Monday, April 8, 2013

KIONGOZI KUTUHUMIWA NI KUKOSA UAMINIFU KWA WATU WAKO.


 Neno "TUHUMA" kamwe halifai kutajwa kwa kiongozi yeyote yule anaye fuata utawala wa haki na usawa kwa watu wake. Hata hivyo uwepo wa neno hilo katika kila tawala haukosekaniki kuwepo kwani watawala hawa wamekosa UAMINIFU kwa watu wao kwa kujiwekea maslahi yao kwanza na ya wengine baadaye. 

ADHAA YA MAJI TANZANIA
Kukosekanika kwa uaminifu huo ni kuwa na mipango mingi isiyo kuwa na tija kwa jamii na hata utekelezaji wake kuwa mgumu pia, kutokana na RUSHWA, KUTOWAJIBIKA, NA KUJILIMBIKIZIA MALI KWA WINGI.
Hali hii kamwe haitoweza kutoweka ktk jamii zetu, kama wananchi hatutawajibika kuwawajibisha "VIONGOZI WANAO TUHUMIWA KWA KUKOSA UAMINIFU" hasa ktk kutekeleza majukumu yao. Ni vema kwa VIONGOZI wetu kujitathimini kwanza wao wenyewe ktk mambo haya yafuatayo ilikuleta maendeleo yenye TIJA ktk jamii nayo ni:

1. Uimara wake ktk ushawishi wa kimaendeleo hasa kuweza kushirikisha wadau mbali2 kuchangia mfuko wa kimaendeleo ktk eneo lake la utawala, kama vile NGO's mbalimbali.

2.Kuweza kutambua changamoto za kimaendeleo ktk eneo lake mfano kujua kama wananchi wana ari ya kuchangia au kutochangia mambo ya kimaendeleo.

3.Kuangalia fursa mbalimbali zitakazo mwezesha yeye kuleta maendeleo ktk eneo lake.

4.Kutathimini madhara ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kutokana namiradi ambayo itaanzishwa, kwani si kila mradi utakuwa na matokeo chanya miradi mingine huleta adha ktk jamii.
RAI YANGU: KAMA NI MTUMISHI AWAJIBISHWE KUTOKANA NA KANUNI ZA KAZI YAKE NA KAMA NI WA KISIASA AWAJIBISHWE KWA KUTO MPA KURA 2015, MPE UNAYE DHANI ANASTAHILI BILA KUJARI ITIKADI YA VYAMA ILIMRADI ANAWEZA ANASIFA

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...