Bale ndiye mchezaji ghali zaidi kwa sasa baada ya Real kumnunua kwa pauni86milioni kutoka Spurs.
Madrid, Hispania. Barcelona walitumia busara kubwa
 kuanza kumtumia Neymar katika wiki ya kwanza ya La Liga msimu huu na 
Real Madrid wanaonekana watafuata sera hiyo kwa Gareth Bale, pamoja na 
kuwa na majeruhi wengi kwa sasa.
Klabu hiyo tajiri, kwa sasa ina pointi tisa sawa na mabingwa Barca katika mechi tatu.
Real wametumia euro 100 milioni kwa kumsajili Bale ambaye wamepanga kumtumia leo dhidi ya Villarreal.
Winga huyo mwenye miaka 24, alicheza dakika 30 tu 
akiwa na Wales kwenye mchezo wa kusaka kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi 
ya Serbia siku ya Jumanne, kocha Chris Coleman ametahadharisha kuwa 
utayari wa mchezaji huyo.
Bale aliwaambia wanahabari Alhamisi kuwa “nipo vizuri ni matumaini yangu nipo tayari kucheza Madrid.
“Ni wazi nipo nyuma ya wenzangu kwa utayari wa mwili, lakini nafikiri naweza kucheza,” alisema Bale.
Villarreal, pamoja na Atletico Madrid ndizo timu 
pekee zilizoshinda katika michezo yote mitatu, hivyo leo watakuwa 
wakijaribu ubora wa safu yao ya ushambuliaji dhidi ya Real.
Mabingwa watetezi Barca wanahabari njema kuelekea 
mchezo wake wa leo nyumbani dhidi ya Sevilla, wakati kiungo wake Sergio 
Busquets na beki Daniel Alves wote wamerejea katika kikosi hicho.
Neymar na mwanasoka bora wa dunia, Lionel Messi pia wamereja wakiwa fiti baada ya kuziongoza Brazil na Argentina kushinda.
Kocha Barca, Gerardo Martino amekuwa akimtumia 
Neymar kwa baadhi ya michezo, alicheza dakika zote 90 waliposhinda 3-2 
dhidi ya Valencia.
Nyota huyo mwenye miaka 21, alionyesha kiwango cha
 juu akiwa na Brazil ilipocheza dhidi ya Australia na Ureno, akifunga 
bao moja kila mechi.
 
 
No comments:
Post a Comment