Friday, September 15, 2017

Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki tatu tu. Sehemu ya kwanza

 LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:- Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.
Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500 -Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jioni.

Inaendelea part 2


Thursday, September 14, 2017


Ladies BreakFast๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡



1. Kamwe usiishi na mwanaume ambaye hujaolewa naye, usiishi na 'boyfriend' wako kinyumba hata kama ni mchumba wako, utaonekana uko 'cheap' na ndoa unaweza ukaisikia kwenye bomba.
Labda kama mmeamua kuishi hivyo hivyo bila Ndoa halali inayotambulika serikalini au na dini zenu.
.
.
2. Usibebe mimba ya boyfriend wako. Siyo busara. Zuia kupata mimba kabla hajakuoa. Kumbuka kwamba kamwe huwezi kutumia ujauzito kama kigezo cha kumfanya akuoe. Wanaume wangapi wana watoto nje ya Ndoa?
.
.
3. Jitahidi kuzuia kutoa mimba, mmefanya, umepata mimba itunze kutoa mimba kunaweza kukakufanya uwe mgumba maisha.
.
.
4. Kamwe usiwatenge wazazi wako kwa sababu ya mwanaume, muda mwingine mapenzi hufanya watu waonekane wapumbavu. Usiruhusu mapenzi yatawale akili yako, penda kwa akili na sio kwa moyo.
.
.
5. Usifikirie kujiua kisa 'boyfriend' wako kakutosa, hana thamani hiyo, siyo mwanaume mzuri pekee katika dunia.
.
.
6. Usipoteze masomo yako kwa sababu mwanaume amekutaka umtembelee kwake. Hii itakufanya uonekane uko 'cheap' pia na kumbuka kesho yako ni muhimu kuliko huyo 'boyfriend' wako mlikokutana ukubwani.
.
.
7. Usimwombe mwanaume akuoe, hustahili kufanya hivyo na wewe una thamani yako, usijiweke kuwa wa rahisi kiasi hicho.
.
.
8. Hakuna kitu mwanaume hapendi kama majibizano, kubaki kimya ni adhabu kubwa sana kwa mwanaume mkorofi. Niamini mimi katika hili.
.
.
9. Katika ndoa Usimchunguze mwanaume kama unampenda na unajua huwezi kumuacha. Mwanaume siku zote huhitaji nafasi na uhuru, hapendi kuingiliwa katika mambo yake, mnaweza mkapinga ila huo ndio ukweli toka enzi na enzi. Kama una uwezo wa kuachana naye mchunguze tu bila wasiwasi wowote.
.
.
10. 'Wavulana' hutizama mwili wa mwanamke na kumhitaji kwa ajili ya kuburudisha maungo yao, ila 'wanaume' hutizama hulka na tabia za mwanamke katika malezi, uvumilivu, usaidizi, ushauri wa maendeleo na amani ya moyo (piece of mind).
____________________________________
KUMBUKA: Maneno yangu siyo sheria, ila nimeongelea kutokana na uzoefu na jinsi mambo yanavyoendelea katika ulimwengu wa sasa, unaweza ukaamua kuyafuata au ukayapotezea.  - #regrann

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...