WENYEKITI wa Kamati ya Umoja wa
Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa, ameutaka uongozi wa
Shirikisho la Muziki Tanzania, kumchukulia hatua ya kinidhamu, msanii wa
muziki wa mduara Shilole ambaye pia ni muigizaji wa filamu kwa kosa la
kukiuka maadili ya Tanzania katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani
Iringa.
Shilole alipanda jukwaani akiwa anacheza
wimbo wake wa ‘Nakomaa na jiji’ huku akiwa amevaa nguo ambazo
zilionesha maumbile yake yote ya mwili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Billa
alisema Shirikisho la muziki chini ya rais wake, Addo Novemba wanatakiwa
kuchukua hatua zaidi juu ya shilole kwa kosa la kuwadhalilisha wanawake
ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ya Tanzania.
“Hatukatai hayo mambo yapo lakini kwa
staili ile sisi kama viongozi wa sanaa hatutaweza kuvumilia, shirikisho
la muziki wakishindwa kutekeleza hili lazima kamati ilivalie njuga swala
hilo, kiukweli wanalidhalilisha taifa hawa wasanii, mbona wanaume
hafanyi shoo zao uchi,? Alihoji Billa.
Alisema shirikisho la muziki liige mfano
wa shirikisho la filamu kama lilivowaonya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel
kwa makosa kama hayo, ambapo anamini kwaasilimia kubwa kunachangia kuwa
na nidhamu wanapopanda jukwaani.
“Angekua
ameenda kwa shughuli za filamu wangelifanya wao lakini hili shirikisho
la muziki wanatakiwa wakae meza moja na Shilole kulizungumzia hilo, wao
wanakua wazito kuwachukulia hatua wasanii wa muziki kuliko filamu lakini
kwa hili haitawezekana, ,” alisema.
No comments:
Post a Comment