Sunday, October 19, 2014

EPISOD-6 PLAYGIRL STORY YAKUSISIMUA BOFYA UPATE KUISOMA

Play gal – 06

Ilipoishia..

...Yule mlinzi akaushikilia ufunguo
 wake wa getini vizuri huku
 anamuita bosi wake Jerry kwa
 sauti akienda mpaka mlangoni
 nakutaka kuingia...

Endelea...

Yule mlinzi alifungua ule mlango nakuingia mpaka ndani..
 "..Aisha huyu mlinzi naona hatujui vizuri enh.."
 Nilimwambia Aisha huku kila mmoja akipandisha nguo yake vizuri tayari kwa nakuruka ukuta japo haukuwa mrefu sana..
 Ndani ya muda mchache kila tulikuwa nje ya geti huku tukifurahia kitendo tulichomfanyia Jerry.
 "..sasa shosti tukafanye shangwe wapi..?"
 "..hilo tu wala usihofu, we twende pale 'nyumbani lounge' tukaburudike na mdada Jide kisha turudi zetu hostel..

***

Ilituchukuwa mwendo wa kama nusu saa kwa mwendo wa bajaj huku tukifurahia kwa mbwembwe zote..
 Ilipotimia mida ya saa 8 usiku Aisha alikuwa kalewa sana ila kwa upande wangu nilikuwa bado niko freshi, hivyo tukatoka nje nakukodi tena bajaj mpaka chuoni kwetu Cbe zilipo hostel.
 Ndani ya dakika chache tayari tulikuwepo hostel, nilimkokota Aisha wangu mpaka bwenini, tukajipumzisha japokuwa akili yangu ilikuwa haipo pale kabisa, kila muda nilitamani japo nipige simu ya Jerry nijue kama tumempa ulemavu wa maisha au limekufa kabisa..
 "..naombea nisikie limekufa hata sasa hivi.."
 Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiuweka mto vizuri tayari kwa kulala..
 Kesho yake asubuhi na mapema ambapo Aisha alikuwa bado na uchovu kalala fofofo, nilichukuwa simu yangu nakutuma meseji ya kiuchokozi kwa Jerry huku nikiamini kwa asilimia zote itajibiwa tu, niliandika hivi..
 '..Mambo Jerry, miss u..!'
 Kweli haikupita muda nikapigiwa simu..
 "..hallow.."
 "..sorry, naongea na Jerry..?"
 Sauti niliosikia ni tofauti na ile ya Jerry..
 "...Jerry yupo hapa Ocean road kalazwa yupo hoi toka usiku wa leo kwani we nani mwenzangu.."
 Nikajichekea kimya kimya na kwa dharau huku nikiendelea kumdadisi yule mtu..
 "..jamani mpe pole sana sana, mchana wa leo nitakuja kumuangalia, mie ni rafiki yake naitwa Tina.."
 Nilipomaliza tu kuongea na simu, nilishikwa na furaha ya ajabu huku mwili ukinisisimka nakuamini alichonifanyia mara ya mwisho kwake tayari nimeshalipizia..
 Ilipofika mida ya saa 5 tano tano, Aisha naye alikuwa ameshahamka hivyo nikamwelezea kila kitu, nakumwambia yeye abaki mie nitaenda huko hospital kuhakikisha..,
 Kwakujifanya na mie nilikuwa nampenda Jerry nikanunua Juici kubwa ya box na matunda matunda mchanganyiko, kama kawaida kichwani nikajifuka kwa mtandio huku chini nikiwa na gauni refu lenye heshima, nikiwa ndio nakaribia tu hospitali ya 'Ocean road' nikanyanyua simu nakupigia tena ile namba ya Jerry..
 "..samahani, unaweza kunielekeza wodi aliyolazwa..?"
 "..njoo huku 'block C' wodi namba 4 single.."
 Nilifuata maelekezo mpaka hapo, na nilipoingia nilikutana na wasichana wengi kama 10 na, huku wakiwa wameleta vyakula mbalimbali, wanaume walikuwa wawili tu huku baadhi ya wasichana wakishindwa kujizuia nakulia kwa sauti ya juu..
 Jerry bado alikuwa usingizini hivyo nilishindwa kumuona akiongea..
 Yule niliyekuwa naongea naye kupitia simu ya Jerry ni ndugu yake kabisa na Jerry, nilipofika yeye ndiye alikuwa karibu yangu sana nakunipa maendeleo ya Jerry alivyoambiwa na dokta..
 Nikuwa itamchukuwa muda mrefu kupona haswa lile eneo la juu ya nanii yake..
 Matamanio mengine yakanianza hapo..
 "..duh, Kumbe ndugu zake Jerry wazuri, dah ila sidhani kama atakuwa na tabia kama za Jerry.."
 Niliusemea moyo huku nikimpa vile vitu nilivyoleta. Kama kawaida Tina mie nikishaonaga wanaume weupe tu akili yote inahama nakuanza matamanio..
 Nilijikaza Tina mie nakumuongelesha yule mkaka..
 "...samahani naweza kukwambia kitu, mie nataka kuondoka.."
 "..bila samahani wala usihofu.."
 Alinifuata nikamtoa mpaka nje nakuanza maongezi naye..
 "..najua utashtuka kukuita huku lakini nachoweza kukwambia ni kwamba..."
 Kabla sijamalizia kuongea, yule kaka akapigiwa simu akapokea, alivyomaliza tu kuongea na simu akanyong'onyea ghafla..
 "...Ohh my God..!! Jerry hatunaye tena...

Nikabaki na mshangao huku siamini amini, tukajikuta wote tunakimbia mpaka wodini kuhakikisha kama kweli Jerry kafa..
 Tulipofika tu wodini wasichana walikuwa bado wamemzunguka Jerry huku wakimlilia zaidi,
 "..itakuwa kafa kweli nini..?"
 Niliusemea moyo huku nikijipenyeza katikati ya wale wasichana.
 Tabasamu kubwa alilokuwa analitoa ndicho kitu kilichowatoa zaidi machozi wakinadada waliokuwa wanamlilia, Jerry alikuwa hajafa japokuwa alikuwa hawezi kuongea lakini macho yake yaliweza kuangaza huku na kule..
 Bado swali moja lilinisumbua kichwa, ninani aliyemwambia ndugu yake Jerry kwenye simu kama Jerry kafa..?
 Nilimshika tena mkono kwa mara ya pili yule ndugu yake na Jerry mpaka nje..
 "..embu niambie vizuri nani aliyekwambia Jerry amekufa..?"
 "..anhaa, ile simu nilipigiwa na mjomba na nikweli Jerry amefariki.."
 "..Jerry..? Jerry gani sasa..?"
 "..Huyo mjomba wetu naye anamtoto anaitwa Jerry ujue jina la Jerry ni la marehemu babu yetu, sasa huyo mtoto wake mjomba alizaliwa akiwa na moyo mkubwa, na aliugua sana, ndio hivyo tena kazi ya mungu haina makosa.."
 "..dah, poleni sana.."
 Nilisisimka kana kwamba na mie ni ndugu wao tena ukarimu niliomuoneshea huyu kaka..
 "..kwa hapa Dar unakaa wapi..?"
 "..mh, nakaa kinondoni pale 'mkwajuni.."
 Alinijibu huku akinionesha tabasamu nakunifanya nisisimke tena huku nikiuangalia 'lips' zake mara mbili mbili jinsi zilivyokuwa pana..
 "..hata kama wanamatatizo, sijui wamefiwa, sijui wanauguza, mie hilo wala silitambui, huyu
 Kaka kweli simuachi.."
 Niliusemea moyo huku nikimrembulia macho nakuvilazimisha vidimpozi vyangu feki..
 "..ok, lakini unaonekana kama umeoa enh.."
 "..we bado umri haujafika, ndio kwanza nipo mwaka wa kwanza pale Ifm.."
 "..sasa hapo kinondoni unaishi na nani..?"
 "..pale nimeamua kupanga tu kachumba kamoja, sipendi kukaa hostel.. Wewe unakaa wapi..?"
 Kabla sijamjibu dokta akaja maeneo yale tulipokuwa naye nakuongozana naye mpaka ofisini..
 Nilirudi kumuangalia Jerry kinafiki kujua anahali gani..
 Kwa kipindi hiki alikuwa kafunga macho kuonesha kuwa anausingizi sana, nilitamani nichukuwe sindano pale pembeni yangu nakumchoma tena nanilii yake..
 Kitendo alichonifanyia Jerry cha kuniingilia kinyume na maumbile ndicho kilichoniuma sana nakumchukia Jerry kila nilipokuwa namuangalia pale kitandani..
 "..na kama amenipa ukimwi, naurudisha tena kwenye ukoo wao, nitahakikisha natembea na ndugu zake mpaka nawamaliza.."
 Hasira kali nilizokuw nazo ilinibidi kuzipunguza kwa kutoka nje kabisa huku nikimsubiria John 'ndugu yake Jerry' atoke huko ofisini kwa dokta..
 Haikumchukuwa muda sana nikamuona John ametoka huku akionekana mwenyehuzuni sana..
 "..enhe vipi dokta kakwambiaje..?"
 Nilimuuliza kwa shauku ya hali ya juu..
 "...Dah, 'bro' maendeleo yake yanatia huruma, na nikija kumjua aliyemfanyia hivyo, atanijua kama mimi natokea Pemba ama Unguja.."
 "..ok, niambie basi kitu gani umeambiwa na dokta..?"
 "..ni kwamba bro Jerry anapata shida sana kukojoa, hivyo watamfanyia upasuaji mdogo ili kupata njia nyingine yakutolea mkojo. Na vile vile kunamshipa ambao unatumika kupitishia 'sperm' (manii/shahawa) nao ulichanjwa ukawa wazi hivyo anaweza akakosa uwezo wa kuzalisha tena maishani mwake.."
 Pale pale nikajifanya kama muvi za kibongo nikaanza kutoa machozi yakinafiki huku nikilazimisha kukohoa na makamasi kuyavuta yalioambatana na chafya bandia..
 Alinibembeleza sana, lakini ni kama alinizidishia sauti, kwani nilizidisha sauti kana kwamba nimefiwa.
 Umati wa wauguzi pamoja na wapita njia ndio walionisaidia kuninyanyua pale chini nilipokuwa natapatapa huku nikilitaja jina la Jerry mara nyingi nyingi.
 John alinibeba akisaidiana na wapita njia mpaka kwenye gari ya Jerry kisha,
 "..unaishi wapi nikupeleke..?"
 Aliuliza John kwa hasira, kwani nilivyolia kwa sauti kulimkera sana, kumbe mie nilikuwa na mtego wangu.. Nikashusha pumzi huku nikijifuta machozi feki nakumuangalia John..
 "..nipeleke kwako kwanza
 nikabadilishe nguo yangu ya ndani imechafuka sana, niko katika mwezi.."
 Nilimdanganya ili iwe rahisi kuwa naye lakini alionesha kama kushtuka kitu,
 "..lakini mbona hapa kuna vyoo na unaweza kubadilisha tu.."
 "..kama hutaki nishushe, kwani hapa kuna mabafu? Nataka nioge kabisa.."
 "..ok, mie niko tayari kukupeleka hadi kwako hata kama ni mbali..
 "..naishi hostel, na leo Jumapili wanaume kibao bwenini.."
 Hadi mwenyewe akakubali nakuliwasha gari nakuelekea kwake, furaha ya ajabu iliyoamsha mshawasha wangu huku nikijiamini kwa asilimia zote huko tuendako lazima anifanye tu..
 Ile tunafika njia panda ya kuelekea kinondoni, John akapigiwa simu lakini hakupokea alichoniambia nipokee halafu niweke 'laudi spika' kwakuwa yeye anendesha gari,
 "..halow.."
 "..vipi mpenzi wangu J uko wapi? Mi niko kwako hapa..
 Itaendelea

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...