Thursday, November 28, 2013

MAN UNITED YAFANYA MAUAJI, YAWAPIGA WAJERUMANI 5-0 NYUMBANI KWAO



article-2514548-19AF0C4700000578-538_634x439_34593.jpg



wachezaji wa Manu wakishangilia moja ya magoli yao
article-2514548-19AF0EF300000578-546_634x448_a5791.jpg

Wyne Rooney na Giggs wakifurahia ushindiarticle-2514548-19AF0FC400000578-195_634x453_ac806.jpg
Kagawa akikata mbuga kuelekea kutafuta goli
MANCHESTER United imefanya mauaji makubwa ugenini, baada ya kuitandika Bayer Leverkursen mabao 5-0 nchini Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya.
Mabao ya United usiku huu yamefungwa na Valencia dakika ya 22, Spahic aliyejifunga dakika ya 30, Evans dakika ya 65, Smalling dakika ya 77 na Nani dakika 88.
Wayne Rooney ndiye alikuwa nyota wa mchezo kutoka na kupika mabao manne katika ushindi huo ambao haukutarajiwa.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra/Buttner dk70, Jones, Giggs, Valencia/Young dk80, Kagawa, Nani na Rooney/Anderson dk80.
Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Omer Toprak, Can, Bender/Kohr dk81, Reinartz/Hegeler dk70, Rolfes, Castro, Son Heung-min/Derdiyok dk70 na Kiessling.

article-2514548-19AF0C4700000578-538_634x439_34593.jpg



wachezaji wa Manu wakishangilia moja ya magoli yao
article-2514548-19AF0EF300000578-546_634x448_a5791.jpg

Wyne Rooney na Giggs wakifurahia ushindiarticle-2514548-19AF0FC400000578-195_634x453_ac806.jpg
Kagawa akikata mbuga kuelekea kutafuta goli
MANCHESTER United imefanya mauaji makubwa ugenini, baada ya kuitandika Bayer Leverkursen mabao 5-0 nchini Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya.
Mabao ya United usiku huu yamefungwa na Valencia dakika ya 22, Spahic aliyejifunga dakika ya 30, Evans dakika ya 65, Smalling dakika ya 77 na Nani dakika 88.
Wayne Rooney ndiye alikuwa nyota wa mchezo kutoka na kupika mabao manne katika ushindi huo ambao haukutarajiwa.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra/Buttner dk70, Jones, Giggs, Valencia/Young dk80, Kagawa, Nani na Rooney/Anderson dk80.
Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Omer Toprak, Can, Bender/Kohr dk81, Reinartz/Hegeler dk70, Rolfes, Castro, Son Heung-min/Derdiyok dk70 na Kiessling.

PITIA SURA ZA MBELE NA KURASA ZA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO NOVEMBER 28- 2013





DSC 0002 cd0ea

DSC 0003 96fdd
DSC 0004 d1c3e
DSC 0005 ad787
DSC 0006 f81e0
DSC 0007 3ad8bDSC 0008 c7968DSC 0009 2d49dDSC 0010 e9c8aDSC 0011 6628c

DSC 0012 c8074

DSC 0013 12efb


DSC 0014 4bcae

SASA WEKINDU WA MSIMBAZI WACHUKUA BEKO WA YANGA NA ATAKUJA IJUMAA HII



NewDocument_951f5.jpg
SIMBA imemtumia tiketi ya ndege kipa wa zamani wa Yanga, Yaw Berko na atatua jijini Dar es Salaam kesho Ijumaa kufanya mazungumzo ya mwisho na klabu hiyo ya Msimbazi.
Mwanaspoti linaweza kuthibitisha pasipo shaka kuwa Berko atatua kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Kenya kwa ajili ya kufanya makubaliano ya kuidakia Simba kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaoanza Januari 25 mwakani.
Simba imepanga kumpa mkataba wa miezi sita Berko ambao utakwisha Juni mwakani na kuwepo kwake kutategemeana na kanuni mpya za Ligi Kuu Bara kwani huenda kusiwe na makipa wa kigeni kuanzia msimu ujao kama kanuni mpya zitaanza kutumika.
Tayari uongozi wa Simba umempa maagizo kipa wao wa sasa raia wa Uganda, Abel Dhaira kumtaka atafute timu nyingine kutokana na kupungua kiwango pamoja na gharama kubwa.
Mmoja wa waandishi maarufu wa Ghana aliliambia Mwanaspoti jana Jumatano kuwa Berko amepokea tiketi hiyo na atatua katika ardhi ya Tanzania Ijumaa.
Berko alipopigiwa simu kuthibitisha habari hizo, kwanza aliguna, halafu akazungumza kwa Kiswahili; "Wewe nani? Baada ya mwandishi kujitambulisha na kumuuliza kuhusu suala la kujiunga Simba alicheka halafu akasema: ''Nipigie baadaye tuzungumze nipo mazoezini." Hata hivyo hakupatikana tena.
Viongozi wa Simba walionekana kushangazwa kila walipotafutwa kuthibitisha hilo, huku wengi wakisema hawana habari na hilo.
Hata hivyo, uchunguzi wa ndani wa Mwanaspoti unaonyesha kuwa Berko ameipokea tiketi ya ndege aliyotumiwa na Simba na atatua kesho Ijumaa kufanya mazungumzo na klabu hiyo ya Msimbazi.
Berko aliondoka Yanga mwaka huu baada ya klabu hiyo ya Jangwani kumpa dola 7,500 (Sh 12 milioni) alizokuwa anawadai kutokana na kuvunja mkataba.
Yanga ilimtoa Berko kwa mkopo kwenda FC Lipopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili wabadilishane na Mnyarwanda Kabange Twite, pacha wa kiraka wa klabu hiyo, Mbuyu Twite, lakini mpango huo ulishindikana msimu uliopita.
Baadaye kipa huyo bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa mwaka 2011/12 alibaki Jangwani lakini bila kucheza akawa mtu wa kujifungia chumbani muda wote makao makuu ya Yanga.
Berko, ambaye matarajio yake ya mbele ni kuwa mchungaji wa kanisa alipokuwa anawaaga mashabiki wa Yanga mapema mwaka huu, alisema anaondoka Jangwani, lakini kuna siku watamkumbuka.
"Nimefanya kazi vizuri na Yanga na sasa narudi nyumbani kufanya mambo mengine, nitawakumbuka sana, na Yanga najua watanikumbuka sana," alisema Berko alipokuwa anaondoka.
Akiwa Yanga, Berko anakumbukwa kuwa kipa imara klabuni hapo na akawa kipa bora wa ligi msimu wa 2010/2011, ingawa nyota yake ilififia alipokuwa na majeruhi ya bega yaliyokuwa yanamweka benchi mara kwa mara hali ambayo ilizua utata kuwa alikuwa anafanya makusudi.
Berko alijiunga na Yanga mwaka 2009, akitokea Liberty Proffessional ya kwao Ghana, timu ambayo ilimuibua pia Michael Essein na nyota wengine kibao wa Ghana. Aliletwa nchini na kocha wa zamani wa Yanga, Mserbia Kostadin Papic aliyewahi kufundisha katika klabu ya Hearts of Oak ya huko.
Berko anajivunia kuiwezesha timu kutwaa mataji ya ubingwa wa Bara msimu wa 2010/2011 na Kombe la Kagame mara mbili mfululizo; 2011 na 2012.
Mwaka 2011 alidaka mechi zote Kombe la Kagame, lakini 2012 alidaka hadi robo fainali alipoumia na kumuachia Ally Mustafa 'Barthez' aliyedaka hadi ubingwa.
Chanzo:Mwanasport mtandaoni

HAPPIEST MOMENT IN MA LIFE, SIKU AMBAYOOO KWA HESHIMAA NA TAADHIMA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU ALINIITUNUKU SHAHADA YA KWANZA YA SIASA NA UTAWALA( BACHELOR OF ART IN POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION)

Hans Mbedule Dimo Ndani ya vazi la hishimaaaaaaa

 Nipo na kijana mtanashati Mlekwa ukipendaa muite mtoto wa Wenger

Babyto Fetty alihusika vilivyo

Tuesday, November 12, 2013

MSANII WA BONGO MOVIES MUHARAMI ATHUMAN a.k.a FRANCO WA BELINDA AJA NA MCHAKATO WA KUIBUA VIPAJI VYA WAIGIZAJI



Franco wa Belinda

Si sura ngeni kama ni mfuatiliaji mzuri wa film za kibongo, maarufu kama Bongo Movies, Franco wa Belinda kama alivyozoeleka kwa wadau wa tasnia hii alianza kuonekana katika film ya FAMILY TEARS iliyoandaliwa na kampuni ya Game 1st Quality. kweli ndondondo si chururu Super Director MSHINDO JUMA4(Mlezi wa wana) akakiona kipaji cha Franco na kumsajili kwenye kampuni yake ya SSG na kumchezesha movie nyingi kama Radhi ya Mama, Honey Moon, Belinda na My Brother, kutokana na malengo ya kujitanuaa zaidi kisanaa Franco aliaga kwa Super Director na kuruhusiwa bila kinyongo na kuamua kuanzisha kampuni yake mwenye ijulikanayo kama MKWAMA's FILM PRODUCTION chini ya uangalizi wa KAZINGINI PRODUCTION iliyopo Morogoro Mjini,




baadhi ya wasanii chipukiz wa mkwama's film production kutoka kongwe


Hivi sasa wamefungua tawi lake Kibaha Kongowe
UKIFIKA KONGOWE WE ULIZA K.SAM FILM ukifika K.SAM basi umefika MKWAMA FILMN& KAZINGINI PRODUCTION
MOVIES ZILIZOTENGENEZWA NA MKWAMA'S PRODUCTION NI KAMA VILI MDANANDA ILIYOSAMBAZWA NA IMK INTERTAINMENT.
KAENI MKAO WA KULA VITU VIKALI KUTOKA KWA FRANCO WA BELINDA AKIWA NA CHIPKIZI VYAJA aliongeza Franco wa Belinda kwa kujiamini



vijana wakiwa mazoezini na pozi tofauti tofauti

Sunday, November 10, 2013

BRAKING NEWZ!! NDUGU ZITTO Z. KABWE (MB) ATOA TAMKO RASMI KUHUSIANA NA KINACHOITWA “TAARIFA YA SIRI YA CHADEMA”...SOMA HAPA ALICHONENA!!! Read more: http://www.hansmbedule.blogspot.com




Ndugu Wanahabari,
NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa “Taarifa ya Siri ya Chadema” ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.

Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.

Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na kunikasirisha.

Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi mali katika nje za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.

Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu.

Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.

Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.

Raia huyo wa Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.

Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara mojakukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.

Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.

Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa KUPOTEZWA endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi, kikanda, kikabila na kidini.

Natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii. Nitahakikisha kwamba wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.

Ni matarajio yangu kwamba wale wenye mapenzi mema na Tanzania, mimi binafsi na utawala wa sheria, wataelewa nia yangu ya kutafuta haki katika suala hili.

Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”
Forward Ever, Backward Never- Kwame Nkrumah
Zitto Kabwe (Mb)


Read more:

Wednesday, November 6, 2013

CHECK OUT THIS SERIES OF CAUGHT IN THE ACT, WHICH WAS MOST DISASTROUS? WHO REALLY FOUGHT FOR MAN?

Who had the Nigerian blood? Case A Case B Case C Case D Meanwhile for women that go all out stealing married men from their Homes Be Warned!!!. Many days for the thief, one day for the Owner. Just a Piece of Advice. - See more at: http://ellist.com/ng/forum/3523/photos-caught-in-the-act#sthash.X3hj6pI0.eZaJxaNO.dpuf






PICHA ZA AKINADADA WALIOPIGWA WAKIWA NA PEDESHEE NDANI YA BONGO








Monday, November 4, 2013

TAARIFA MAALUM KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU




  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu  ya mwanafunzi  na ufaulu jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa.
Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani). 
---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo.
 
Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya sekondari kwa ujumla.
Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.
Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za CA zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%). Kwa upande wa Zanzibar, CA zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia arobaini (40%) na mtihani wa mwisho asilimia sitini (60%). Pamoja na kwamba Baraza halijawahi kuutumia mifumo hii tangu ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama za CA. Kuna mawazo pia kwamba mfumo wa CA kuchangia matokeo ya mwisho ya mwanafunzi pia utumike kwa watahiniwa wa kujitegemea (private candidates).
 Kwa sasa matokeo ya mitihani ya watahiniwa hawa yamekuwa yakitumia alama za mtihani wa mwisho tu na hivyo kutafsiriwa kama utaratibu ambao unamwonea mwanafunzi ambaye anahamu ya kujiendeleza kielimu lakini anakwama kwa sababu mfumo unaotumika siyo rafiki kwa mtahiniwa.
Kwa mantiki hii, Wizara imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ili kupata muundo mmoja na ulio wazi kwa wadau wote wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imedhamiria kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika na ambayo inahuishwa mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi mbalimbali.
VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA MWAKA 2014 KIDATO CHA SITA
Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:
a)      Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine.
b)      Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii
(i)         makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alama Blitakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini).

(ii)        Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili.

(iii)       Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama na ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha. Alama F ilikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1. 
c)      Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika
(i)         Alama A itakuwa na maana ya ufaulu uliojipambanua (distincion or outstanding performance),
(ii)        Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance),
(iii)       Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance),
(iv)       Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance);
(v)        Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance),
(vi)       Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na
(vii)      Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance). 
Wataalamu katika maeneo mbalimbali ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa kushirikiana na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.
d)      Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu mzuri ambao hauhitaji urekebu wa lazima, wakati alama D na E ni alama za ufaulu unaohitaji urekebu kadri mwanafunzi atakavyokuwa anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana na mahitaji ya eneo husika (targeted remediation). Alama F iwe alama ya eneo linalohitaji urekebu wa hali ya juu (intesive remediation) ili mwanafunzi huyo aweze kumudu masomo kadri anavyoendelea kukua kielimu ama atakapoingia katika ulimwengu wa kazi.
e)      Makundi ya alama yatajumuisha CA kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40 na mtihani wa mwisho kwa asilimia isiyozidi 60 kwa makundi yote ya watahiniwa ikiwemo wale wa kujitegemea (private candidates). Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri unapoanzia ambayo ni C au 40.
f)       CA kwa upande wa Kidato cha Nne zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili (alama 15), matokeo ya Kidato  cha Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa Mock (alama 10) na kazi mradi  auProjects (alama 5). Kwa upande wa Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana na muundo unaotumika sasa.
g)      CA zitumike pia kwa watahiniwa wa kujitegemea. Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegmea ambao wanarudia Mitihani, CA zao  zitumike zile zilizotumika kutoa matokeo yake ya mitihani ya awali.  Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa Qualifying Test (QT), matokeo ya QT yatumike kama CA na mtihani wa mwisho uchangie alama 60.
h)      Kwa vile alama endelevu kwa mwaka 2013 kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne tayari zimeshawasilishwa Baraza la Mitihani  Tanzania, alama hizo zichangie asilimia 40 katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013.
i)        Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) utaandaliwa na kuanza kutumika pale utakapokuwa tayari na wadau wataelimishwa kuhusu muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya sekondari.
j)        Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia. Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya sekondari ya kawaida na nane ya elimu ya sekondari ya juu kupimwa. Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya mitihani unaweza ukafanyika iwapo matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani liguswe na kuhuishwa pia.
Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini:
Jedwali Na 1
MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU
ALAMA
UWIGO WA ALAMA
IDADI YA ALAMA
TAFSIRI
A
75 - 100
26
Ufauli Uliojipambanua
B+
60 - 74
15
Ufaulu bora sana
B
50- 59
10
Ufaulu mzuri sana
C
40 - 49
10
Ufaulu mzuri
D
30 - 39
10
Ufaulu Hafifu
E
20 - 29
10
Ufaulu hafifu sana
F
0 - 19
20
Ufaulu usioridhisha
Kwa aina hii ya muundo wa alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla haujaanza kutumika, katika kipindi hiki mpaka wakati huo, muundo wa madaraja utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.
Jedwali Na 2
MUUNDO WA MADARAJA
MUUNDO WA ZAMANI
MUUNDO MPYA
MAELEZO
POINTI
DARAJA
POINTI
DARAJA
7-17
1
7-17
I
Kundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana
18-21
II
18-24
II
Kundi la ufaulu mzuri sana
22-25
III
25-31
III
Kundi la ufaulu mzuri na wa wastani
26-33
IV
32-47
IV
Kundi ufaulu hafifu
34-35
0
48-49
V
Kundi la ufaulu usioridhisha

Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.
Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu.
HITIMISHO
Mabadiliko haya yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. Yako mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu. Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ama Big Results Now (BRN). Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.
Imetolewa,
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...