MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amedaiwa kujiua kwa kujilipua kwa petroli kisa mapenzi.
Taarifa
zinasema, kufuatia moto mkali uliotokana na petroli hiyo, mbali na
mwanafunzi huyo aliyejitia mhanaga kwa mapenzi, watu wengine wanane
waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.
Akithibitisha,
leo Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, amesema tukio hilo
lilitokea jana mida ya saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka,
Kata ya Nzughuni.
Kamanda
alifafanua kwamba mapema mwanafunzi huyo alinunua lita tano za mafuta ya
petroli katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua na
kisha kwenda kujilipua akiwa katika saluni ya Irene Mapunda ambaye
inasadikiwa alikuwa mpenzi wake.
Alisema,
mwanzoni watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini
hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na
kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa
karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo
kuteketea.
"Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi,
hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa
kina juu ya tukio hili," ilieleza taarifa ya Kamanda wa Polisi.
Taarifa
iliwataja waliojerihiwa kuwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11)
Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau
(30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21) ambao wote wamelazwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na tathimini ya hasara
iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.
No comments:
Post a Comment