Tuesday, July 9, 2013

ABIRIA WA BASI LA KING CROSS WANUSURIKA AJALI IKIWA NI DAKIKA 2 BAADA YA KUTOKA STENDI

 Askari wa usalama  barabarani  mjini Iringa  akiwawataka abiria  wa basi la King Cross linalofanya  safari  zake kati ya Iringa - Mkulula Isimani kushuka katika basi hilo baada ya  kutaka  kutokea ajali mbaya  eneo la Miyomboni barabara  kuu ya Iringa- Dodoma ikiwa ni dakika mbili pekee  toka litoke  stendi kuu basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 47  lilikuwa na abiria  zaidi ya 100 pamoja na mizigo hadi mlangoni 

 Abiria  wa basi la King Cross  wakishuka katika basi hilo kwa shida baada ya  kutakiwa kushuka na askari wa usalama barabarani  ,gari hilo  lishindwa kukata kona kutokana na uzigo wa mzigo hivyo kulazimika polisi kuingilia kati japo abiria  baadhi  walionesha kugoma kushuka
 Hapa abiria  wakiendelea  kushuka katika gari  hilo chini ya usimamizi wa  polisi
 Baadhi ya abiria wakiwa wameshuka katika gari  hilo huku bado likiwa limejaa ,hawa  wote  chini  walikuwemo katika gari  hilo ambalo kwa macho ukiliona ni dogo ila idadi ya abiri  walioingia kweli ..hatari  kubwa
 Umati  wa abiria  walioshuka katika gari  hili lenye uwezo  wa kuchukua abiria 47 pekee

 Askari  polisi  mjini Iringa  wakishusha abiria katika basi la King Cross  linalofanya safari  zake kati ya Iringa - Mkulula Isimani wilaya ya Iringa  vijijini leo baada ya kujaza kupita  kiasi na  kushindwa  kukata  kona  kuingia barabara kuu ya Iringa - Dodoma eneo la Miyomboni

 Huu  ndio  umati mkubwa  uliokuwepo  ndani ya  basi  hilo ambalo lilijaza abiria  kupita  uwezo  wake  pamoja na mizigo ambapo baadhi ya  abiria  walilazimika  kubeba mizigo yao wakiwa ndani ya basi  hilo



 Hili ni Betrii ambalo  lilichomoka baada ya  gari hilo kushindwa  kukata  kona
 Mheshimiwa  diwani Franzisca Kalinga  wa kata ya Malenga Makali (kulia) pia alikuwemo katika  basi hilo

Hapa gari  hilo likipelekwa  polisi chini ya ulinzi mkali wa polisi  huku akibiri  wakitafutiwa basi jingine  zuri .

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...