Risti ambazo wanadai kuwa wamekuwa wakitozwa faini kubwa ambazo kisheria haipo kabisa
Hali ya mgomo wa madereva daladala katika Manispaa ya Iringa limechukua sura mpya baada ya madereva hao kuamua kueleza uozo uliopo katika ofisi za Sumatra mkoa wa Iringa kuwa amekuwa chanzo cha wao kunyanyasika.
Madereva hao wamesema kuwa hawajapendezwa na utendaji kazi wa Sumatra ikiwa ni pamoja na kuondoka mkoa wa Iringa kutokana na kushindwa kuifanya kazi hiyo kwa misingi inayokusudiwa.
Madereva hao wametoa kilio chao katika kikao cha kamati ya usalama barabarani kilichofanyika katika ukumbi wa jumba la maendeleo mjini Iringa.
Kwani wamedai kuwa vikwazo mbali mbali ambazo wamekuwa wakivipata madereva mjini Iringa vinasababishwa na utendaji mbovu wa Sumatra mkoa wa Iringa pamoja na baadhi ya askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa ambao wamekuwa wakichangia kuwakandamiza zaidi.
Suala la kufutwa kwa stendi ya posta na miyomboni kutakiwa kupita badala ya kuegesha daladala zao pia limekuwa ni kikwazo zaidi kwa madereva hao na kuwa hawapo tayari kuendelea kufanya kazi iwapo kiongozi huyo wa Sumatra mkoa wa Iringa ataendelea kuwepo ofisini .
Awali mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas aliwataka madereva hao kutuliza jazba na kueleza madai yao katika kamati hiyo ili kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. |
No comments:
Post a Comment