Friday, May 31, 2013

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 YATANGAZWA UPYA KWA TAARIFA ZAIDI BOFYA HAPA


Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa
                 Dar es Salam,Tanzania
WAKATI Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), ikitangaza matokeo mapya ya kidato cha nne leo, baada ya kufanya marekebisho ya alama za viwango vya ufaulu, njama za kukwamisha Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa inaadaliwa.
Habari zilizonaswa na Habarimpya.com zinadai kwamba, Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejipanga kukwamisha hotuba ya Wizara hiyo, kwa madai kwamba Waziri huyo ameshindwa kusimamia sekta ya Elimu.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM mjini Dodoma zinadai kwamba, Wabunge hao wamepania kukwamisha hotuba hiyo na kumtaka Waziri huyo ajiuzuru ili kukisafisha Chama hicho kutokana na aibu ya mkanganyiko wa kufeli kwa Wanafunzi mwaka huu.
"Hotuba ya Wizara ya Eilimu haiwezi kupitishwa kirahisi kama Kawambwa hata jiuzuru, hatuwezi kuendelea kuwa na mawaziri wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo katika setka zao, kitendo cha mawaziri hao kushindwa kuwajibika ipasavyo ndiyo inayochangia kuharibu Chama"kilisema chanzo hicho kwa masharti ya kutotajwa majina yake na kuongeza:.
"Huu mpango unaendelea kusukwa na wabunge wa CCM waliopania kurudisha heshma ya Chama, lakizima tuanzie ndani kuwajibishana wenywe kabla ya wapinzani kuanza, kwani tukishindwa sisi watatumia udhaifu wetu kuwashawishi wananchi na hatimaye watazidi kuichukia Serikali". Wakati Waziri Dk Kawambwa akiandaliwa mazingira ya kung'olewa, Necta inatarajia kutangaza matokeo yaliyoongeza kiwango  cha  ufaulu kufikia asilimia kati ya 54 na 57, wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
 Kusoma majina ya watahiniwa wapya bopya hapa  http://196.44.162.25/csee2012/Olevel.htm

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...