Sunday, August 6, 2017

SEX SLAVE. Sehemu ya.(1)

******
Jasho lilizidi kumtoka Mzee Alex Mwandambo!Hasira zilimpanda maradufu, mapigo yake ya moyo yalimwenda mbio,kifo cha kuteseka ndicho kitu alichokuwa anakifikiria kichwani mwake huku akiwa katika kasi ya ajabu akiendesha gari lake usiku wa saa saba kurejea nyumbani kwake,alishaelewa nini maana ya ugonjwa hatari wa virusi vya UKIMWI unavyotesa kabla ya kukutowesha duniani,aliona bora afe haraka kuliko kufa na kifo kibaya kama hicho,
alijilaumu sana kuisaliti ndoa yake,alimlaumu shetani siku zote.Watoto wake Jamal na Mackline aliwaonea huruma sababu bado walikuwa wadogo mno kukosa mapenzi ya baba yao.Alifika nyumbani kwake Afrikasana na kuweka gari getini kabla ya kuingiza gari ndani.Geti likafunguliwa na mlinzi.
“Noo! Hapana lazima nikumalize Hafuani,siwezi kukuacha uendelee kuishi duniani”
Hapo ndipo Mzee Alex Mwandambo alipogeuza shingo yake nyuma na kuanza kurudisha gari kinyume nyume na kulitoa kwa kasi kama mtu aliyechangayikiwa,alitetemeka kwa hasira,Msichana mdogo aliyemuambukiza ukimwi hakutaka kumuacha hai,alitaka kumuua,hiyo ndiyo aliamini kuwa ingekuwa adhabu ya binti huyo ambaye atakaye ukatisha uhai wake.
Kifupi Mzee Alex Mwandambo alikuwa mfu aliye hai na hivyo ndivyo alivyoamini tangu apewe majibu hayo wiki nne zilizopita.
Alivyofika Mwenge mataa alikunja kulia na kuchukua barabara inayokwenda Ubungo baada ya dakika kumi baadaye alifika maeneo ya chuo kikuu cha UDSM bado alikuwa katika mwendokasi uleule,alivyofika kituo cha polisi alikunja kona na mbele kidogo kulikua kuna msitu wenye giza na miti mingi,aliweka mguu kati na kupiga breki za ghafla na kufanya vumbi litokee na kuonekana japokuwa kulikuwa kuna giza totoro,kutokana na hasira  alizokuwa nazo alishuka garini bila ya kufunga mlango huku gari likiwa bado linawaka, linamulika! taa za mbele hazijazimwa.
“Wewe Malaya bado haujafa tu?”
Hilo ndilo swali la kwanza kulitupa kwa msichana aliyekuwa amefungwa kwenye mti na kamba za katani amezungushiwa mwilini.Licha ya kufungwa kwenye mti huo kwa siku mbili bila kupata matunzo lakini bado alikuwa mzuri,alikuwa mweupe wa kung’aa mwenye midomo milaini..
ITAENDELEA..  -

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...