Wednesday, July 17, 2013

BREAKING NEWS. BENEDICT CHALES LUKUMAY WA CLUB MASAI AFARIKI KWA AJALI YA GARI. KWA HABARI ZA KINA BOFYA HAPA



clip_image001Marehemu Benedict (Kulia)
  Habari nilizozipata muda mchache uliopita na kuthibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu zinasema Benedict Chalres Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.
Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajili ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku. Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku akinieleza kuwa ilitokana na ajali ya gari.
"Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma ya roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.
Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.
Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.
Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani nyinginezo.
Ndugu Benny (Chief ) a.k.a Abogaa alikuwa shabiki wa kutupwa wa klabu ya Yanga.
Mungu alaze Pema ROHO ya Marehemu Ben.....

ARSENAL YAENDELEZA MAUWAJI, YAWAFUMUA 7-1 WAVIETNAM


ARSENAL imeendeleza wimbi la ushindi mnono katika mechi za kujiandaa na msimu, baada ya  kuifumua mabao 7-1 Vietnam XI kwenye Uwanja wa My Dinh mjini Hanoi.
Ushindi huo umemoa majibu kadhaa kocha Arsene Wenger, kwanza kama atashindwa kusajili mshambuliaji wa kiwango cha dunia kabla ya mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa, Olivier Giroud atatosha kwenye kampeni ya ushindi baada ya kufunga mabao matatu peke yake.
Pili, anaweza kumtumia Bacary Sagna katika beki ya kati itakapotokea dharula kama atakwama kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams baada ya beki huyo kulia wa Arsenal kucheza namba nzuri .
Na tatu, inayoweza kuwa muhimu kuliko zote, Jack Wilshere na kama yuko fiti kabisa kuanza msimu, baada ya kucheza mechi yake ya kwanza  tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo cha mguu Mei.
Shukrani! Wachezaji wa Arsenal wakiwa wamebeba bango la 'Asanteni' kwa ajili ya mashabiki baada ya kuwafunga Vietnam
 Shughuli: Beki wa Arsenal, Bacary Sagna akiupitia mpira miguuni mwa Nguyen Anh Duc wa Vietnam


Mbali na mabao matatu ya Giroud, mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain, Chuba Akpom mawili na Ignasi Miquel ambao wote walifunga pia kwenye ushindi wa 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dream Team ya Indonesia.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk71, Sagna/Aneke dk71, Jenkinson/Olsson dk71, Koscielny/Mertesacker dk46, Gibbs/Miquel dk46, Arteta (Nahodha)/Ramsey dk46, Rosicky/Zelalem dk46, Oxlade-Chamberlain/Wilshere dk66, Gnabry/Walcott dk46, Podolski/Miyaichi dk46 na Giroud/Akpom dk46


Olivier Giroud akifunga moja ya mabao yake 
 Mbali na mabao matatu ya Giroud, mabao mengine ya Arsenal  yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain, Chuba Akpom mawili na Ignasi Miquel ambao wote walifunga pia kwenye ushindi wa 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dream Team ya Indonesia.
Kikosi cha Arsenal  kilikuwa; Szczesny/Martinez dk71, Sagna/Aneke dk71, Jenkinson/Olsson dk71, Koscielny/Mertesacker dk46, Gibbs/Miquel dk46, Arteta (Nahodha)/Ramsey dk46, Rosicky/Zelalem dk46, Oxlade-Chamberlain/Wilshere dk66, Gnabry/Walcott dk46, Podolski/Miyaichi dk46 na Giroud/Akpom dk46




RATIBA YA MECHI ZA ARSENAL KUJIANDAA NA MSIMU

Julai 14 na Indonesia XI walishinda 7-0
Julai 17 na Vietnam wameshinda 7-1
Julai 22 na Nagoya Grampus (Uwanja wa Toyota, Japan) Saa 5.30 asubuhi
Julai 26 na Urawa Red Diamonds (Uwanja wa Saitama, Japan - Kombe la Saitama City) Saa 5.30 asubuhi
Agosti 3 na Napoli (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 4 na Galatasaray (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 10 na Manchester City (Uwanja wa Olimpiki, Helsinki) Saa 9 jioni

Monday, July 15, 2013

MTOTO ABAKWA NA KUWEKWA MIWA SEHEMU ZA ZILI MPAKA KUFA...!!! (+18)


Vanusia Silva Pereila mdada mwenye miaka 9 mkazi wa kijiji kimoja nchini brazil,mapema wiki hii amebakwa karibu na shamba la miwa na watu wanaoaminika kuwa ni watumiaji wa madawa ya kulevya.



 
MAELEZO ZAIDI KUTOKA CHANZO CHA HABARI HII HAYA HAPA.
The horrific crime happened in Arataca, state of Bahia, Brazil. Vanusia Silva Pereira was taken to a vacant lot, punched in the face, raped and then had a sugar cane forced up her snatch.

The victim’s father, identified as Mr. Wilson, an agricultural laborer told police that Vanusia chose bad company to hang out with lately and that was her demise. Police do not suspect that her murder was a crime of passion, however coroner who examined the body said the woman had been subjected to exceptional violence before death which brought the possibility of this being the crime of passion back into question.

Saturday, July 13, 2013

VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULY 13-2013. PATA NEWS ZA KITAIFA, KIMATAIFA,MICHEZO ,NA UDAKU KWA SANAA


DSC07289 DSC07290 DSC07291 DSC07292 DSC07293 DSC07294 DSC07295 DSC07296 DSC07297 DSC07298 DSC07299 DSC07300 DSC07301 DSC07302 DSC07303 DSC07304 DSC07305 DSC07306 DSC07307 DSC07308 DSC07309 DSC07310 DSC07311 DSC07312 DSC07313

SIMBA YAFANIKIWA KUMSAJILI MFUNGAJIA BORA WAKAGAME 2013 HAMIS TAMBWE. PATA UNDANI ZAIDI

.
.
Simba sports Club ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajili mfungaji bora wa michuano ya Kagame Cup 2013 Hamis Tambwe kutokea Vital O ya Burundi kwa kumpa mkataba wa miaka miwili July 12 2013 kuanza kuwatumikia wekundu hao wa Msimbazi kwa mujibu wa shaffihdauda.com

.Tambwe mbele ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba.

Thursday, July 11, 2013

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO YA UFUNDI -


WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO
UFUNDI NA CHUO CHA 'MANEGEMENT' NA MAENDELEO YA MAJI
Wanafunzi Kuripoti katika shule walizopangwa Muhula wa kwanza kwa wanafunzi
wa Kidato cha Tano kuanzia mwaka huu 2013 itaanza mwezi Julai. Wanafunzi
wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa masomo husika.
Aidha, kama baadae upungufu utajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa kufanya
taratibu za kuazima walimu wa muda na kutoa taarifa kwa uongozi wa halmashauri
husika kuhusu upungufu wa walimu uliopo. Kwa nafasi hii, ninaagiza wanafunzi wote
kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 29 Julai, 2013. Kama kutakuwa na
sababu yoyote ya msingi ya kuhamia shule nyingine, uhamisho wa kawaida utafanywa
baada ya kuripoti shuleni kupitia kwa mkuu wa shule husika, Mkurugenzi wa Halmashuri
/Manispaa na Katibu Tawala wa Mkoa.
(Wizara haitabadilisha shule walizopangwa wanafunzi)

Wanaporipoti wanatakiwa kuwa na:
   Original Result slip na Living Cerificate                                                                                                                                                                                                                                                                 




 
KWA MAJINA YA WAVULANA BOFYA LINK HII http://www.moe.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=221 MAJINA YA WASICHA BOFYA HII LINK
http://www.moe.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_download&gid=222&Itemid=385K

Tuesday, July 9, 2013

ABIRIA WA BASI LA KING CROSS WANUSURIKA AJALI IKIWA NI DAKIKA 2 BAADA YA KUTOKA STENDI

 Askari wa usalama  barabarani  mjini Iringa  akiwawataka abiria  wa basi la King Cross linalofanya  safari  zake kati ya Iringa - Mkulula Isimani kushuka katika basi hilo baada ya  kutaka  kutokea ajali mbaya  eneo la Miyomboni barabara  kuu ya Iringa- Dodoma ikiwa ni dakika mbili pekee  toka litoke  stendi kuu basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 47  lilikuwa na abiria  zaidi ya 100 pamoja na mizigo hadi mlangoni 

 Abiria  wa basi la King Cross  wakishuka katika basi hilo kwa shida baada ya  kutakiwa kushuka na askari wa usalama barabarani  ,gari hilo  lishindwa kukata kona kutokana na uzigo wa mzigo hivyo kulazimika polisi kuingilia kati japo abiria  baadhi  walionesha kugoma kushuka
 Hapa abiria  wakiendelea  kushuka katika gari  hilo chini ya usimamizi wa  polisi
 Baadhi ya abiria wakiwa wameshuka katika gari  hilo huku bado likiwa limejaa ,hawa  wote  chini  walikuwemo katika gari  hilo ambalo kwa macho ukiliona ni dogo ila idadi ya abiri  walioingia kweli ..hatari  kubwa
 Umati  wa abiria  walioshuka katika gari  hili lenye uwezo  wa kuchukua abiria 47 pekee

 Askari  polisi  mjini Iringa  wakishusha abiria katika basi la King Cross  linalofanya safari  zake kati ya Iringa - Mkulula Isimani wilaya ya Iringa  vijijini leo baada ya kujaza kupita  kiasi na  kushindwa  kukata  kona  kuingia barabara kuu ya Iringa - Dodoma eneo la Miyomboni

 Huu  ndio  umati mkubwa  uliokuwepo  ndani ya  basi  hilo ambalo lilijaza abiria  kupita  uwezo  wake  pamoja na mizigo ambapo baadhi ya  abiria  walilazimika  kubeba mizigo yao wakiwa ndani ya basi  hilo



 Hili ni Betrii ambalo  lilichomoka baada ya  gari hilo kushindwa  kukata  kona
 Mheshimiwa  diwani Franzisca Kalinga  wa kata ya Malenga Makali (kulia) pia alikuwemo katika  basi hilo

Hapa gari  hilo likipelekwa  polisi chini ya ulinzi mkali wa polisi  huku akibiri  wakitafutiwa basi jingine  zuri .

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...