Wednesday, January 22, 2014

HAYA SASA MAJANGA KWA WANAJANGWANI ETI MMILIKI WA YANGA AIBUKA,ATAKA KWENDA KWA KIKWETE

 BABUYANGA001
ALIYEJITANGAZA kuwa mmiliki
wa klabu ya Yanga, Juma
Mwambelo, amesema yu tayari
kukabidhi nyaraka
zinazotafutwa na uongozi wa
klabu hiyo kwa Rais wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga,
Clement Sanga, alitangaza
kwenye mkutano wa Yanga
kwamba Mwambelo anashikilia
hati za umiliki wa klabu ya
Yanga kimakosa na anatakiwa
kuzikabidhisha haraka
iwezekanavyo kabla ya
kuchukuliwa hatua.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Mwombelo alisema
yupo tayari kumpa Rais Kikwete
naye aukabidhi uongozi wa
Yanga chini ya Yusuf Manji.
“Kweli hati hizo ninazo kwa
kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu
ya Yanga, ila Rais Kikwete pekee
ndiye naweza kumkabidhi, hata
mwanaye Ridhwani nimewahi
kumueleza kuhusiana na hili,”
alisema.
“Mimi ndiye mmiliki wa Klabu ya
Yanga, nina hati miliki halali ya
klabu, hii hapa (anaonyesha),
nina hati miliki ya jengo la
Jangwani, pia ninayo ya jengo la
Mafia, lakini hiyo waliiba na
tayari nilisharipoti polisi.
“Kuhusu hati ya jengo la
Jangwani ipo benki na yenyewe
sijailipia kwa kuwa kuna deni,
deni hilo ni zile fedha
ziliyotumika kujenga Uwanja wa
Kaunda. Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali
kutoa hati kisha kuirudisha
wizarani na kutolewa rasmi.
“Nashangaa Yanga wanapodai
wanatumia katiba mpya, hii siyo
halali, katiba halali ya Yanga ni
ile ya mwaka 1967 ambayo
nakala yake hii hapa
(anaonyesha),” alisema.
Alipoulizwa juu ya uhalali wa
wanachama wa sasa wa klabu
hiyo, alisema: “Wanachama
wengine wote ni feki, mpaka
unatokea mgawanyiko mwaka
1975, wanachama halali wa
Yanga walikuwa 400, kuanzia
hapo hakuna wanachama halali
tena, hata akaunti zinazotumika
siyo za klabu.
“Hapa nilipo nimekuja polisi
(Magomeni) ili kutoa taarifa ya
kujihami, nahofia kupigwa
kutokana na walichokisema
kwenye mkutano,” alisema.
Katika mkutano mkuu wa
Jumapili, uliofanyika kwenye
Ukumbi wa Karume, PTA
Sabasaba jijini Dar es Salaam,
uongozi wa Yanga ulimtaja
mzee Juma kuwa ndiye aliyeiiba
hati ya jengo la klabu hiyo tangu
Juni 24, 2009.
“Mimi nilipigwa na watu mwaka
1987 nikapoteza fahamu kwa
siku tano, tangu pale sijawahi
kwenda klabuni wala uwanjani
kuitazama Yanga, hata huyo
Mrisho Ngassa simjui, namuona
tu kwenye magazeti, kikubwa
ninachotaka ni utaratibu
ufuatwe ndani ya Klabu ya
Yanga,” alisisitiza huku
akitabasamu.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...