Matunda husaidia kuongeza mbegu za uzazi. 
            
HALI ya maisha pamoja na mazingira husika yanayomzunguka binadamu imeelezwa kuwa ni chanzo cha kushuka kwa nguvu za kiume.
Madaktari  wengi wameripoti juu ya kuwepo kwa 
ongezeko la wagonjwa wengi wa kiume ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya 
upungufu wa nguvu za kiume.
Mwaka jana mwishoni gazeti la The Independent llilopo nchini Uingereza liliripoti kuwa hali ya afya ya viungo vya uzazi hususani kwa wanaume ilishuka kwa kiwango kikubwa na hiyo ilitokana na utafiti uliofanywa duniani juu ya ubora wa mbegu za kiume.

Utafiti huo ulionyesha kuwa katika miaka ya 1989 
hadi 2005  ulionyesha kuwa kati ya wanaume 26,000 waliofanyiwa uchunguzi
 robo tatu yake walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kuzaa.
Mwaka  1989 na  2005, kwa mujibu wa gazeti moja la
 Uingereza lilisema kwamba  “Wanaume 26,000 wanakabiliwa na tatizo hilo 
la upungufu wa mbegu za kiume.’’
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikisababisha 
nguvu hizo kuporomoka ni pamoja na kuvaaji wa nguo za ndani ambazo 
zinabana, pia wataalamu  walieleza kuwa ufumbuzi juu ya sababu maalumu 
ya nguvu hizo kushuka bado haujapatikana.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Utafiti huo ulifanywa na daktari mmoja maarufu 
katika Hospitali ya Royal Garden nchini humo aliyejulikana  kwa jina la 
Solomon Wasike ambaye alisema kuwa wiki mbili zilizopita alipata mgonjwa
 mwenye tatizo kama hilo.
Aliongeza kuwa mwanamume huyo alikuwa na umri wa 
mika 28 alikuwa amefika katika kliniki yake kwa ajili ya kupima juu ya 
uwezo wake wa kuzaa.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Daktari Wasike alisema kuwa baada ya maelezo hayo 
aliamua  kuchukua mbegu zake mwanaume huyo  kwa ajili ya vipimo 
aliongeza kuwa majibu yake yalikuwa na utata kwa kuwa yalionyesha kuwa 
mtu huyo alikuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha mbegu hali ambayo 
iliyosababisha mke wake kutopata mimba.
Wasike alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza 
mara kwa mara katika kliniki hiyo kuwa na wagonjwa wengi wa kiume wenye 
matatizo katika afya ya uzazi.
“Kinachotusumbua ni kwamba vijana wengi wanaokuja 
katika hospitali  hii wamekuwa na matatizo sawa katika mbegu za kiume na
 jambo hili linazidi kusikitisha kwa kuwa asilimia kubwa ya watu 
wanaokuja ni vijana.
Aliongeza kuwa hali hiyo inafanya tuamini kuwa 
licha ya wengine kuwa na matatizo hayo tangu kuzaliwa lakini asilimia 
kubwa ya vijana wanapatwa na tatizo hilo kwa sababu ya  hali ya maisha 
wanayopitia pamoja na mazingira wanayoishi.
Hata hivyo takwimu za kitaifa bado hazijafanywa  
juu ya tatizo licha ya kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya wanaume 
kutoka katika katika hospitali mbalimbali.
Pia kuna takwimu kutoka katika kituo cha afya Nairobi IVF 
Centre, ambacho ni mojawapo kati vituo ambavyo uhusika na upimaji wa 
mbegu za kiume kwa kiasi kikubwa ambao nao pia waleleza kuwa kiwango 
kidogo cha mbegu za kiume ambazo pia huwa ni dhoofu  kimezidi kujitokeza
 kwa baadhi ya wanaume wengi nchini humo.
Dk Joshua Noreh ambaye alikuwa anahusika na 
upimaji pamoja na utoaji wa huduma katika kituo hiko alisema kuwa 
wastani wa wanaume ambao wanatembelea katika kituo hiko huwa na umri wa 
miaka 35.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa data kutoka katika 
kituo chake asilimia 14 ya wanaume ambao mbegu zao zilifanyiwa utafiti 
zilionyesha kuwa wamekuwa na tatizo  hilo.
Aliongeza kuwa hali hiyo imezidi kwa asilimia tatu.
Aliongeza kuwa hali hiyo imezidi kwa asilimia tatu.
Miaka mitatu iliyopita asilimia 11 ya wanaume 
walionekana kuwa na tatizo hiyo hali ambayo imeonyesha kuwa tatizo hilo 
limekuwa likikua kila baada ya mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka Shirika la Chakula 
Duniani (WHO)  lilieleza kuwa mwanamume mwenye mbegu za kiume ambazo 
hazina matatizo anatakiwa  awe na mbegu za kiume kuanzia milioni 10 hadi
 20 kwa milimita.
Tatizo hilo la kuwa na mbegu za kiume ambazo ni 
dhoofu zinazosababisha kutokuwa na uwezo wa kuzaa husababishwa na 
kubadilika kwa hali ya maisha pamoja na kubadilika kwa mazingira.
Daktari huyo aliwataka wanaume kuwa makini na maisha ambayo wanaishi kwa kuwa yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mbegu hizo.
Daktari huyo aliwataka wanaume kuwa makini na maisha ambayo wanaishi kwa kuwa yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mbegu hizo.
Pia aliwataka wanaume kupunguza uvutaji wa sigara 
pamoja na unywaji wa pombe kupitiliza, kula vyakula vya kukaanga vyenye 
mafuta kwa kuwa vinaongeza  kwa kiasi kikubwa tatizo la kushindwa kuzaa.
Utafiti uliofanywa mwaka 1940 ulionyesha kuwa 
asilimia 50 ya nguvu za kiume hushuka kutokana na kiwango kikubwa cha 
unywaji wa uvutaji wa sigara, pombe pamoja na mabadiliko ya mazingira.
Pia uvutaji wa sigara 20 kwa siku na ulaji wa chipsi, baga, soseji inachangia kwa asilimia 43 kuharibu nguvu za kiume.
Pia uvutaji wa sigara 20 kwa siku na ulaji wa chipsi, baga, soseji inachangia kwa asilimia 43 kuharibu nguvu za kiume.
Dk Wasike alisema kuwa asilimia kubwa ya wanaume 
wanaosumbuliwa na tatizo hilo kutokana na hali ya mazingira wanayoishi 
ni wale ambao wanafanya kazi shambani kwa kuwa kuna aina ya madawa 
ambayo yanapulizia yanaharibu mbegu hizo.
Pia aliongeza kuwa wanaume ambao wanaendesha 
vyombo vya moto na kukaa karibu na injini hizo za magari na wale ambao 
wanapakata kompyuta katika mapaja kwa muda mrefu wanahatari kubwa ya 
kupata tatizo hilo.
Aliwataka wanaume kula mboga za majani kwa wingi 
na matunda na kupunguza ulaji mkubwa wa nyama na maziwa kwa kuwa hivyo 
pia ulichangia tatizo hilo.
Vilevile aliwataka wanaume kula vyakula vyenye 
virutubisho ambavyo vitasaidia katika kujenga mwili ikiwemo na kuvipa 
uwezo mbegu hizo.
Wanaume pia walitakiwa kuacha kuoga kwa kutumia maji ya moto kwa kuwa hupunguza uwezo wa kutengeneza nguvu zao.
Wanaume pia walitakiwa kuacha kuoga kwa kutumia maji ya moto kwa kuwa hupunguza uwezo wa kutengeneza nguvu zao.
Alishauri pia kama mwanamume anapenda kuongeza nguvu za kiume 
mwilini mwake anatakiwa apunguze kuvaa nguo za ndani ambazo zinabana na 
badala yake kuvaa zinazoachia ili kuwezesha mwili kupata hewa.
Ili kupunguza tatizo hilo hususan kwa vijana 
walitakiwa kupunguza kula mirungi kwa sababu ni hatari katika viungo vya
 uzazi vya mwanamume yeyote ambaye anapenda afya yake.
Wasike ilisema kuwa wananchi wengi wamekuwa 
wakidharau kula maharage ya soya, lakini kwa upenda wake alisisitiza 
kuwa anawashauri watu kupendelea kula maharage ya soya kwa kuwa yana 
virutubisho aina ya estrogen ambavyo huzalisha aina ya virutubisho vya 
testosterone vinavyosaidia katika uzalishaji wa mbegu za kiume.
Pia kwa mujibu wa tafiti mbalimbali walibaini ya 
kuwa Kuna aina mbili  ya vyakula ambavyo vilifanyiwa utafiti na kubaini 
kuwa ni moja ya vyakula vilivyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina 
madhara katika engezeko la nguvu za kiume.
Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na tangawizi 
ambapo walieleza kuwa huweza kuliwa ikiwa imechemshwa ambapo wengine 
huifanya kama ni chai.
Pia tangawizi hiyo inaweza kuchanganywa na vitu 
asilia mfano  wa kiasili kwa kutumia asali, kitunguu saumu ama tangawizi
 yenyewe.
Aina ya pili ni tunda la Tikiti maji ambapo linaweza kuliwa kwa kutengenezwa kama juisi au linaweza likaliwa lenyewe kama tunda.
Aina ya pili ni tunda la Tikiti maji ambapo linaweza kuliwa kwa kutengenezwa kama juisi au linaweza likaliwa lenyewe kama tunda.
Kutokana na kuwapo kwa tatizo hilo la upungufu wa 
nguvu za kiume nchini Kenya  waliamua kufungua mtandao wa masuala ya 
afya ya uzazi ili kuwawezesha kutoa mafunzo mbalimbali juu ya tatizo 
hilo.
Kiongozi wa masuala ya afya ya uzazi nchini humo, 
Dk Isaack Bashir alisema kuwa mtandao huo pia utatoa fursa kwa wataalamu
 mbalimbali kuelezea juu ya afya ya uzazi.
Alisema kuwa mtandao huo ulifadhiliwa na USAID wakisaidia na FHI pamoja na Wizara ya Afya kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.
Alisema kuwa mtandao huo ulifadhiliwa na USAID wakisaidia na FHI pamoja na Wizara ya Afya kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.
 
No comments:
Post a Comment