LOS ANGELES, Marekani
WAKATI wanawake wengi duniani wakihangaika kukuza ukubwa wa makalio yao, huku wengine wakitumia njia ya kuvaa taiti zenye hipsi, wanaume wengi huko mjini Los Angeles wamejikuta wakigeukageuka kumwangalia mwanamke mwenye makalio makubwa kupita kiasi kila apitapo njiani.
WAKATI wanawake wengi duniani wakihangaika kukuza ukubwa wa makalio yao, huku wengine wakitumia njia ya kuvaa taiti zenye hipsi, wanaume wengi huko mjini Los Angeles wamejikuta wakigeukageuka kumwangalia mwanamke mwenye makalio makubwa kupita kiasi kila apitapo njiani.
Mikel Ruffinelli ni mwanamke ambaye mpaka sasa 
‘ameishavunja shingo’ za wanaume wengi. Makalio yake na hispi zake za 
asili zimemfanya atawazwe kuwa mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko 
wanawake wote duniani.
Mikel anayeishi nchini Marekani hajatumia dawa za 
mchina wala dawa zozote kama wafanyavyo akina dada wengine na ndiye 
aliyetambulishwa kuwa ndiye mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake 
duniani. Mpaka sasa mama huyo mwenye familia yake ana  hispi zenye  mita
 2.44.
Umbile lake halikuja hivihivi, bali alikuwa ni mtu
 mwenye umbile la kawaida, licha ya kukiri kuwa ndugu zake wengi wana 
maumbile makubwa.
Hipsi za mwanamama huyo zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku kadiri alivyokuwa akijifungua watoto wake.
Mikel Ruffinelli, ambaye ni mama wa watoto wanne 
ana umri wa miaka 39 na ni mkazi wa Los Angeles amejisifia kuwa umbile 
lake limekuwa likiwachanganya wanaume wengi.
Akiwa na kiuno kidogo kisichoendana na mwili wake cha inchi 40, hispi zake zina mzunguko mkubwa wa inchi 96.
“Nalipenda umbile langu na sina mpango wa kujikondesha kwa diet,” alinena Mikel na kuongeza kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake wenye maumbile makubwa siyo wale wembamba wembamba.”
Akiwa na kiuno kidogo kisichoendana na mwili wake cha inchi 40, hispi zake zina mzunguko mkubwa wa inchi 96.
“Nalipenda umbile langu na sina mpango wa kujikondesha kwa diet,” alinena Mikel na kuongeza kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake wenye maumbile makubwa siyo wale wembamba wembamba.”
Lakini kauli hiyo, imepingwa vikali na Jennifer 
Lopez, Kim Kardashian na Beyonce ambao wanasema inategemea na mwanaume 
husika na namna kile anachokipenda, lakini wakati mwingine hutegemea na 
mazoea ya mwanamume.
Mikel pamoja na kutamba na maumbile yake hayo 
ambayo anadai ni urithi toka kwenye familia yake ambapo karibuni ndugu 
zake wote wa kike nao wana hispi kubwa.
Mikel amelazimika kuishi tofauti ili aweze 
kuendana na umbile lake, hawezi kuenea kwenye gari ndogo hivyo gari 
analoliendesha ni kama lori.
Akiwa nyumbani kwake inabidi akae kwenye makochi 
yaliyotengenezwa kwa chuma badala ya mbao, pia kitanda chake nacho ni 
futi saba kwa saba.
Mume wa Mikel, Reggie Brooks mwenye umri wa miaka 
40 ameelezea kupagawishwa na umbile la mkewe na ameongeza kuwa kila siku
 humsifia kwa kumwambia jinsi gani alivyo mrembo.
Mikel na mumewe wapo kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa
 na wamefanikiwa kupata watoto watatu ambapo mtoto wa kwanza wa Mikel 
alizaliwa katika ndoa yake ya kwanza kabla hajaachika na kuolewa na 
Reggie.
Mikel ameongeza kuwa kwa miaka mitano iliyopita amekuwa 
akijiingizia kipato chake kwa kupiga picha za mavazi kwa ajili ya Tovuti
 ya Big Beautiful Women ambapo katika kila wakati anapoitwa kupigwa 
picha hulipwa Dola 1,000.
Anasema, “Mara nyingi ninapokuwa katika picha za 
tovuti, ninajitahidi sana kuchagua nguo zitazonifaa. Hivyo wabunifu 
wananifunza kuuelewa mwili wangu na nguo ipi inaufaa, nami sina tatizo 
katika suala la uvaaji.”
Mikel Ruffinelli, mwenye uzito wa kilogramu 191 amekuwa na unene uliozidi tofauti na urefu alionao.
“Ninaipenda shepu yangu na sina matatizo ya kiafya
 hivyo sioni sababu ya kupunguza mwili kwa kujinyima kula na wakati huu 
nina mpango wa kuongeza mlo ikiwezekana,” anasema Mikel ambaye hula kuku
 mzima na vyakula vingine vya wanga na protini kwa siku.
Mazoezi ya Mikel hutegemea na siku husika, mara 
nyingi anasema hufanya matembezi ya jioni akiwa na mume wake na wakati 
mwingine huamua kutembea sehemu moja hadi nyingine kuzunguka nyumba 
yake.
Mume wake ambaye ni mtaalamu wa masuala ya 
kompyuta anasema anavutiwa zaidi na mkewe na hapendi kabisa apungue 
mwili na anadhani ni mwili mzuri tu kwa kuwa hajatumia madawa kuukuza.
Alipokuwa na umri wa miaka 22, Mikel alipata mtoto
 wake wa kwanza Andrew ambaye hivi sasa ana miaka 19, kutoka katika 
uhusiano uliopita na hapo ndipo alipoanza kuongezeka uzito.
Alianza kwa kuongezeka kilo 82.5 na baadaye alifikia kilo 108. Baadaye alikutana na Reggie na baada ya miongo mitatu sasa wana watoto watatu. Destynee, 13, Autumn, nane na Justyce, saba. Na hivi sasa hipsi zake zimetanuka mpaka kufikia uzito wa kilogramu 191.
Alianza kwa kuongezeka kilo 82.5 na baadaye alifikia kilo 108. Baadaye alikutana na Reggie na baada ya miongo mitatu sasa wana watoto watatu. Destynee, 13, Autumn, nane na Justyce, saba. Na hivi sasa hipsi zake zimetanuka mpaka kufikia uzito wa kilogramu 191.
“Nilikuwa nikiongezeka nikiwa na ujauzito.  
Sikujua ni kwa nini uzito uliongezeka sana na hipsi kuwa kubwa, 
niliendelea kula zaidi, lakini nilivyojifungua sikuweza kurudia mwili 
wangu wa awali, hivyo ndivyo ilivyokuwa.”
Mikel, ambaye alisomea Shahada ya Saikolojia, ni mwenye afya na hamu kubwa ya kula na anayeweza kumaliza chakula kingi kwa siku.
“Ni maajabu kuona mwanamke anakula kalori 3000 kwa siku lakini kwangu mimi ni jambo la kawaida.
“Ninapata kifungua kinywa cha mayai mawili, soseji
 na viazi kadhaa. Mchana chakula changu kikubwa ni samaki wa kukaanga na
 chakula cha wanga kingi tu, lakini chakula cha jioni huwa ninahitaji 
zaidi mlo mzito.
“Ninapenda kutengeneza kuku wa kuoka wawili 
wakubwa na wali. Nina fungu kubwa, lakini ninapenda chakula kizuri, 
ninaandaa pia vitafunwa kama karanga, klipsi na vingine vinavyoweza 
kuliwa usiku.”
No comments:
Post a Comment