Wednesday, March 27, 2013

HII NI BALAA SASA, WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WALIOKATA RUFAA NA KUTAKA MITIHAN YAO ISAHIHISHWE TENA WAMEFELI ZAIDI YA MARA YA KWANZA. KWA UNDANI ZAIDI BOFYA HII LINK


.
Tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea kufanya kazi, imefahamika kwamba wanafunzi takribani elfu kumi waliokata rufaa ili mitihani yao isahihishwe upya, wamefeli zaidi baada ya kusahihishwa na bado NECTA imetoa muda zaidi kwa wengine wanaotaka kufanya hivyo.
Taarifa iliyoripotiwa na Nipashe imesema taarifa za ndani za baraza la mitihani la Taifa (NECTA) na wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa, wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata mwanzoni.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya NECTA vilizungumza na gazeti la NIPASHE kwamba mitihani kwa wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa March 12 2013 na kuhitimishwa March 15 2013 ambapo wengi wamefeli zaidi.
.
.
Mmoja wa watu kwenye timu ya NECTA amekaririwa akisema “baada ya Wanafunzi kadhaa kukata rufaa NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo yote na kuanza kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa umakini, kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli kimeongezeka”
Katibu mtendaji wa NECTA Dr. Joyce Ndalichako alithibitisha kuwa mitihani ya Wanafunzi waliokata rufaa imesahihishwa kweli, ila hana taarifa kama matokeo ya wanafunzi hao yanaonyesha wengi wamefeli zaidi kwa sababu alikua safarini kikazi lakini kasema swala la kufeli zaidi kwa Wanafunzi waliokata rufaa linawezekana kwa sababu kila mwaka limekua likijitokeza hivyo ni la kawaida.
Stori imeandikwa na http://mjengwablog.com/ kutoka gazeti la Nipashe.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...