Monday, January 28, 2013

HABARI NA PICHA ZA MATUKIO YANAYOTOKEA MTWARA, SOMA UPATE UNDANI ZAIDI. BOFYA HII LINK

.
POLISI jana wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima katika kata ya Chikongola Manispaa
ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake, huku mwandishi wa habari mmoja wa Channel 10 akiripotiwa kujeruhiwa.Habari ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa polisi mkoani ni kwamba zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na
kuanza kutembeza mkong’oto kwa wananchi ili kuzima vuguvugu hizo.
Mwandishi wa hizi habari lipojaribu kuwasiliana na kamanda Nzuki kwa njia ya simu za mkononi hakuweza kupatikana lakini kwenye line nyingine ni kwamba wananchi walitoa tuhuma hizo baada ya kukuta ungo ikiwa na tunguri ndani yake
ambayo inadaiwa kuwa ni ndege ya wachawi uwanjani kwake maeneo ya makaburi Msafa.
Wananchi walijikusanya nyumbani kwa Diwani huyo na kumshinikiza awatoe wachawi nje ili waweze kuwaadhibu amri
iliyopingwa na Diwani huyo, muda ulivyozidi kwenda ndivyo wananchi walivyozidi kuongezeka na hatimaye kulijitokeza kundi la watu walioanza kutia vurugu hali iliyomlazimu Chehako kuomba msaada wa polisi.
Mashuhuda wa tukio walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa polisi walipofika waliwasihi wananchi kutawanyika kwa kuwa ungo na tunguri zake zilikuwa zimeteketezwa kwa moto na diwani huyo mbele ya wananchi hao.
Chenako akihojiwa nyumbani kwake alisema Wananchi waliendelea kupinga na kudai ndani ya nyumba kuna rubani na abiria wa ndege amewahifadhi… polisi wakawachagua wananchi watano na kuingia ndani ya nyumba kuwasaka watu hao lakini hawakuona kitu, walitoka nje na kuwambia wenzao lakini hawakukubali, walianza kurusha mawe kwenye nyumba ndio polisi wakaanza kupambana nao kwa kuwarushia mabomu.
Chehako alibainisha kuwa ni kawada yake kuamka alfajiri kwa ajili ya sala ya
asubuhi, lakini asubuhi ya jana alishindwa kuamka mapema, hata hivyo
hakuweza kuhisi jambo lolote.
Katika mapambano hayo ya wananchi na polisi wananchi kwa kutumia mawe wamemjeruhi Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Mtwara John Kasembe kwa jiwe kichwani, pia Ofisa mmoja wa polisi ambae hakutaka kutajwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba gari moja ya polisi PT 1421 limevunjwa kioo cha mbele kwa mawe.
Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
Wakiwa katika mahakama ya mwanzo Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba
mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi. (Taarifa imeandikwa na mtwarayetu.blogspot.com)
Mahakama ya Mwanzo.
Mwandishi aliejeruhiwa.
.
.
Picha zote ni kutoka kwenye camera ya mtwarayetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...