Saturday, June 15, 2013

MSICHANA MIAKA 19 MBARONI KWA KOSA LA KUTUPA KICHANGA CHA UMRI WA SIKU 10–SINGIDA




Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP.Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa
 waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kukamatwa kwa Aziza Jumanne (19)
 mkazi wa kijiji cha Sughana jimbo la Singida kaskazini kwa tuhuma ya jaribio la kuuwa mtoto
 wake wa kiume mwenye umri wa siku kumi.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mkulima Aziza Jumanne (19) mkazi wa kijiji cha

 Sughana tarafa ya Mgori jimbo la Singida Kaskazini, kwa tuhuma ya jaribio la kumtupa m

toto wake wa kiume mwenye umri wa siku 10 kwa lengo la kumuua.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida Geofrey Kamwela, amesema kuwa tukio hilo la aib
u na la kusikitisha, limetokea Juni 12 mwaka huu saa nane mchana kweupe katika kijiji cha Sughana.
Amemtaja mtoto huyo mchanga wa kiume aliyetupwa na mama yake kuwa ni Akramu Alfa.
Kamwela amesema siku ya tukio mama yake mkubwa na mtuhumiwa Mariamu Ramadhanai a
lipata wasi wasi baada ya kutomwona Aziza akiwa muda mrefu bila kuwa na mtoto wake mchanga.
Amesema “kutokana na wasi wasi huo, Mariamu aliweza kuita majirani kwa ajili ya kumhoji A
ziza alikompeleka mtoto wake mchanga.
Baada ya kumhoji Aziza aliweza kufunguka na hivyo kwenda kuonyesha mtoto wake shamb
ani alikomtupa na bahati nzuri, walikikuta kichanga hicho bado ki hai”.
Kamanda huyo amesema kuwa uchunguzi wa awali unaomyesha wazi kuwa Aziza ametenda 
kosa hilo baya baada ya kutekelezwa na mwanaume aliyempa mimba na kumzaa Akramu.
Hili ni tukio la pili ndani ya mwezi moja na nusu kwa watoto kutupwa na mama zao kwa lengo la
 kuwaua.
Mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, inadaiwa mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu tawi l
a mkoa wa Singida, alimtupa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi mitano kwenye pag
ala la nyumba.
Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela hadi sasa mzazi huyo hajulikani alikokimbilia na mama
 yake mzazi kutoka Babati alifika ili amchukue mtoto huyo aliyetekelezwa, lakini hakuweza 
kukabidhiwa kwa madai hakuna ushahidi wa kuonyesha amezaliwa na mtoto wake aliyekuwa 
akisoma uhasibu.
Chanzo Lindi Yetu

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...