Mahakama kuu leo imetangaza
dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa
ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje
ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya
kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja
adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu
umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo
wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo
masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake
itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba
uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho
kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani
Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya
masharti.
No comments:
Post a Comment