Friday, March 29, 2013

JENGO LAANGUKA JIJINI DARESAALM: RAIS AZURU MAHALI JENGO LILIPOANGUKA HUKU UOKOAJI UKIENDELEA. KWA TAARIFA ZA PICHA ZA JENGO HILO BOFYA HII LINK


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.  
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri. 
 
 Raisi Jakaya Kikwete Akiangalia Jinsi zoezi la Uokoaji linavyoendelea mara baada ya kuwasili kwenye eneo la tukio katika Mtaa wa Zanaki na Hindra Ghandi
 2Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova kulia akizungumza jambo na Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia ambaye ameungana na wananchi wengine katika tukio hilo.

 Wananchi wakiendelea na zoezi la uokoaji katika eneo la tukio mapema ya leo
 Baadhi ya wakazi wa jiji la dar wakifunga minyororo kwenye moja ya kontena lililofukiwa na vifusi baada ya jengo la ghorofa 15 kuporomoka
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiwa katika zoezi la uokoaji
 1
Madaktari wa kujitolea wakimhudumia mmoja wa majeruhi waliyeokolewa kwenye ghorofa lililopolomoka leo asubuhi.
 Usalama uliimarishwa kila kona ya eneo la tukio huku askari wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi wakifanya kazi yao ipasavyo
 Askari wakifanya kazi yao kuhakikisha usalama unakuepo
 Wananchi wakiendelea na zoezi la kuondoa kifusi kwaajili ya kuokoa watu waliofukiwa na vifusi
 Gari likitolewa baada ya kuangukiwa na vifusi mara baada ya jengo la ghorofa 15 kuanguka
 Vijana Wa JKT wakiendelea na zoezi la uokoaji katika eneo la tukio

 Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wakibadilishana mawazo kuhakikisha zoezi linaenda vizuri
Zoezi la Uokoaji likienda huku greda zikifanya kazi ya kusomba vifusi
Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia zoezi la uokoaji kutoka Vikosi vya Uokoaji na wananchi waliojitolea kuokoa uhai wa wenzetu.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...