MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa,
imewahukumu watu saba kutumikia kifungo cha miaka 196 pamoja na kazi
nzito,mara baada ya kupatikana na hatia ya kuharibu mali pamoja na
kujeruhi na kusababisha kifo cha mzee mwenye umri wa miaka 68.
Waliohukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 28 kila
mmoja na adhabu nzito ni Oden Msongela(40),Gilbeth
Mwanandenje(43),Philibeth Abel(20),Meres Namazali(68), Edwin
Masimba(30), Sabas Alfred(18),Wenseslaus Kakwale(30) pamoja na Michael
Simfukwe(33) wote wakazi wa kijiji cha Lusaka kilichopo Tarafa ya
Laela,Wilaya ya Sumbawanga.
Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa
Polisi ,Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Shani mbele ya Hakimu
Mkazi wa Mahakama hiyo,Manase Goroba kuwa washtakiwa hao kwa pamoja
walitenda kosa hilo Mei 13 mwaka jana majira ya usiku mara baada ya
washtakiwa hao kuvamia nyumba tatu za wakazi wa Kijiji cha Lusaka, na
kisha kuzibomoa kwa kile walichowatuhumu wenye nyumba hizo kuwa ni
wachawi.
Mwendesha mashtaka huyo wa polisi aliendelea
kuieleza mahakama hiyo kuwa katika tukio hilo washtakiwa hao kwa pamoja
walimpiga na kisha kumuua Mzee mwenye umri wa miaka 68 aitwae Michael
George, mkazi wa kijiji hicho na kisha kumjeruhi kwa kumkata na panga
mguuni Vestina Mwananzumi (29).
Mara baada ya maelezo ya ushahidi yaliyotolewa na
upande wa mashtaka yakiongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi
,Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Shani yaliiridhisha mahakama hiyo
jambo lililosababisha Hakimu Manase Goroba kutoa adhabu ya miaka saba
kwa kila mmoja na kwa kila kosa la washtakiwa hao walilofikishwa nalo
mahakamani hapa.
Hata Hivyo,hakimu huyo pia aliifafanulia mahakama
hiyo kuwa adhabu hiyo ya miaka saba kwa kila kosa waliloshtakiwa
nalo,hivyo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka saba tu kwa vile
adhabu hizo zinaambatana .
Hakimu Goroba alisema kuwa pia washtakiwa hao
wataendelea kukabiliwa na kesi nyingine ya mauji ya Mzee Michael
George ambayo bado upelelezi wake unaendelea.
No comments:
Post a Comment