Hatua ya mwisho ya michuano ya kufuzu kombe la dunia kwa Bara la Afrika imeanza hii leo kwenye viwanja viwili tofauti .
Nchini Ivory Coast The Elephants ambao ni timu ya taifa ya Ivory Coast waliwakaribisha Senegal katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo .
Ivory Coast wakiongozwa na Didier Drogba walishinda mchezo kwa matokeo ya 3-1 baada ya mabao ya Drogba , Salomon Kalou huku bao lingine likiwa la kujifunga mwenyewe toka kwa mlinzi wa Senegal Ludovic Sane .
Mwishoni kabisa mwa mchezo huo Senegal walipata la ugenini ambalo linawapa matumaini kwenye mchezo wa marudiano ambalo lilifungwa na mshambuliaji Papiss Demba Cisse .
Matokeo haya yanawafanya Ivory Coast kwenda kwenye mchezo wa marudiano wakiwa na matumaini ya kusonga mbele huku wakifahamu kuwa wanahitaji kupata walau sare ili kukata tiketi ya kwenda Brazil.
Kwingineko Burkina Faso wakiwa kwenye uwanja wao wa Agosti 4 waliwafunga Algeria 3-2 katika mchezo uliokuwa na upinzani wa aina yake .
Mabao ya Burkinabe yalifungwa na Jonathan Pitroipa , Aristide Bance na Djakaridja Kone huku Algeria wakifunga kupitia kwa Soufiane Feghouli na Carl Medjani .
Michezo hii itaendelea hapo kesho wakati ambapo Nigeria watacheza na Ethiopia huko Addis Ababa huku Tunisia nao wakicheza na Cameroon . Siku ya jumanne Ghana watakuwa wenyeji wa Misri .
No comments:
Post a Comment