Friday, June 28, 2013

BOFYA HII LINK NA UPATE KUJUA SABABU YA WANAWAKE KUKOSA HAMU YA KUJAMIIANA NA MWANAUME PIA


Ni nadra kwa watu kujitangaza kuhusu uwezo wao katika uhusiano, lakini hili ni tatizo
Matatizo ya kufanya mapenzi au kujamiiana kwa wanawake yanatambulika kama tatizo linalojirudia kwa muda mrefu ambapo huathiri mzunguko wa tendo la kujamiiana (kusisimka, kufikia kilele, kurudia) na hivyo kusababisha msongo wa mawazo au kuharibu uhusiano  wa wanandoa au wapenzi.
 Tatizo hili huathiri asilimia 43 ya wanawake wa rika zote duniani na huonekana zaidi kwa wanawake wenye umri kati ya 45-64.
Athari za mitandao ya kijamii;
Katika tafiti mpya iliyofanyika mwaka huu nchini Marekani, imeonyesha ya kwamba kati ya ndoa 6,000 zilizovunjika asilimia 57 zimesababishwa na mwenza mmoja au wote kupenda kutumia  mitandao kupita kiasi hivyo  kupoteza msisimko kati ya wenza wawili na hatimaye kupungua hamu ya kujamiiana.
 Nini husababisha hali hii?
Msongo wa mawazo – Asilimia kubwa ya tatizo hili  husababishwa na msongo wa mawazo  unaotokana na ugumu wa maisha (uchumi), matatizo katika uhusiano (ugomvi, kutoelewana, kutoaminiana au kukosa uaminifu katika uhusiano na magonjwa mbalimbali.
Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano au  ndoa
Kujifungua mtoto – Hii ni kutokana na homoni aina ya prolactin kuwa katika kiwango cha juu wakati mama ananyonyesha, homoni hii pia hufanya kazi ya kumfanya mtu kuridhika baada ya tendo la ndoa/kujamiana.  Mbali na kunyonyesha, homoni ya prolactin pia huongezeka wakati mtu amelala (usingizi mzito au REM sleep), wakati wa alfajiri, baada ya kufanya mazoezi, kula,baada ya tendo la kujamiana, baada ya upasuaji mdogo na hata baada ya kupata degedege.
Sababu nyingine ya kuongezeka kiwango cha kichocheo hiki cha prolactin ni kuwa na saratani katika ubongo. Dalili za saratani hii ni pamoja na kutonyonyesha vizuri kwa mama, kukosa hedhi, ugumba kwa wanawake na uhanithi kwa wanaume.
Kupungua mzunguko wa damu katika tupu ya mwanamke na hivyo kusababisha maumivu wakati wa kujamiana.
Hypothyroidism – Matatizo ya homoni ya tezi la koo, huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume.
Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi au vya majira kwa muda mrefu
Unywaji pombe kupindukia – Kinyume na fikira potofu za watu wengi ambao huamini  kwamba unywaji pombe kali huongeza hamu ya kujamiiana au kupunguza uzito lakini ukweli ni kwamba pombe kali au kilevi cha aina yoyote hupunguza hamu ya kujamiiana na pombe huongeza uzito na kusababisha utapia mlo.

Ugonjwa wa kisukari
Uvutaji sigara
Ujauzito – Kutokana na mabadiliko katika mfumo wa homoni au vichocheo wakati wa ujauzito, na pia kutokana na mabadiliko ya maumbile ya wanawake wakati huu na hivyo kuchangia kutojiamini kwa mwanamke.
Uzito uliopitiliza Ugonjwa wa mifupa
Utumiaji dawa ya kulevya
Madhara katika neva inayohusika na kuongeza msisimko wakati wa kujamiiana na wakati wa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kwa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi au katika mfuko wa kizazi.
Madhara ya dawa – Kama dawa za kutibu shinikizo la damu na dawa za saratani.
Uchovu – Kuzidiwa kwa mwanamke na majukumu ya kulea mtoto/watoto, kazi na kumhudumia mume wake hivyo kusababisha uchovu.
Ugonjwa wa moyo na saratani ya aina yeyote ile, wasiwasi.
Baadhi ya watu  wenye historia ya kubaskwa ambao hawajapata matibabu ya kisaikolojia hukosa hamu ya kujamiiana pia. Au wale waliopata maumivu awali.  Baadhi ya wanawake wana tupu ndogo isiyo na ute hivyo husababisha maumivu makali wakati wa tendo.
Ni kundi gani la wanawake lililo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili?
Wanawake ambao wana historia ya kupungua hamu ya kujamiana
Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali
Wanawake ambao waliofika umri wa kuacha kupata hedhi (miaka 42-58)) na kupata dalili mbalimbali kama kutokwa na jasho usiku, kukosa usingizi mzuri na msongo wa mawazo.
Wanaume
Kwa wanaume, visababishi vya tatizo la kupungua hamu au uwezo wa kujamiana ni kama ifuatavyo;
Msongo wa mawazo kama nilivyoeleza hapo juu
Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano/ndoa
Unywaji pombe kupindukia kama nilivyoeleza awali
Utumiaji wa dawa za kulevya
Uvutaji sigara – Hupunguza kiwango na uzito wa shahawa kwa wanaume. Uzito wa shahawa hupungua kwa asilimia 22-57 kwa wale wanaovuta sigara.
Uwezo wa shahawa kuogelea kwenye mirija ya uzazi ya mwanamke pia nao hupungua kwa asilimia 20 kwa wale wanaovuta sigara ikilinganishwa na wale wanaume wasiovuta sigara.
Tafiti nyingine zimethibitisha kuwa wanaume wanaovuta sigara wana asilimia kubwa ya kutoa shahawa ambazo hazina maumbile mazuri au ya kawaida na hivyo kuongeza uwezekano wa mimba au  kuzaa mtoto mwenye maumbile ambayo sio ya kawaida.
Sababu nyingine ni:
Uzito uliopitiliza– Kutokana na kuongezeka kwa mafuta ambayo husababisha mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na uume kuwa mdogo na  kupungua uwezo wa kujamiana. Kupungua uwezo wa kujamiana au kufanya mapenzi kwa wanaume  ni ishara mojawapo ya  ugonjwa wa moyo na kiharusi.
Matatizo ya vichocheo katika tezi la koo au Hypothyroidism.
Kuwa na wasiwasi na msongo wa mawazo.
 Kupenda kutazama picha za ngono kupita kiasi  kwa kutumia mitandano ya kijamii kama ilivyo kwa wanawake.
Umri – Kuanzia miaka ya 40,kiwango cha  kichocheo aina ya prolactin huongezeka na kusababisha kuongezeka kwa kichocheo  kingine aina ya ‘dihydro-testerone’ ambacho husababisha tezi dume kuongezeka na hatimaye kupunguza uwezo wa kusisimika kwa mwanamume
Madhara katika neva inayohusika na kusimika kwa uume (pudendal nerve damage).
Kuendesha baiskeli  kwa muda mrefu (kwa kipindi kimoja) – Hii hugandamiza neva na mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume na kusababisha tatizo la kupungua kwa uwezo wa kusimika kwa mwanamume kwa muda tu.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...