Katika mitaa ya miji na majiji nchini, siyo jambo
la ajabu kukutana na mabango hayo, ambayo hata hivyo kushamiri kwake
kunaleta picha kwamba ni kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo
nchini, huku watoa huduma husika wakinufaika kwa kujikusanyia kiasi
kikubwa cha fedha kutoka kwa wahitaji.
Pia dawa zinazodaiwa kukuza makalio maarufu kama
‘mchina’, zimekuwa gumzo baada ya kuingia nchini, huku zikielezwa kukosa
ubora na kwamba zina madhara makubwa.
Lakini, sasa unaweza kuachana na dawa hizo za
Kichina, baada ya kugundulika mmea wenye uwezo wa kukuza makalio,
matiti, pamoja na kurefusha uume.
Taarifa za kiutafiti zinautaja mti huo kwa jina la Mvunge, ukiwa na uwezo wa kukuza makalio, matiti na kurefusha uume.
Kaimu Msajili wa Tiba Asili na Tiba Mbadala
nchini, Dk Naomi Mpemba anasema kuwa mmea huo ambao huwa ni mti mkubwa
upo na kwamba una uwezo mkubwa wa kukuza maumbile hayo.
Anabainisha kuwa mmea huo ambao hukua na kuwa mti
mkubwa huzaa matunda yanayotumika kama dawa na unapatikana wilayani
Korogwe Mkoa wa Tanga, Pwani, Mbeya, Morogoro na baadhi ya mikoa nchini.
“Tulifuatilia na kutambua kuwa mti huo upo maeneo
hayo na unatumiwa zaidi na waganga, hata picha za mti huo tunazo,”
anasema Dk Mpemba na kuongeza:
“Jina jingine unaitwa Miegeya, mara nyingi
unastawi katika maeneo yenye ardhi ya unyevunyevu, una tabia ya kustawi
kama Mwembe na matunda yake huonekana kufanana na Mbuyu.”
Hata hivyo, anasema kuwa asilimia kubwa ya waganga
wa tiba asili na tiba mbadala wanaotumia dawa hiyo ni wale wasiokuwa na
usajili kutoka baraza hilo, hivyo kufanya huduma hizo kinyume cha
utaratibu.
“Kwa mujibu wa masharti yaliyopo katika agizo la
Serikali kwa waganga hao, miiko, maadili na utendaji wa kazi zao
umeelekeza kuwepo na usiri na kuaminiwa, kwa hiyo sisi tunaamini
wanaojitangaza kutibu mambo hayo ni matapeli,”anasema Dk Mpemba.
Wasiwasi
Wasiwasi
Huku akionyesha wasiwasi wa kutoa picha za mti huo, Dk Mpemba
alisema kwamba endapo utaonekana wazi kupitia vyombo vya habari, jamii
inaweza kuathirika kwa sehemu kubwa kuutafuta.
Dk Mpemba alitahadharisha kuwa matumizi ya mmea
huo siyo mazuri kwa vijana, badala yake akasisitiza matumizi ya lishe
bora kupitia vyakula vinavyojenga mwili.
“Suluhisho ni lishe na siyo kuhangaika na dawa za
ajabu, tatizo lenu vijana vyakula ni chipsi, mayai, nguvu zikiwaishia
matokeo yake ndiyo mnaanza kutafuta dawa za kurefusha sehemu za siri,
haitawasaidia, dawa ni lishe tu,”alisisitiza Dk Mpemba.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Tiba za Asili wa
Taasisi ya Utafiti wa Tiba nchini NIMR, Dk Hamis Malebo, alisema Nimr
inaufahamu mmea huo, ingawa haijaufanyia utafiti wa kuthibitisha uwezo
wake huo.
Alisema mmea huo kisayansi unaitwa Kigelia Africana na unapatikana katika maeneo mengi ya Afrika.
“Masuala ya tiba asilia yanaweza wakati mwingine
kuwa na utata na sisi hatuwezi kusema sana kwa sababu hatujafanya
utafiti,” alisema Dk Malebo.
Alisema Nimr haiwezi kuzungumza kwa undani kwa
sababu bado haijawathibitisha watu waliowahi kupata tiba ya mmea huo,
wala haijahakiki chochote kuhusu matunda au mizizi ya mti huo kufanya
kazi.
CHAMA
Mkurugenzi wa Kampuni ya Boresa na Mratibu wa Chama cha uratibu wa dawa za tiba asili Tanzania, Boniventura Mwalongo anasema:
“Serikali ifanye majadiliano na kuchunguza, kisha
ieleze sasa kama mwanaume kuwa sehemu fupi za siri ni tatizo, au
mwanamke kuwa na makalio madogo ni tatizo kwa sababu ya mazingira
yalivyo kwa sasa kwenye jamii.”
Mwalongo alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema
kuwa uchunguzi unahitajika, ili kutofautisha ugonjwa na maumbile ambayo
mtu alizaliwa nayo, ili kutoa msaada wa huduma hiyo kama walivyo
wagonjwa wengine.
“Kwa sasa kinachofanyika ni utapeli tu, kwa sababu
huwezi kujua kama ni ugonjwa au ni maumbile. Kwa nini mtu aongezewe
ukubwa wa maumbile yake wakati alizaliwa hivyo?” alisema akihoji na
kuongeza:
“Endapo itabainika kweli kuna ugonjwa, watu wanapungua ukubwa wa sehemu zao za siri, basi kunahitajika huduma hiyo.”
Mwalongo alisema kuwa mbali na kuwepo kwa dalili
za uhitaji wa huduma hiyo nchini, haoni kama kuna ulazima wa Serikali
kushughulikia suala hilo, badala yake akataka iwekeze katika matibabu ya
huduma nyingine.
“Kuna magonjwa mengi sana ya zamani na
yaliyoendelea kuibuka kwa sasa, kuna magonjwa yanayosababishwa na
unywaji na ulaji mbovu, dhambi na ukosefu wa mazoezi, ili kuepusha
gharama ya magonjwa haya Serikali inatakiwa kuwekeza elimu kwa
jamii,”alisema Mwilongo.
Kauli ya Serikali
Mbali na kukithiri kwa matibabu ya dawa hizo,
Serikali imeendelea kutoa onyo kali kwa waganga wote wanaotoa huduma
bila kusajiliwa kama ilivyoagizwa.
Matumizi mengine ya Mvunge
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha
kuwa mti huo umekuwa ukitumika kwa miaka mingi, ambapo baadhi ya wazazi
ama vijana binafsi huamua kwenda kwa wataalamu wa tiba za asili na
kupatiwa huduma hiyo baada ya kubainika kuwa maumbile yao kuwa madogo
isivyo kawaida.
Mti huo pia unaelezwa kutumika kuponya wazee ambao
viungo vyao vimepoteza uhalisia wake pamoja na kutibu ugonjwa wa kuziba
njia ya haja ndogo, ukipata umaarufu katika maeneo ya Wilaya za
Handeni, Kilindi na Bagamoyo mkoani Pwani,ambapo hupatikana zaidi maeneo
ya mabondeni.
Mizizi, matunda, mbegu za matunda, magamba ya mti na majani vyote hutumika kama dawa na chakula.
Matunda yaliyoiva na mabichi ya mti huo ni sumu
kwa binadamu, lakini baadhi ya watu hukausha matunda hayo na
kuyachanganya katika pombe za kienyeji ili kuongeza ladha.
Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa
ya asili, kwa mfano kulainisha chakula, kutibu kushindwa kupumua, kutibu
majeraha na maradhi ya ngozi.
Utafiti wa mti huo katika kutibu bakteria, fungasi na uvimbe unaendelea kufanyika katika nchi za Korea, Japan na India.
Ushuhuda
Mmoja wa watu wanaotoa tiba hiyo ya asili wilayani
Handeni Mkoa wa Tanga, akifahamika kwa jina la Dk Ramadhani Chenyewe,
anasema kuwa ametibu watu wengi wakiwamo vijana na wazee kutoka ndani na
nje ya wilaya hiyo, waliohitaji kuimarishwa nyeti zao.
Chenyewe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Waganga wa Jadi (MACO) wilayani Handeni, anafafanua kwamba, kwa kutumia
dawa hiyo msimu wa mvua nyingi, nyeti hukua kwa haraka katika muda
usiozidi mwezi mmoja, kutokana na tunda la mti huo kukua haraka.
“Hilo jambo ni la kweli wengi ninaowatibu wana
tatizo uume ni mdogo, na wengine nao ni wazee ambao wanaona mabadiliko
katika sehemu hizo kwa kuwa ndogo, tofauti na awali. Basi wakija huwa
ninangalia kwanza kama kweli ni ndogo, baada ya kuthibitisha ndipo
ninamuongezea,” anasema Dk Chenyewe.
Aliongeza: “Nimewasaidia wengi, tiba yenyewe ni
kwamba unakwenda kwenye mti kabla ya kufanya chochote, unaufanyia kitu
kama tambiko, baada ya hapo ndipo shughuli ya tiba zinaanza kwa kutumia
pia matunda ya mti huo ambayo yanakua kwa urefu.”
Hata hivyo, anaonya kuwa kazi hiyo inahitaji
uangalizi mkubwa kwa vile inaweza kuwa kubwa kupita kiasi, hali
inayoweza kusababisha madhara kwa mwenza.
Amewataka wanajamii kuacha kwenda kwa waganga
kukuza nyeti zao kwa nia ya tamaa ya kutaka kuwakomoa wenzi wao, akisema
hilo siyo kusudio la kuanzishwa kwa tiba hiyo ya aina yake.
Mmoja wa watu waliopatiwa tiba hiyo ya kukuza
nyeti, ambaye ni mkazi wa mjini Handeni, aliyeomba jina lake lisitajwe,
anasema kwamba alikwenda kwa waganga hao kutokana na kuona kiungo chake
hakilingani na vya wenzake.
“Mimi wakati tunacheza na wenzangu hasa kwenda
kuogelea, nilikuwa nashangaa mbona ya kwangu ni ndogo sana ukilinganisha
na wenzangu. Nikamweleza babu yangu, ambaye naye aliniangalia kisha
akanishauri twende kwa mganga ambaye anakuza kwa kutumia yale Mavungwe,”
anasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 27.
Kijana huyo anadai kwamba alitibiwa na kufikia
malengo yake kwa muda wa mwezi mmoja, tangu kufanyiwa tiba katika mti
huo maarufu sana kwa waganga wa jadi mkoani Tanga.
ebanar! Kaka wewe ni mkali kinoumer aminia vitu vyako unavyovitupia humu blogini,sema mimi mwenyewe ninatatizo la kimaumbile ayo ivyo ingekuwa vizuri sana kama ungeweka mawasiliano ya email au namba ya simu ya uyo mtaalamu wa uko "TANGA-HANDEN" anayeitw DK.Ramadhani chenyewe ili nipate iyo tiba,fanya huo msaada kaka kwani nimeshahangaikia sana iyo kitu bila kufanikiwa.
ReplyDeleteNicheki kwenye ht25411@gmail.com nikupe contacts
DeleteWeka contact zake bac mtaalam huyo ili tuzpate tiba kwa urahic...!!
ReplyDeleteDr kanyas mtaalamu wa tiba asili anazo dawa kwa ajili ya mapungufu ya nguvu za kiume na kurrfusha uume na kunenepesha uume ..anatibu UTI ..PID..PRESHA KISUKARI..
DeleteDAWA ZOTE NI ZA ASILI HAZINA MADHARA
..mtafute dr kupitia 0764839091
Hyo dokta ni muongo kanidhulumu
DeleteTupatie contact za mtaalam huyo ili tuweze kupata tiba kwa urahic.
ReplyDeleteDr kanyas ..tiba zote za asilijuu ya masuala ya uzazi ugumba..uti..na nguvu za kiume na kurefusha uume na kunenepesha uume ..dawa zote ni za mitishamba asili.mmtafute kupitia 0764839091
Deletenaitadji kupata dawa ya kunenepecha uum wangu naka CONGO DRC
ReplyDeleteDr kanyas mtaalamu wa tiba asili toka tanga anatoa tiba kwa magonjwa yote ..anatibu mapungufu ya nguvu za kiume ..anazo dawa kwa ajili ya kurefusha uume na kunenepesha uume ..mtafutr kupitia 0764839091
Deletenamba nimuhim kwamawasiliano zaidi
ReplyDeleteMtafute dr kanyas mtaalamu wa tiba toka tanga juu ya tiba ya kurefusha uume na kunenepesha uume na kuongeza nguvu za kiume kupitia 0764839091
DeleteThis comment has been removed by the author.
DeleteNataka kupunguza mana mzigo mkubwa sana
ReplyDeleteUwo mti nimeuona seemu
ReplyDeleteWapi
DeleteDr kanyas mtaaalamu wa tiba asili toka Tanga anazo dawa kwa ajili ya kutibu magonjwa yote pia anazo dawa kwa ajili ya mapungufu ya nguvu za kiume ..pia anazo dawa kwa ajili ya kurefusha uume na kunenepesha
ReplyDeleteuume..dawa zote ni za asili...kwa msaada zaid wasiliana nae kupitia 0764839091 ...pia anatibu UGUMBA ...KUZIBUA MIRIJA YA UZAZI... ...KUONDOA PRESHA KISUKAR..MTAFUTE DR KUPITIA 0764839091.....
Dr kanyas ..anazodawa kwa ajili ya kuondoa kitambi ..chunus..tumbo kubwa kwa wamama ...mtafute kupitia0764839091
ReplyDeleteMwizi mkubwa, huna Dawa mpaka leo hujaniletea. Musimsikilize huyo. Tapeli!
DeleteMi nawaacha wale chumvi ila mwisho watakufa na kisukari
ReplyDeletewww.rogersalvine.alvinejnr