Tuesday, September 24, 2013

KWA GHARAMA HIZI ZA USAJILI TUTEGEMEE NINI LIGI KUU ENGLAND, JE TIMU YAO YA TAIFA ITABOMOKA AU KUIMALIKA?



TULIJUA  England wako hatarini kufuzu kushiriki kwenye Kombe la Dunia, tulijua timu ya vijana chini ya miaka 21 ya England haitavuka hatua ya Makundi katika michuano ya Ulaya wakati wa kiangazi – walifungwa mechi zote tatu wao wakifunga bao moja tu.
Tulijua timu ya vijana ya England chini ya miaka 20 itafanya vibaya wakati wa michuano ya dunia Uturuki na kabla ya kutoka katika hatua ya makundi. Timu ya England chini ya miaka 20 haijawahi kushinda mechi tangu wakati Jamie Carragher na Michael Owen walipoichezea mwaka 1997.
Move over Brits: Brendan Rodgers failed to sign a single domestic player in the summer
Kaa pembeni Waingereza: Brendan Rodgers hajasajili hata mchezaji mmoja wa nyumbani wakati wa kiangazi
Manuel Pellegrini
Arsene Wenger
Tunacheki pembeni: Manuel Pellegrini na Arsene Wenger wameamua kuamini vipaji vya nje.

Klabu ambazo hazijanunua Waingereza

Arsenal  (wametumia pauni mil 42.5 kwa wachezaji wanne)
Chelsea (wametumia pauni mil 65.5 kwa wachezaji nane)
Liverpool (wametumia pauni mil 23.3 kwa wachezaji nane)
Manchester City (wametumia pauni mil 94.9 kwa wachezaji watano)
Manchester United (wametumia pauni mil 28.5 kwa wachezaji wawili)
Newcastle (Hajatumia kitu, wachezaji wawili, japokuwa mkopo wa Loic Remy ni pauni milioni 2)
Southampton (wametumia pauni mil 35.5 kwa wachezaji watatu)
Stoke (wametumia pauni mil 7 kwa wachezaji sita)
Tottenham (wametumia pauni mil 97.5 kwa wachezaji saba)
NB: Everton na West Brom wamesajili wachezaji wawili tu wa England kwa mkopo (Gareth Barry na Scott Sinclair)
Lakini usajili wa majanga kwenye soka la England unazidi kuwa kwenye hali mbaya, BIN ZUBEIRY inaangalia jinsi ambavyo klabu za Ligi Kuu England zinawapotezea wachezaji wazawa.
Klabu zimefanya usajili wa jumla ya wachezaji 150 wakati huu wa kiangazi, ni 34 tu (asilimia 22.66) kati ya 150 ndiyo Waingereza.
Chakusikitisha zaidi klabu sita kati ya saba ambazo zimemaliza kwenye saba bora msimu uliopita - Manchester United, Manchester City, Chelsea, Arsenal, Tottenham, Liverpool  – zote hazijasajili mchezaji hata mmoja wa Kiingereza.
Everton, ambayo ilimaliza nafasi ya sita imesajili mchezaji mmoja wa England, Gareth Barry tena kwa mkopo – hii inaonyesha ni jinsi gani vipaji vya wazawa vinakazi kutoka.
Kwa upande wa Fulham, ambao huwa wanachukua wachezaji wa mataifa mbalimbali wamenunua wachezaji wawili wa England - Darren Bent (29) ambaye alishindwa kuvuma Aston Villa na Scott Parker (32) umri umemtupa mkono.
Belgian: Marouane Fellaini was David Moyes only major signing in he transfer window
Mbelgiji: Marouane Fellaini alikuwa usajili mkubwa wa David Moyes kwenye dirisha hili la usajili.
£15.5million: West Ham's Andy Carroll was the most expensive Englishman bought in the transfer window
Pauni mil 15.5: staa wa West Ham, Andy Carroll alikuwa mchezaji wa Kiingereza mwenye thamani kubwa zaidi wakati huu wa kiangazi.
Steven Caulker
Swansea City's English midfielder Jonjo Shelvey
Wamenunuliwa: Steven Caulker na Jonjo Shelvey walihnunuliwa kwa pauni mil 9 na pauni mil 6

Wachezaji wa England walionunuliwa wakati wa kiangazi

Aston Villa - Jed Steer
Cardiff - Steven Caulker, Simon Moore, John Brayford
Crystal Palace - Dwight Gayle, Jack Hunt, Jerome Thomas, Kevin Phillips, Jason Puncheon (mkopo), Neil Alexander, Steven Dobbie, Barry Bannan
Everton - James McCarthy, Gareth Barry (mkopo)
Fulham - Scott Parker, Darren Bent (mkopo)
Hull - Tom Huddlestone, Curtis Davies, Steve Harper, Danny Graham (mkopo), Jake Livermore (mkopo), George Boyd, Allan McGregor
Norwich - Nathan Redmond, Carlo Nash, Gary Hooper
Sunderland - Duncan Watmore
Swansea - Jonjo Shelvey, Jernade Meade
West Brom - Scott Sinclair (mkopo), Lee Camp
West Ham - Andy Carroll, Danny Whitehead
Katika ya klabu zilizosajili waingereza ni Swansea, Sunderland, Aston Villa na West Brom wachezaji hawako kwenye akili za makocha.
Michael Laudrup amesajili wachezaji 10 wawili tu kati yao ni waingereza Jonjo Shelvey na Jernade Meade, kinda kutoka Arsenal.
Paul Lambert, msimu uliopita alisifika sana kwa kuwapa nafasi Waingereza kama Matt Lowton na  Ashley Westwood, lakini safari hii ameenda kusajili wachezaji sita kutoka nje na mmoja tu wa England Jed Steer kipa wa vijana chini ya miaka 19 kutoka Norwich. 
Paulo Di Canio amesajili wachezaji 14 – mmoja tu Muingereza ambaye anamiaka 19 Duncan Watmore kutoka klabu isiyokuwa na ligi ya Altrincham. 
Asilimia 50 ya wachezaji wa wazawa waliosajiliwa wakati huu wa kiangazi wamesajiliwa na timu zilizopanda daraja.
Na wachezaji hao ni wale ambao wanahaha kufufua vipaji vyao. Tom Huddlestone na Jake Livermore pale Hull, wanahaha kurudisha vipaji vyao baada ya kuuzwa na Spurs, na hawapo hata kwenye akili ya Roy Hodgson wakati Danny Graham alichemka Sunderland na sasa anajaribu bahati yake kwenye uwanja wa KC. 
From Russia with love: Willian cost Chelsea £32million from Anzhi Makhachkala
Kutoka Urusi: Willian ameigharimu Chelsea pauni mil 32 kutoka Anzhi Makhachkala
Tottenham Hotspur's Paulinho
Fernandinho
Muhimu: Wabrazil Paulinho na Fernandinho ni mfano kwa klabu kubwa kutoka

Umri tatizo England

35 - Frank Lampard
33 - Steven Gerrard
32 - Ashley Cole, Michael Carrick
31 - Phil Jagielka, Rickie Lambert
30 - Jermain Defoe
29 - Glen Johnson
28 - Leighton Baines, Ashley Young
27 - Wayne Rooney, Gary Cahill, James Milner
26 - Joe Hart, John Ruddy
25 - Fraser Forster
24 - Theo Walcott, Tom Cleverley
23 - Chris Smalling, Kyle Walker, Daniel Sturridge
22 - Andros Townsend, Danny Welbeck
21 - Phil Jones, Jack Wilshere, Steven Caulker
19 - Ross Barkley
18 - Raheem Sterling 
Kevin Phillips, Jerome Thomas na Jason Puncheon wametua Crystal Palace ni bora zaid kwa klabu hiyo. Simon Moore kipa namba mbili wa Cardiff, ametoka klabu ya daraja la kwanza ya Brentford. 
Idadi inathibitisha tatizo linalohatarisha fursa za wachezaji wa England wa kizazi cha sasa na kijacho.
Mwenyekiti mpya wa FA, Greg Dyke, amechukua nafasi ya David Bernstein na ni rahisi kwa wachambuzi kuandika kutaka kuona mabadiliko. Timu ya taifa ya England inasimamiwa na FA na chama hicho kinatakiwa kulinda mustakabali wa wachezaji wa England.
Sheria yoyote itakayotungwa inaweza kuingiliwa na sheria za soka za Ulaya, mfano wakiamua kuweka sheria ya kutumia wachezaji sita wa England katika kila mechi sheria za Ulaya zitatengua hilo.
Ukweli ambao ni mgumu kuukubali ni kwamba Ligi Kuu England ni ligi ya dunia na FA imeshazidiwa nguvu. Tangu ilipojitenga mwaka 1992 na kuzubaa kwa FA imeruhusu ligi hiyo kuwa juu zaidi kwenye soka la England.
Veteran: Frank Lampard is the oldest member of the current England squad at 35
Babu: Frank Lampard ndiyo anaumri mkubwa zaidi kwenye kikosi cha sasa cha England miaka 35.

Kadiri mikataba minono ya matangazo inavyozidi kuingiwa ni pigo kwa Ligi Kuu na Klabu zake. Timu zinakuwa zikihaha kufanya biashara zaidi na FA inabaki ikiangalia nidhamu tu.
Maendeleo ya wachezaji wa England yako mikononi kwa klabu za ligi kuu. Lakini sasa hivi hawaaminiki tena, klabu zimezidi kujuza watoto kutoka nje ya England kwenye timu zao za vijana.
Ross Barkley
Raheem Sterling
Sura mpya: Ross Barkley (19) na Raheem Sterling (18) ndio wachezaji makinda zaidi kwenye kikosi cha England.

Na wakati huu ligi inaingia kwenye msimu mpya timu ya taifa sasa mashabiki wa England wanaachwa wakiwa na hofu juu ya mustakabali wa muundo wa timu yao ya taifa siku zijazo.
Hatari zaidi iko kwa Wales ambao safari hii hakuna hata mchezaji mmoja aliyesajili wa timu za ligi kuu, lakini Gareth Bale anawabeba kwa kwenda Hispania.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...