MSHTAKIWA wa kesi ya wizi wa Fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania, Ajay Somani
amefariki dunia baada ya kujipiga risasi.
Habari zilizolifikia Mwananchi Jumamosi wakati
tunakwenda mitamboni na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ilala, Marietha Minangi, zinasema kuwa Jay alijipiga risasi jana
asubuhi, maeneo ya Upanga karibu na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
“Alijipiga risasi saa 2 asubuhi nyumbani kwake
Upanga, karibu na Hospitali ya Muhimbili.”, alisema Kamanda Minangi na
kuongeza kuwa haijajulikana tukio hilo kwa kwa hakuacha ujumbe wowote.
Jay alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa
pesa hizo kiasi cha Sh5.9, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yeye
pamoja na ndugu yake Ajay Soman, ambaye anatumikia kifungo cha miaka
miwili jela baada ya kupatika na hatia katika kesi nyingine ya EPA.
Mbali na ndugu hao wawili, washtakiwa wengine
katika kesi hiyo ni Kanda wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na
binamu yake Frijala Hussein, ambao tayari wanatumikia kifungo gerezani
baada ya kupatikana na hatia katika kesi nyingine tatu za EPA.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni waliokuwa
wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Madeni na Bosco Kimela aliyekuwa Kaimu Katibu wa BoTna Imani Mwakosya,
ambapo walisomewa maelezo ya awali Julai 26, 2012 na kesi hiyo iko
katika hatua ya usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa mashtaka.
No comments:
Post a Comment