Tuesday, February 19, 2013

JUKWAA LA KIKRISTO MBEYA LATOA TAMKO

Akina mama wakilia baada ya kifo cha ghafla cha Padri Evarist Mushi kilichotokea jana asubuhi kwa kupigwa risasi muda mfupi kabla ya kuanza misa ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki la Kigango cha Mtoni, Zanzibar. Picha na Martin Kabemba. JUKWAA la Kikristo Tanzania (TCF) katika Mkoa wa Mbeya, limetoa tamko la kuitahadharisha Serikali na kuitaka ichukue hatua za haraka za mata na kuwafikisha kwenye vyobo vya sheria wote waliohusika na mauaji ya Padri, Evarist Mushi. Akisoma tamko hilo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa na maaskofu, mapadri na wachungaji, Katibu wa Jukwaa hilo, Askofu Damianus Kongoro, alisema kuna mambo yanayotendeka waziwazi yakiwa na athari kubwa kwa amani na ustawi wa nchi na wananchi kwa jumla. Alisema mambo hayo ni pamoja na uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya watu wasiopenda amani lakini hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa na Serikali kuwashughulikia. Askofu Kongoro alisema kuuawa kwa wachungaji, mapadri na maaskofu kuanza kutoa matokeo mabaya. Alisema hatua zinazochukuliwa na Serikali haziridhishi wala kukidhi matakwa ya wananchi wapenda amani na badala yake, Serikali inakaa kimya au inachukua hatua ambazo kimsingi, hazitatui tatizo. *Habari na Salma Said na Elias Msuya, Zanzibar, Brandy Nelson, Mbeya na George Njogopa, Dar.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...