Ligi kuu ya England imeendelea hii leo kwa michezo iliyopigwa kwenye viwanja nane ambapo timu 16 zilikuwa uwanjani .
Katika
mchezo wa kwanza mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester United
waliwafunga vijana waliopanda daraja Crystal Palace mabao mawili bila .
Mabao
ya United kwenye mchezo huo yalifungwa na Washambuliaji Robin Van
Persie na Wayne Rooney.Robin Van Persie alifunga bao lake baada ya
mwamuzi kuizawadia United Penati kufuatia kiungo Ashley Young kuangushwa
na kiungo wa kimataifa wa Afrika Kusini Kagisho Digkacoi ambaye
alionyeshwa kadi nyekundu huku Wayne Rooney akifunga kwa mpira wa adhabu
ndogo toka umbali wa mita 30.
Kwingineko Arsenal waliwafunga Sunderland 3-1
katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Sunderland The
Stadium Of Light . Arsenal walianza kufunga bao lao kwneye mchezo huo
kupitia kwa mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud ambaye hii leo
amefunga bao lake la nne kwenye ligi kuu msimu huu akipata pasi toka kwa
Mesut Ozil ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza . Sunderland
walisawazisha bao hilo kupitia kwa kiungo Craig Gadner kwa mkwaju wa
penati baada ya beki wa Arsenal Laureant Koscielny kumchezea rafu
mchezaji wa Sunderland . Arsenal walirejea mchezoni na kuongeza mabao
mawili ya haraka yaliyofungwa na kiungo Aaron Ramsey.
Newcastle
United waliwafunga Aston Villa 2-1 huku wafungaji wakiwa Hatem Ben Arfa
na Yoan Goufran kwa Newcastle na Christian Benteke akifunga bao pekee
la Villa.
Tottenham
Hotspurs waliwafunga Norwich City 2-0 . Mabao ya Spurs yalifungwa na
Gylfi Siggurdson ambaye alifunga mabao yote mawili.
Mechi
ya Hull City na Cardiff City timu mbili ambazo zimepanda daraja msimu
huu iliisha kwa sare ya 1-1 . Hull walianza kufunga kupitia kwa Curtis
Davies kabla ya Peter Wittingham hajaisawazishia Cardiff City kwenye
kipindi cha pili .
Fulham
na West Bromwich Albion nao walitoka sare ya 1-1 . Wafungaji kwenye
mchezo huo walikuwa Steve Sidwell kwa Fulham na Gareth McAuley kwa West
Brom.
Chelsea walipoteza
mchezo wao wa kwanza chini ya kocha Jose Mourinho baada ya kufungwa na
Everton 1-0 . Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na kiungo Steven
Naismith ambaye leo (jumamosi)alikuwa anasherehekea siku yake ya
kuzaliwa .
Mchezo kati ya Manchester City na Stoke City uliopigwa huko Brittania Stadium uliisha kwa sare ya bila kufungana.
Matokeo ya Mechi Za Ligi Kuu Ya England.
Manchester United 2-0 Crystal Palace .
Aston Villa 1-2 Newcastle United .
Tottenham 2-0 Norwich City .
Sunderland 1-3 Arsenal.
Hull City 1-1 Cardiff City .
Fulham 1-1 West Bromwich Albion.
Stoke City 0-0 Manchester City.
Everton 1-0 Chelsea.
No comments:
Post a Comment