Thursday, March 28, 2013

NZIGE NI BALAA WAVAMIA MAZAO KIASI CHA KUWEZA SABABISHA JANGA LA NJAA. JE NI WAPI HUKO PATA UNDANI ZAIDI KWA KUBOFYA HII LINK

 
Wananchi wanahofia kuwa huenda wakakumbwa na njaa baaada ya mabilioni ya Nzige kuvamia Madagascar

Nzige wamevamia eneo kubwa la Madagascar na kutishia mimea pamoja na kuzua wasiwasi kuhusu upungufu wa chakula.
Kwa mujibu wa shirika la chakula la umoja wa mataifa, (FAO) mabilioni ya mimea iliharabiwa na nzige hao na huenda asilimia sitini ya wananchi wakakumbwa na njaa.
Takriban dola milioni 14.5 inahitajika kukabiliana na janga hilo katika nchi ambayo watu wake wengi ni maskini.
Ni janga mbaya zaidi kuwahi kukumba kisiwa hicho tangu mwaka 1950, kwa mujibu wa FAO.
Mtaalamu wa kupambana na nzige, Annie Monard, aliambia BBC kuwa janga hilo ni tisho kubwa kwa kisiwa hicho cha bara hindi.
"janga la mwisho kama hili kuwahi kutokea ilikuwa miaka ya hamsini na kudumu kwa miaka 17 kwa hivyo ikiwa hakuna hatua zitakazochukuliwa basi huenda ikachukua miaka mitano au kumi kukamilika,'' alisema mtaalamu huyo.
Takriban asilimia 60,ya watu milioni 22 wa kisiwa hicho, huenda wakakumbwa na njaa.
Kwa sasa takriban nusu ya nchi imeathirika kutokana na nzige hao, kulingana na shirika la FAO.
Shirika hilo linataka, wahisani kuchangisha takriban dola milioni 22 kama msaada wa dharura kwa kufikia mwezi Juni ili kunyunyizia nzige hao dawa.
Janga hili la nzige limetishia mifugo na mchele shambani ambacho ni chakula rasmi cha raia wa Madagascar

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...