindwa kutambua mchango wao na kudai wanatumiwa wakati wa kampeni za viongozi lakini baada ya kufanikiwa na walichukuwa wakikitaka wanawasahau wasanii..
hiki ndicho alichokiandika kupitia instagram
"Dah! hivi kweli Serikali imekosa majibu ya swali la mh: Mbunge kuhusu mapato ya biashara ya ringtones..!? Kweli sasa naanza kuamini kuwa Serikali Inatukumbatiaga tu kwa Mda mfupi na kututumia Wasanii kwenye Kampeni zao kwa Maslahi yao Binafsi, kisha wanatu Damp Baada ya kufanikiwa kwenye Uchaguzi wao, bila kujali Thamani na Mchango wetu kwao...."

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...