Wednesday, July 17, 2013

ARSENAL YAENDELEZA MAUWAJI, YAWAFUMUA 7-1 WAVIETNAM

ARSENAL imeendeleza wimbi la ushindi mnono katika mechi za kujiandaa na msimu, baada ya  kuifumua mabao 7-1 Vietnam XI kwenye Uwanja wa My Dinh mjini Hanoi.
Ushindi huo umemoa majibu kadhaa kocha Arsene Wenger, kwanza kama atashindwa kusajili mshambuliaji wa kiwango cha dunia kabla ya mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa, Olivier Giroud atatosha kwenye kampeni ya ushindi baada ya kufunga mabao matatu peke yake.
Pili, anaweza kumtumia Bacary Sagna katika beki ya kati itakapotokea dharula kama atakwama kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams baada ya beki huyo kulia wa Arsenal kucheza namba nzuri .
Na tatu, inayoweza kuwa muhimu kuliko zote, Jack Wilshere na kama yuko fiti kabisa kuanza msimu, baada ya kucheza mechi yake ya kwanza  tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo cha mguu Mei.
Shukrani! Wachezaji wa Arsenal wakiwa wamebeba bango la 'Asanteni' kwa ajili ya mashabiki baada ya kuwafunga Vietnam
 Shughuli: Beki wa Arsenal, Bacary Sagna akiupitia mpira miguuni mwa Nguyen Anh Duc wa Vietnam

Mbali na mabao matatu ya Giroud, mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain, Chuba Akpom mawili na Ignasi Miquel ambao wote walifunga pia kwenye ushindi wa 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dream Team ya Indonesia.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk71, Sagna/Aneke dk71, Jenkinson/Olsson dk71, Koscielny/Mertesacker dk46, Gibbs/Miquel dk46, Arteta (Nahodha)/Ramsey dk46, Rosicky/Zelalem dk46, Oxlade-Chamberlain/Wilshere dk66, Gnabry/Walcott dk46, Podolski/Miyaichi dk46 na Giroud/Akpom dk46

Olivier Giroud akifunga moja ya mabao yake 

RATIBA YA MECHI ZA ARSENAL KUJIANDAA NA MSIMU

Julai 14 na Indonesia XI walishinda 7-0
Julai 17 na Vietnam wameshinda 7-1
Julai 22 na Nagoya Grampus (Uwanja wa Toyota, Japan) Saa 5.30 asubuhi
Julai 26 na Urawa Red Diamonds (Uwanja wa Saitama, Japan - Kombe la Saitama City) Saa 5.30 asubuhi
Agosti 3 na Napoli (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 4 na Galatasaray (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 10 na Manchester City (Uwanja wa Olimpiki, Helsinki) Saa 9 jioni

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...